Mjadala wa Ushauri na tiba ya maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)

Hi Doctor,

Naomba msaada kwa hili Doctor. Nina mchumba ambae nategemea kufunga nae ndoa siku chache zijazo. Mchumba wangu huyu ana tatizo la kuumwa na tumbo sana (hadi analia na kugaragara) pindi anapoingia period. Huumwa kwa muda wa siku mbili. Je, tatizo hili linatokana na nini? Na tiba yake ni nini? Naomba msaada wako nimuokoe kwenye maumivu haya. Asante sana
 
maumivu makali ya tumbo wakati wa kuanza period yana sababishwa na mfuko wa uzazi(uterus) inapojisafisha baada ya kushindwa kupokea kilichotarajiwa,yaani kuanza kutengezwa mimba, hivyo mishipa ya damu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwezesha ukuaji wa mtoto hujibandua kutoka kwenye ukuta wa uterus kusababisha damu kutoka,kwa sababu inaanza kuacha vidonda maumivu makali hutokea,ni vema kutumia dawa za kupunguza maumuvu au kuwaona DK.mabingwa wa wanawake.
 
Mpe pole sana huyo mwenzi wako mtarajiwa! Ni vema akawaona wataalamu wa magonjwa ya kinamama hilo ni tatizo linalotibika kabisa.
Dysmenorrhea huwapata baadhi ya kina dada na akitibiwa tatizo hili huisha kabisa, wakati mwingine endometriosis pia husababisha maumivu makali wakati wa period.
 
Kama anajijua vizuri awe anameza dawa za maumivu mapema siku anayotarajia. . .yani akiona dalili tu.

Inawezekana akiwa anaumwa hua analala akidhani itasaidia. . .I used to think so,it doesn't. Mazoezi hata kutembea tu kunasaidia.Tatu awe anakunywa maji ya uvugu vugu kwa wingi. . . pia aweke maji ya moto kwenye chupa au mfuko wa plastic alafu atumie kukandia tumbo chini ya kitovu. Kitu kingine anavhoweza kufanya ni kuavoid vitu vyenye sukari ya kutengenezwa kama soda siku mbili kabla ya siku zake na kuendelea mpaka amalize.Pia juice ya nanasi inasaidia. . .

Mpe pole.
 
ngoja nikamfundishe mdogo wangu...huwa analalamika sana na yeye.
wozaaaa
 
Wana JF, nina msichana ambaye huwa anapata maumivu makali sana akiwa kwenye siku zake (akiwa kwenye hedhi). Huwa anatapika sana na maumivu ya tumbo huwa ni makali sana. Nimekuwa nikimpeleka hospitali na huwa wanamchoma sindano ya kutuliza maumivu hayo na hupewa vidonge. Lakini kila mwezi, akiwa mwezini lazima atapike na huwa na maumivu makali sana.Ninaomba kama kuna mtu anayefamu dawa ya kumaliza tatizo hilo.
 
pole sana mkuu, umeshawahi kumpeleka kwa dakatari wa magonjwa ya kina mama? kuna kina dada wanaopatwa na tatizo hili, wanashauriwa pia kutumia dawa za maumivu kama Mifenamic acid ambayo ni prostaglandin blocker kwani maumivu hayo husababishwa na release ya prostaglandin, pia ni vyema aende hospitali kumwona daktari wa kina mama,
 
Dysmenorrhoea. Unahitaji kutumia antispasmodics na analgesic. Iliozoeleka sana ni Buscopan. Lakini elezea vizuri. Maumivu ndiyo yana anza na kupunguwa baada ya kutoka au yana anza pamoja na hedhi. Pole sana.
 
sex.jpg

Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.

Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Karibu nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia 15 wanasema kuwa hupata maumivu makali. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

• Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.
• Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.
• Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).
• Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

Maumivu ya Tumbo la Hedhi... Sehemu ya Pili


stomach_cramps_web507.jpg


kukasababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
• Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.
• Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.
• PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
• Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
• Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo, hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?

1. Maumivu mara nyingi si makali.
2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti (spasmodic).
3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.
4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.
5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.
7. Kufunga choo.
8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.
9. Kuhisi maumivu ya kichwa.
10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.

Inapasa kujua kuwa, kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hutambua wanapopata tumbo la hedhi bila hata msaada wa daktari. Wanawake wanashauri iwapo watapata maumivu makali sana ni bora

wakamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo **** matatizo mengine ya kitiba yanayosababisha maumivu hayo kuwa makali.
Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama

vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS). Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.

Kuna baadhi ya tiba za mitishamba pia ambazo husadia kupunguza muamivu ya tumbo la hedhi. Hapa namaanisha herbal, wenzetu Wachina ni watalamu wazuri katika ujuzi huo. Vilevile wanawake washauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu

hayo, baadhi ya hivyo vimetaja kama kuoga maji moto, kutumia hot bottle na hata kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo. Kuna baadhi husaidia kwa kufanya mazoezi kama yoga, meditation, kusuliwa, tiba ya sindano (Acupunture), TENS au kushituliwa

mishipa ya fahamu ( Transcitaneous Electric Nerve Stimulation na hata wengine husaidiwa kwa tendo la kujamiiana. Vilevile kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.

Tunaelezwa kuwa tunaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
 Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, cofeini, Sodium na sukari.
 Kufanya mazoezi.
 Kujiepusha na wasiwasi na mawazo.
 Kuepuka kufuta sigara.
… Haya kina mama na kina dada, Mkumbuke kuwa afya ni zenu na inabidi Muzitunze!
Chanzo: Mashosti blog
 
kushukuru sana kwa huu uzi manake menigusa kunako. sasa tuanze hivi jamani haya dysmenrrhoea jamani iko na utata sana. mfano halisi mimi huwa ninaumwa sana nimeshafanya hadi ulta sound na MRI lakin huwez kuamni hakuna tatizo ambalo ni la kitabibu. nakumbuka ilifika wakati dr kamugisha akasema ishu ipo kwenye mirija kwamba imebana hivyo huwa haitanuki irahisi kuachia damu kutoka ila bado sikupata furaha na jiabu hili manake nimezaa 3 times na zote ni kawaida na katika zote sijawah kupata tearing sasa iweje kwenye hedhi iwe midogo na kuniletea maumivu?

istoshe niliamini kwamba kama tatizo ni kwenye kutanuka basi nikisha zaa tatizo litaisha nikajikuta wapi, regardless ya kuzaa kwenye umri ambao unaruhusiwa kiafya. hadi leo hii nina maumivu ambayo hayasikii dawa yeyete ya maumivu na huwa najichukia kwakweli to me ni heri niwe mjamzito kuliko niwe kawaida. haya mra kuna wengine wakanipa darasa la kitaa kwamba nikibadili jinsia nitapona lakin nimejiuliza pana mahusiano gani hapa sipati jibu. istoshe nikisema niendelee kuzaa ili nipate kadada mbona nitajaza nyumba mikia pasi kumpata huyo dada?

uamzi niliofikia nakwenda kufunga uzazi kwa kukata mirija ya kizazi ili nisitumike tena na nisiumwe what do you suggest?
 
Kwa kutambua mchango mkubwa wa JF na watumiaji wake katika kupata suluhisho la matatizo katika jamii, nimeona nililete kwenu tatizo ili. Kuna rafiki yangu amekuwa akiumwa sana hata kufikia hali ya kupelekwa hospitalini kila mwezi na kulazwa wakati wa hedhi. Kwa taarifa nilizopata toka kwake amesema tatizo ili limekuwa likiambatana na maumivu makali ya tumbo, kupata homa kali, kuvimba mwili mzima, kutapika na kukosa hamu ya kula.

Tatizo ili limekuwa likimpata tangu aanze kupata hedhi na halionyeshi dalili za kupungua bali limekuwa likiongezeka kadri miaka inavyokwenda. Familia nzima imekuwa katika hali ya huzuni na kukosa furaha kwa sababu ya matatizo ya binti yao. Mama yake mzazi amekuwa akihangaika huku na kule pasipo mafanikio.

Kwa yeyote anayejua suluhisho au namna ya kupunguza/ kumaliza tatizo hili, tafadhali tunaomba msaada wako.
 
Hiyo ni hedhi tu jamani? Au kuna tatizo jengine limejificha? Amejaribu kufanyiwa full medical check up?
 
Tatizo hilo lipo siyo hedhi ya kawaida linaitwa dysmenorrhea kitaalam.tatizo hili linaweza kuwa la awali au linasababishwa na tatizo jingine ktk mfumo wa uzazi ambalo hujitokeza kuwa na dalil baadaye msichana akikua.

Mara nyingi watu hawa hupata maumiv makal sana saa 48 baada ya kuona mp,maumiv huelekea kwenye nyonga na yana ambatana na maumiv ya mgongo, kukosa ham ya kula,kutapika, kuharisha maumivu ya kichwa na kupoteza fahamu kwa muda, kwa wengine hali hii huweza kujitokeza muda mfup kabla ya mp na ni kwa sababu ya chemikaki ziitwazo prostaglandins

Mara nyingi sana tiba ya tatizo hili ni kutoa dawa za maumiv lakin kuna utaalam mpya ambao kwa sasa unaweza kuutumia,ni wa asili na hauna madhara, if u dont like being in trouble when your mp comes,cal me at 0752720276.pole sana.
 
Kuna mdada kaolewa, huu ni mwaka wa tano sasa, hajapata mimba kabisa. Pili, akiingia mwezini, baada ya siku kumi na tano anaanza kupata maumivu kidogokidogo, siku zinavyosogea ndo anavyozidi kuumwa. Ni nini haswa tatizo? Nimemshauri waende hospitali na mumewe, mumewe kakataa.
 
Nijuavyo siku hizo azisemazo zinafanana na dalili za maumivu mwanamke anazosikia wakati yai linatembea kwenye ile mirija....ndio siku za hatari. Dalili zingine ni joto la mwili wake kupanda na ute mreefu unatoka ukeni.

Soma na hii kidgo kuhusu Mimba.

Ishu ya mimba ipo complicated kidgo na mara nyingi huwa wanawake ndio wanasingiziwa matatizo endapo tu hapati mimba bila kujua kuwa hata sisi wanaume tunae matatizo. Hii mimi sio taaluma yangu, ila ntaeleza kwa kadiri nilivyo elekezwa na kufanyia kazi.

-Tarehe ya hatari kabisa ya mwanamke katika kupata mimba ni siku ya 14 na 15 tangu siku ya kwanza amepata MP. Ila hata siku mbili kabla ya tarehe hizo za hatari, endapo ametembea na mwanaume, anaweza kupata mimba kwa kuwa tu (X) inaweza kudumu katika mwili wa mwanamke kwa siku 3, wanasema hapa ni kwa wanaotaka mtoto wa kike.

-Mwanaume naye, lazima mbegu zake ziwe ok, zisiwe zimeharibika, zisiwe hazina mikia au chache n.k

-Kama mnatafuta mimba, siku hizo za danger mwanamke ajiepushe kula vyakula vya jamii ya kunde, pizza n.k

-Style ya kifo cha mende ni perfect zaidi, na mwanamke atulie asiende huko bafuni kwao kunawa japo kwa muda mrefu hivi.

Dalili zinatofautiana kati ya mwanamke na mwanamke,....kuna mtu namfahamu, yeye alikuwa anaena Mp kama kawaida kwa miezi mitano na hajastukia kama imenasa....lol.

Mimba ni crzy stuffs, wakati mnaitafuta....walahi itawatesa ili muipate sio mchezo....but wakati hamna mawazo nayo...hiiyo imetokea.........kuna kaka (rafiki yangu) alikaa na mwanamke kwa zaidi ya miaka 5, hawakupata kitu....yule dada akawa anasimangwa na mama mkwe eti hazai...wakaachana....dada akaolewa na mwanaume mwingine, kaka nae akaoa mwanamke mwingine....yule dada now ana mi'bausing baby boy mitatu...na jamaaa nae ana kijiji cha watoto....sasa sijui utasema ni nini wakati walihangaika sana.

Nina jirani yangu hivi, yeye aliishi na mkewe zaidi ya miaka 7 bila mtoto, na hakuna mahali hawajaenda ktk kuisaka sasa...kuna mama mmoja ambaye naye ni jirani yetu....(ofkoz hii ishu inajulikana mtaa mzima)...yeye huyu mama baba yake mzazi,ni hawa madaktri wa kienyeji waliosajiliwa na Muh2.....akaja hapo kwa huyo mama (mwanae) kumtembelea. Huyo mama akaifuta ile familia yenye shida, kuwa waje kumjaribu baba yake anadhani angewasaidia......ile familia ikamfuata yule mzee......akawapa dawa, ili yule mtafuta mtoto ainywe siku anaanza Mp, na stop siku MP inaisha.....kwa malipo kuwa...40,000/- alipwe mtoto akizaliwa.! Mwezi uliofuata mama kajaaa....hawakusubiri ajifungue....wakapeleka zaidi kwa huyo mzee. Hivi wana mitoto ya kumwaga......!

WANAWAKE WASINYANYASWE kwa kutopata MIMBA, MUNGU ndiye mpangaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom