Mawaziri kufukuzwa, upande wa pili.

JEKI

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
4,845
2,938
Mimi ni kati ya waumini wa uwajibikaji, nashangaa hata waziri mkuu kubakia madarakani. Tuyaache hayo, hivi wakati tunasherekea tunajua upande wa pili wa majangili? Naamini nao wanasherekea na nionavyo huenda walikuwa na mkono wao, tunaambiwa hata baadhi ya wabunge wanahusika na ujangili.

Je katika operesheni hii, haiwezekani majangili nao walipenyeza ushawishi kwa watendaji ili kuiharibu operesheni hii ili ionekane isiyo na maana zaidi ya kuonea watanzania tu? Katika nchi yetu lawezekana kabisa, tujiulize nini hatima ya operesheni tokomeza? Nashauri iendelee ila mawaziri wajao wahakikishe wanafanya close supervision ili wawashughurikie mapema wanaoiharibu.

Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Naunga mkono hoja ya kuendeleza OPERATION TOKOMEZA lakini kwa kufuata sheria za nchi!!
 
Na tatizo majangiri wengi ni vigogo wenyewe au watu wenye mahusiano ya karibu na wbunge wetu wenyewe,ni vigumu kuamini kama kilichopiganiwa ni haki,maslahi na utu wa mtanzania au ndo mbinu mbadala ya kuua op.iyo
 
Back
Top Bottom