Maumivu ya kichwa baada ya kujifungua

mimi05

Member
Nov 11, 2010
46
3
Habari wana jamii,naomba ushauri kuhusu maumivu makali ya kichwa upande wa kushoto baada ya kujifungua kawaida.Dr alisema ni kawaida kuumwa kichwa kwa mama anyonyeshaye ila naona yanaongezeka zaidi.Je kama ni kawaida yatachukuwa muda gani kupona? Nilipima HB iko sawa. Asanteni kwa ushauri.
 
hakikisha unakanda maji hadi kichwani
 
Habari wana jamii,naomba ushauri kuhusu maumivu makali ya kichwa upande wa kushoto baada ya kujifungua kawaida.Dr alisema ni kawaida kuumwa kichwa kwa mama anyonyeshaye ila naona yanaongezeka zaidi.Je kama ni kawaida yatachukuwa muda gani kupona? Nilipima HB iko sawa. Asanteni kwa ushauri.

Ulijifungua kwa operation (caeserean section) kwa dawa ya ganzi ya 'spinal' (sindani mgongoni)?
 
Nami naungana na mtoa hoja, Maana hata mimi toka mke wangu ajifungue kwa njia ya kawaida kichwa kinaumwa mtindo mmoja. Alipomuuliza daktari akamwambia atumie panadol. Lakini hali bado inaendelea, akitumia panadol maumivu yanatulia ila akiacha tu yanarudia tena.

Tunaomba wataalamu wa hapa JF, watuelimishe Je hali hii ni kawaida au kuna tatizo lingine? Je, upungufu wa damu baada ya kujifungua unaweza kutokea na kusababisha hali hii? Na nini kifanyike??????
 
Mimi naomba wote wenye shida hizi waseme bp zao wamepima sasa ziko ngapi na kabla ya kujifungua ilikuwa ngapi coz yawezekana ikawa pressure iko juu inaweza kusababisha kichwa kuuma hasa waliojifungua kawaida, kwa waliojifungua kwa operations hii huwa ni side effect ya spinal anesthesia na hii hutokana na kuamka yaani kuinua kichwa kabla ya masaa 24 tangu ujifungue. Lakini pia tusisahau malaria hivyo mpime na BS pia yawezekana ikawa malaria pia.
 
Back
Top Bottom