DOKEZO Mazao ya chakula yasiuzwe nje ya Nchi, hali ni mbaya sana. Serikali zuieni haraka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mleta hoja huenda ana wazo jema.
Bei imepanda (mkulima kapandishwa mshahara) mnaleta marufuku.
Mbona hatuwaoni mkileta hoja hizi mazao yanapokosa soko?

Vija wengi walikuwa wamechangamkia kilimo.
Sasa mnataka wakichukie tena.

Siamini kuwa kwa utaratibu huu iwapo BBT italeta matunda tunayoyatarajia.

Uamuzi ni wenu.
Wakulima hatuandamani na hatuna chama cha kututetea kama walivyo Wafanyakazi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Dogo acha uchawi kama maisha ya town yamekushinda rudi bush, hapa mjini chakula hakijawahi kukosekana sokoni na wakulima wanafurahia bei nzuri ya mazao yao.
 
Haya Kipapi yangu nayatoa keshokutwa halafu nayaweka bei ikipanda mniambie ndo niuze hadi debe lifike Hamsini elfu. Wewe mleta sledi kalime Yako na wewe seeeh!
 
Mtatufidia wakulima?

Nimelima bila msaada wenu wala wa serikali, nimevuna kwa kulala shambani kwenye baridi wiki nzima halafu unataka nizuiwe kulima.

Hivi zinawatosha kweli? Napokea iliyo halali yangu. Ukikinga mwisho wa mwezi mbona sikuzuii?
ila mbolea ikipanda Bei mnaililia serikali itoe ruzuku hivi pesa za ruzuku ni Kodi yako peke yako
 
Ukweli kwa sasa ni huu,

Kutokana na dunia kuwa na mvua chache, na ukanda wa Afrika pia kuathiriwa ni vyema sasa mazao yafuatayo yawekewe zuio la kuuzwa nje ya nchi ili kujihakikishia usalama wa chakula na kulinda soko la ndani.

Mchele, mahindi, muhogo, maharagwe, njegere, choroko, mtama mweupe na kadhalika. Mataifa mengi afrika yameweka zuio na mengine yameanza kutangaza hali ya hatari sababu ya njaa.

Mavuno yalikua kidogo na idadi ya watu imeongezeka maradufu. Wakati ambapo waziri wa kilimo anapambana na project za umwagiliaji na bado hatujakomaa kwenye umwagiliaji ili kua na uwezo wa kuvuna mazao misimu yote kwa mwaka tuchukue hatua hizo kwa sasa.

HAKUNA AMANI YA NCHI KAMA CHAKULA HAKITOSHI.
Jitahidi kuwa na hela tu, njaa za siku hizi ni pesa tu hakuna kufa tena kwa njaa kama zamani kwa kukosa cha kununua
 
Wakulima wa miaka hii ni wasomi, sio wa kipindi cha Nyerere, wengi wanahifadhi mazao na wanauza kwa malengo,
.
20230521_192807.jpg
 
Mazao Sio Mali ya Serikali msiwatupie mzigo wakulima kwa sera zenu mbovu kuhusu kilimo.
Mkulima auze popote penye faida
 
Back
Top Bottom