mazungumzo walipokutana kaburini

badshah

Member
Mar 16, 2013
51
32
jamaa alipata tetesi kuwa mkewe anaingiza buzi ndani kila anapotoka. siku moja kwa mtego akarudi mapema sana huku akiwa na shauku ya kumfumania mkewe.

lakini hakumuona huyo jamaa, lakini alimuona mkewe akiwa na wasiwasi sana hivyo hali hiyo ilimfanya aamini kuwa anachoambiwa ni kweli, hivyo akaanza kutafuta kona zote ndani ya nyumba bila mafanikio.

kutokana na hali ya hasira, presha ikampanda na kufariki palepale. sasa huko kaburini akakutana na mtu mmoja na mazungumzo yakawa kama ifuatavyo:

Mtu: he! vipi mwenzangu imekuaje tena ghafla hivi?

Mume: dah nilitaka kumfumania mke wangu lakini nilipojitahidi kumtafuta anayeniibia sikufanikiwa na kutokana na hasira nikapata mshtuko wa moyo.

Mtu: Dah pole sana wewe ungefungua ndani ya friji ungenikuta, ona sasa nimekufa kwa baridi humo, ungenipata tungeyamaliza hukohuko tusingefika hapa!
 
Back
Top Bottom