Mawasiliano ya barabara Dar - Bagamoyo yakatika

Hilo ndio daraja halis la Bagamoyo ukivuka hapo inaingia njia ya panda kwa kipingu mbele bao bao sec
 
Kinachoonekana kwenye picha ni barabara imetenganishwa na daraja na siyo daraja kuvunjika jamani, daraja lipo, na kama ingekuwa kuvunjika basi lingeonekana lipo vipande kadhaa,
 
Nimetoka Marian asbh, nkapita hapo, niliyaona yale maji.Yalikuwa mengi na kasi yake ilikuwa ya ajabu. Na upande wa pili yalikuwa yanajaa tu. Fundisho kwa madaraja ya mwenge, mbezi na tegeta.
 
We acha utani, si tunataka picha ya daraja lililobomoka wewe unaleta picha ya Kichuguu halafu eti site ya mtu!!!

Mbona sina uhusiano wowote na mada hii?

Hata hivyo maoni yangu ni kuwa hayo ndiyo matokeo ya ujenzi substandard na contract za chapchap. Huenda hakuna clause inayomwadhibu contractor wa kazi yenye matokeo hayo na vile vile warranty inawezekana pia ikawa ni goigoi.
 
Mbona sina uhusiano wowote na mada hii?

Hata hivyo maoni yangu ni kuwa hayo ndiyo matokeo ya ujenzi substandard na contract za chapchap. Huenda hakuna clause inayomwadhibu contractor wa kazi yenye matokeo hayo na vile vile warranty inawezekana pia ikawa ni goigoi.
Mkuu , Jina na avatar yako vina uhusiano moja kwa moja na picha aliyopost huyo jamaa.

Hata hivyo kuhusiana na daraja kuna mambo mengi sana yanayo come into play!

Nakumbuka vizuri daraja hili limejengwa zaidi ya miaka 14 iliyopita na lilijengwa kwa Tshs milioni 100.
Pengine tuangalie vizuri daraja lenyewe halijadhurika isipokuwa tuta linalounganisha daraja na barabara.

Hapo moja kwa moja tunakuja gundua kuwa tatizo ni maintainance na kitu insitwa River Training.
Hatujasahau kuwa pale Morogoro kule Dumila, daraja lilikatika nalo lilisombwa lile tuta kwa kukosa maintainance.

Tunagharamia sana miundombinu hii ya ujenzi lakini hakuna matengenezo au maintainance inayohitajika.

Kwa mtindo huu tutegemee madaraja mengi zaidi kusombwa.
 
Mawasiliano kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo yavunjika baada ya Daraja la Bunju B jiran na bao bao au kwa kipingu kuvunjika Kama unakwenda Bagamoyo nakushauri rudi nyumban hakuna njia!
attachment.php




Dk.Magufuli akisimamia urudishaji wa huduma za daraja la Mpiji:
 
Back
Top Bottom