Mawasiliano ya Siri, Ishara na Dalili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,405
52,046
MAWASILIANO YA SIRI, ISHARA NA DALILI

Na, Robert Heriel.

Jumbe hii isomwe kwa hekima kwao hao wenye hekima, tena wenye ufahamu wazidi kupata maarifa, lakini isomwe kipumbavu kwa hao wenye upumbavu, tena wasipate maana, bali wasomapo waanguke kwenye njia panda za fikra zao.

Niite Taikon wa Fasihi, Mwana kutoka Nyota ya TIBELI, huko ilipo Sayari ya JIBI, nyota yenye mbawa mbili ipaayo kutoka ulimwengu uliomashariki hata magharibi, tena izungukayo kama upepo wa kusini uendao Kaskazini.

Ashukuriwe yeye aliyetupa mambo madogo haya, bila gharama, nasi kwa neema yake tunatoa bure, kwa maana kila kilichotolewa bure kitolewe bure, na kile chenye gharama kitolewe kwa gharama.

Hakuna ajali, kila kitu kinatokea kwa makusudi. Hakuna jambo linalokuja bila taarifa, kila jambo huja kwa taarifa.

Taarifa huwasilishwa kwa njia ya mawasiliano. Kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kutoka kwa mhusika mmoja kwenda kwa mhusiika mwingine.

Mawasiliano ni kitendo cha kupashana habari au taarifa. baina ya wahusika. Wahusika ni viumbe wote hai na wafu waliopo duniani na wasiokuwepo duniani. Mawasiliano ndio msingi wa usalama wa maisha ya kiumbe chochote hapa duniani na nje ya dunia.

AINA ZA MAWASILIANO
Nimegawa aina kuu tano za Mawasiliano
1. Mawasiliano ya Sauti
2. Mawasiliano ya Maandishi, michoro, picha, namba
3. Mawasiliano ya Mijongeo
4. Mawasiliano ya Ishara, Dalili na Alama.
5. Mawasiliano ya nguvu za Kiroho

1. MAWASILIANO YA SAUTI
Haya ni mawasiliano ambayo wahusika hupeana taarifa, hupashana habari kwa kutumia mitetemo ya sauti, mipangilio ya sauti, mivumo na mingurumo ya sauti.

Katika aina hii kuna mambo yafuatayo;
1. Lugha (Hii hutumiwa na binadamu, na viumbe vyote vyenye ala za sauti zinazoruhusu lugha kusemeka)
2. Mingurumo
3. Mikwaruzo
4. Mitetemo
5. Mivumo
6. Milio n.k

Kupitia sauti wahusika huwasiliana na kupeana taarifa na habari kuhusu jambo fulani

2. MAWASILIANO YA MAANDISHI, MICHORO, PICHA NA NAMBA.
Haya ni mawasiliano ambapo wahusika hupeana taarifa kupitia maandishi, michoro, picha na namba. Wahusika wanaotumia mawasiliano haya mara nyingi ni wanadamu, na viumbe wasioonekana wenye asili ya ubinadamu
Lugha ya maandishi inahusika, Ramani, Calenda n.k

3. Mawasiliano ya Mijongea
Haya ni mawasiliano ambayo wahusika hupeana au hupashana habari au taarifa kwa kupitia mijongea ya kimwili na kimaumbile. Wapo viumbe ambao mijongea yao hutoa taarifa fulani, hujaribu kupasha habari fulani. Habari hizo huweza kuwa muda, majira, matukio n.k
kWA MFANO kiumbe ''JUA'' ni nyota ambayo inaonekana inajongea kutoka mashariki kuelekea magharibi kutokana na Dunia kujizungusha. Mjongea huu wa Jua hutoa taarifa ya muda. Pia zipo nyota ambazo usiku hutembea ambazo zikionekana humaanisha jambo fulani.

Pia wapo wanyama, au ndege, au wadadu wanapojongea kutoka sehemu moja hutoa taarifa kuhusu jambo fulani linalokuja.

4. MAWASILIANO YA ISHARA, DALILI NA ALAMA.
Haya ni mawasiliano ambayo wahusika hupeana taarifa kwa njia ya ishara, dalili na alama.
Zipo alama za kijeshi, alama za barabarani, alama za hospitalini, n.k hapa ni kibinadamu
Kwa wanyama, nao wanaalama zao, kwa mfano, wanyama jamii ya Mbwa, simba, chui huweka alama zao kwa kukojolea kwenye mipaka yao. Hizi hufanywa na madume. Hivyo mnyama mwingine akifika eneo lililowekewa alama ya mkojo ya mnyama mwingine hujua eneo hili lipo chini ya utawala fulani
Dalili na ishara za hali ya hewa, kimwili, na kimatukio.
Mtu kabla hajaumwa lazima kuwe na dalili kwenye mwili wake, hii ni kumpa taarifa kuwa kuna kitu kinaendelea ndani ya mwili wake.

5. Mawasiliano ya Nguvu za Kiroho
Haya ni mawasiliano ya siri yanayofanywa katika falme za kiroho na Binadamu.
Mwanadamu ili apate mawasiliano haya ni lazima azingatie mambo yafuatayo:
1. Akubali kwenda kwa waganga wenye viumbe wenye Roho za Utambuzi.
2. Akubali kuingiliwa na viumbe wa Falme za rohoni iwe ni pepo wachafu au Roho watakatifu.
3. Ajiunge kwenye mfumo wa falme za kiroho. Iwe mifumo ya kishetani, kijini au Roho za Mungu.

Kila mwanadamu anaroho, sehemu pekee ambapo mwanadamu anaweza kuwasiliana na falme za Kiroho ni kwenye Ndoto.
Ndoto ni moja ya chombo nyeti muhimu kwa mwanadamu kupokea taarifa za kiroho. Kuhusu maisha ya mtu, nini kitatokea, nini kinaendelea, na nani kilitokea, na nani wahusika wa matukio.

Ndoto huathiriwa na mambo yafuatayo
1. Umri
2. Maovu hasa uzinifu
3. Vyakula
4. Mitindo ya maisha.

1. UMRI
Binadamu yoyote huota. Watoto wadogo ndio huongoza kwa kuota ndoto nyingi na zote zenye maana, ziwe ndoto ya mambo waliyoyaona, waliyoyasikia, au yale yatakayokuja. Watoto huota zaidi kuliko watu wazima.

Ndoto huanza kupungua pale mwanadamu anapofikia umri wa kujielewa na kujitambua. umri wa kuvunja ungo na kubalehe. Pale Mtu anapoanza kutenda dhambi na kutambua hii ni dhambi basi ndipo ndoto huanza kuyeyuka.

2. Maovu hasa zinaa
Roho ya mtu haiathiriki bila kufanya uovu wa kimwili. Mwanaume anapofanya uzinzi na mwanamke anaingia Ubia na roho na huyo anayefanya naye uzinzi.

Utakuwa ni shahidi kuwa, kabla hujaanza zinaa ulikuwa ukiota ndoto nyingi sana. Lakini baada ya kufanya zinaa ndipo uwezo wako wa asili wa kuwasiliana kwa njia ya ndoto ulipoanza kupungua.

Uzinzi ni moja ya njia ya kuunganisha roho. Kumbuka hakuna siri ya watu wawili, hivyo kitendo cha kufanya zinaa na mtu unafanya taarifa zinavuja na pepo wa baya huweza kuziiba au kuzipoteza ndoto hizo usizikumbuke.

Mtu asiyemzinzi ni rahisi kukumbuka ndoto zote alizoziota, kwani hakuna sehemu ya taarifa kuvuja.

Sishangazwi na wapenzi kuota ndoto zinazofanana, hii ni kutokana na mifumo yao ya kiroho kuingia ubia

Ndoto za vyakula ni matokeo ya upungufu wa lishe ndani ya mwili, hizi hutoa taarifa kuwa mwili unaupungufu fulani.

Ndoto za mitindo ya maisha, hizi huwa ni kutokana na mazingira unayoishi, vitu unavyovipenda kuviona, kuvisema, kuvifanya n,k.

Binadamu Hupokea taarifa za maisha yake juu ya kile kinachoendelea au kitakachotokea kupitia mambo yafuatayo

1. NDOTO 70%
2. Mwili 10%
3. Wahusika wa Nje.

1, NDOTO
Asilimia 70 ya kile kinachoendelea kwenye maisha yako umeshakiota, tena hata yatakayotokea mbeleni kwenye maisha yako umeshayaota. Ipo hivi kila siku mtu anapolala usingizi wa masaa kuanzia nane huota ndoto zisizopungua tano.. Shida inakuja kwenye kuzikumbuka na kuzitafsiri. 90% ndoto watu husahau kile walichokiota. Sababu nilishatoa kuwa ni uovu.

Watu wote wanaozikumbuka ndoto zao ni wale wasiokuwa wazinzi. Uzinzi ndio adui namba moja kwa ndoto,

2. MWILI
Mwili huweza kukupasha habari kuhusu jambo fulani bila ya wewe kujua ni jambo gani, je ni jambo zuri au baya, je litatokea muda gani? Hapo ndipo shughuli ilipo
Kila mmoja mwili wake unanamna ya kumpa ishara kuwa kuna jambo fulani linaenda kutokea, kinachofanywa na wengi ni kupuuzia.
Wapo ambapo mioyo yao hushtuka pasiposababu
Wapo ambao siku hiyo huamka hawana amani au wanafuraha wasiojua sababu yake
Wapo ambao mikono yao inawasha, aidha mkono wa kulia au kushoto
Wapo ambao kope zao zinacheza iwe kwenye jicho la kulia au kushoto
Wapo ambao hujikwaa watembeapo kama kiashiria cha jambo fulani
Wapo ambao hujing'ata wanapoongea au kula
Wapo ambao ngozi husisimuka bila ya sababu.

Kumbuka ni lazima ujue kutofautisha masuala ya kiafya na yale yanayotokea kwenye maisha yako.
Ishara zingine ni dalili ya upungufu au maradhi ya mwili, hivyo hiyo ni taarifa kuwa mwili wako unatatizo.

3. Wahusika wa nje
Hapa kuna wahusika wafuatao
1. Binadamu
2. Viumbe hai
3. Hali ya hewa

Unapoongea na watu, iwe kwenye vijiwe, nyumbani, kazini n.k
Fahamu kuwa kuna mmoja kati ya watu hao atakupa ishara ya kitakachotokea mbele yako au kilichotokea nyuma yako. Na hiyo inakuja automatiki, wala hujamwambia, na wala hamzungumzii swala hilo bali unakuta amechomekea tuu.

Je hujawahi kuwa kijiweni ukipiha stori na washikaji/ au mashoga zako alafu ukashangaa mmoja akaongea jambo ulilotoka kulifanya muda mfupi uliopita? Au mmoja akaongea jambo lililokutokea baadaye pindi ulipoondoka.

Mimi mwaka jana, nikiwa kwenye biashara zangu, maeneo ya Goba. Nikiwa nipo nyumbani nikijiandaa kwenda ofisini, rafiki yangu aliyekuja kunitembelea, tukiwa tunaongea mara alichomeka maneno ambayo yalikuwa nje ya kile tulichokuwa tunaongea. Alisema; Leo umechelewa, unawakimbia TRA nini?

Tuliongea kisha nikaondoka. Kufika Ofisini nikiwa nimesahau habari za kauli ya rafiki yangu, mara ghafla naona gari ya TRA Imesimama mbele ya Ofisi yangu. Hapo hapo akili yangu ikakumbuka maneno ya Rafiki yangu kuwa; je ninawakimbia TRA nini?

Kumbuka TRA tangu nifungue hapo nilikuwa namaliza mwaka hawakuwa kufika. Walinifungia na kufuli mpaka nilipofuata baadhi ya taratibu.
Sio kesi hiyo tuu zipo nyingi sana.

2. Viumbe Hai
Wapo viumbe ambao huwa na taarifa za siri ambazo wenye akili huzitumia kufanyia mambo yao. Mathalani, Ndege Bundi ambaye anauwezo mkubwa wa kuona na kunusa kitu kilichokufa. Paka, mbwa, Kuku, njiwa, sisimizi.

Wanyama hawa huwa katika misheni zao lakini huweza kutoa ujumbe fulani, wapo wanyama hunusa visivyoweza kunuswa, huona visivyoonekana kwa urahisi, huhisi visivyohisiwa. Hivyo ukiona wanyama hao wapo sehemu fulani wanalia, au hawajatulia kwa namna yoyote basi usiwe comfortable, jua kuna taarifa imejificha unapaswa uijue.

3. HALI YA HEWA
Hii kila mtu anafahamu ni namna gani inakupa taarifa.

Mawasiliano ya Siri, dalili na ishara ni moja ya mambo muhimu unapokuwa katika mizunguko yako

Sasa nimechoka, acha nipumzike

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Asante sana, utangulizi mzuri sana wa kifasihi huo! Umezungumzia jambo kubwa sana ni kweli hakuna linalotokea bila taarifa! Mimi nimefuatilia sana jambo hili kwa miaka mingi nimegundua kila kitu kinazungumza, huwezi kuamini ndivyo ilivyo. Tatizo letu ni kuelewa lugha isemwayo.
 
Back
Top Bottom