Mauaji ya kimbali Myanmar

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
186dadf36e8a1feddebe0c5632f68164.jpg


LIFAHAMU TAIFA LA MYANMAR/BURMA AU SUVANNABHUMI (NCHI YA KIDHABAHU) NA CHIMBUKO LA MAUAJI YA KIMBALI DHIDI YA WAUMINI WA KIISLAMU YANAYOTEKELEZWA NA WAUMINI WA DINI YA KIBUDHA.

[Makala hii nimeandika kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendele huko katika mkoa wa Rohingya dhidi ya waumini wa kislam.]

Na, Comred Mbwana Allyamtu.
Wednesday 06/9/2017.

Myanmar ambayo Kwa fasili ya Kiswahili huitwa “NCHI ya Kidhahabu” jina linalotokana na lugha ya kimynmar iko katikati ya milima inayoitenganisha na nchi jirani za Asia. Ghuba ya Bengal na Bahari ya Andaman ziko upande wa kusini-magharibi wa nchi hiyo iliyo na pwani yenye urefu wa kilometa 2,000 hivi. Bangladesh na India ziko magharibi; China iko kaskazini; na Laos na Thailand ziko mashariki. Nchi hiyo ni kubwa kidogo kuliko Madagascar na ni ndogo kuliko jimbo la Texas la Marekani. Nchi hiyo huitwaje? Myanmar, au “NCHI ya Kidhahabu” na hapo zamani iliitwa Burma.

Wakazi wa kwanza kabisa wa Myanmar waliiita nchi hiyo Nchi ya “Kidhahabu”. Nchi hiyo ina mali asili nyingi muhimu, kama vile: mafuta na gesi, shaba, bati, fedha, tang’isteni, na madini mengine. Pia, kuna vito vyenye thamani kama vile yakuti, zumaridi, rubi, na vito vyenye rangi ya kijani. Mali asili nyingine zatia ndani misitu ya mvua ya kitropiki yenye miti isiyopatikana sana, kama vile msaji, rosewood, na padauk. Misitu hiyo pia ina wanyama-pori wengi kama vile, tumbili, simba-milia, dubu, nyati, tembo, na kadhalika. Lakini wenyeji wa Nchi ya Kidhahabu (MYAMAR) ndio wenye thamani zaidi. Kaskazini mwa nchi kuna milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin wenye kimo cha mita 5,881. Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; Ayeyerwady , Thanlwin, Sittang . Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170. Bonde lake ni la rutuba na lina wakazi wengi. Karibu nusu ya nchi imefunikwa na misitu.

HISTORIA YA MYNMAR
Tangu 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake.Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885.Mwaka 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni la pekee. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japan ilitwaa karibu nchi yote. Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake tarehe 4 Januari 1948. Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa na jeshi mwaka 1962. Historia ya mapema kabisa ya Myanmar haijulikani sana, lakini yaonekana kwamba makabila fulani yalihamia huko kutoka maeneo ya karibu. Watu wa kabila la Mon waliiita nchi hiyo Suvannabhumi—maana yake ni, “Nchi ya Kidhahabu.” Watu walioongea Kitibeti-Burma walihamia huko kutoka sehemu ya mashariki ya milima ya Himalaya na watu wa kabila la Tai walitoka mahala ambapo sasa ni kusini-magharibi mwa China. Milima mingi ya Myanmar ilitenganisha makabila. Hiyo ndiyo sababu kuna makabila mengi na lugha nyingi.

Mapema katika karne ya 19, Waingereza walioishi katika koloni yao mpya ya India walianza kuwasili. Kwanza walikaa kwenye eneo la kusini halafu wakamiliki nchi yote. Kufikia 1886, Burma, jina la Myanmar la zamani, ikawa sehemu ya British India. Wakati wa Vita ya Pili ya Ulimwengu, nchi hiyo ilikuwa eneo la vita, na baada ya miezi michache mnamo mwaka wa 1942, majeshi ya Wajapani yaliwaondoa Waingereza. Kisha, reli yenye sifa mbaya iliyoitwa “Reli ya Kifo” ilijengwa. Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 400 ilipita kwenye maeneo hatari ya msituni na milimani nayo iliunganisha mji wa Thanbyuzayat huko Burma na mji wa Nong Pladuk nchini Thailand. Kwa sababu kulikuwa na uhaba wa metali, sehemu kubwa ya reli hiyo ilitengenezwa kwa vyuma vya reli vilivyotolewa katikati ya nchi ya Malaya (ambayo sasa ni Malaysia). Sehemu ndogo ya mradi huo—kujenga daraja juu ya Mto Kwai—ilitumika baadaye kama habari kuu ya filamu moja maarufu.

Wanaume zaidi ya 300,000—watu waliotekwa vitani na wenyeji wa India na Burma—walijenga reli hiyo wakisaidiwa na tembo 400. Makumi ya maelfu ya watu walikufa wakifanya kazi hiyo. Reli hiyo ilishambuliwa sana na ndege za kurusha mabomu za majeshi ya Muungano. Hivyo, haikutumika sana na mwishowe iliacha kutumiwa kabisa. Baadaye, vyuma vingi vya reli viling’olewa na kutumiwa kwingineko.

Hatimaye, Waingereza wakafanikiwa kumiliki nchi hiyo tena walipowashinda Wajapani mnamo mwaka wa 1945. Lakini Waingereza hawakutawala kwa muda mrefu, kwani Burma ilipata uhuru mwezi wa Januari 4, 1948. Mnamo Juni 22, 1989, shirika la Umoja wa Mataifa liliidhinisha jina jipya la nchi hiyo, Myanmar. Mtawala mpya hadi mwaka 1988 alikuwa jenerali Ne Win aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa. Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu. Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi. Uchaguzi huru wa mwaka 1989 ulileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi madaraka. Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi hadi mwaka 2011. Upinzani haukuruhusiwa.

UTAWALA
Myanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika madola 7 na mikoa 7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwa Bamar. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa.

Majimbo ya Myanmar
Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:

(1) Dola la Rakhaing (Arakan) (Makao makuu: Akjab (Sittwe))
(2) Dola la Chin (Makao makuu: Hakha)
(3) Dola la Kachin (Makao makuu: Myitkyina)
(4) Dola la Shan (Makao makuu: Taunggyi)
(5) Dola la Kayah (Makao makuu: Loi-kaw)
(6) Dola la Kayin au Karen (Makao makuu: Pa-an)
(7) Dola la Mon (Makao makuu: Mawlamyaing)

Halafu kuna mikoa 7:
(8) Sagaing (Makao makuu: Sagaing)
(9) Tanintharyi (Tenasserim) (Makao makuu: Tavoy)
(10) Irawadi (Makao makuu: Pathein)
(11) Yangon (Makao makuu: Rangun)
(12) Bago (Pegu) (Makao makuu: Bago)
(13) Magwe (Makao makuu: Magwe)
(14) Mandalay (Makao makuu: Mandalay)

WENYEJI WA MYANMAR.
Mara nyingi wageni wanaotembelea Myanmar hushangazwa na ngozi laini ya watu wazee. Wanawake wa huko wanasema kwamba ngozi hiyo laini kama ya kijana hutokezwa na kipodozi cha rangi hafifu ya dhahabu kinachoitwa thanaka. Kipodozi hicho hutengenezwa kutokana na mti wa thanaka. Wanawake hufanyiza rojorojo laini kwa kusaga tawi la mti huo kwenye jiwe gumu tambarare kisha wanaongeza maji kidogo. Wao hupamba nyuso zao kwa kutumia kipodozi hicho. Kipodozi cha thanaka hulainisha, hutuliza, na kulinda ngozi na jua kali la tropiki.

Vazi la lungi ndilo huvaliwa kwa kawaida na wanaume na wanawake nchini Myanmar. Vazi hilo hutengenezwa kwa urahisi kwa kushona ncha mbili za kitambaa chenye urefu wa meta mbili hivi. Wanawake hulivaa kwa kuingia ndani yake, kisha wanalizungusha kama sketi, na kuingiza kiunoni ncha moja inayoning’inia. Nao wanaume hulivaa kwa kufunga ncha zote mbili za vazi hilo kiunoni. Kwa kuwa vazi la lungi ni nadhifu na halibani, linafaa kabisa maeneo ya tropiki. Ukitembelea masoko utaona kwamba watu wa Myanmar wana vipawa vingi. Wana ustadi wa kufuma hariri, kutengeneza vito, na kuchonga vinyago vya mbao. Vinyago vinavyovutia vya wanadamu, simba-milia, farasi, nyati, na tembo vimetengenezwa kwa mbao za msaji, padauk, na miti mingine. Hata vitu vya kawaida kama meza, kuta zinazotenganisha vyumba, na viti vimechongwa mapambo mengi sana. Lakini iwapo unataka kununua vitu hivyo, uwe tayari kupigania bei!

Wenyeji wa Myanmar pia hutengeneza vyombo vinavyopendeza kwa vanishi kama vile, mabakuli, sahani, na masanduku yenye vifuniko. Lakini vyombo vyao ni vya pekee hasa kwa sababu michoro na mapambo yake si ya kawaida. Wao huanza kufuma vyombo vyao kwa kutumia kamba za mwanzi. (Vyombo vya hali ya juu hufumwa kwa mwanzi na manyoya ya farasi.) Chombo kilichofumwa hupakwa vanishi mara saba. Vanishi hiyo hutengenezwa kwa kuchanganya mafuta ya mti wa thisei, au mti wa lacquer, pamoja na mifupa ya wanyama iliyochomwa na kusagwa. Vanishi hiyo inapokauka, msanii huchonga mchoro kwenye chombo hicho kwa kutumia kifaa cha kuchora cha chuma. Kisha, chombo hicho hupakwa rangi na kung’arishwa nacho huvutia sana na kinaweza kutumiwa nyumbani.

Dini Imeathiri Mambo Mengi

Asilimia 85 hivi ya wenyeji wa Myanmar ni Wabudha; na watu wale wengine ni Waislamu na Wakristo. Kama ilivyo katika nchi nyingi za Kusini-Mashariki mwa Asia, dini ni muhimu kwa wenyeji wengi wa Myanmar. Hata hivyo, wageni wengi hawafahamu desturi fulani za dini za huko. Kwa mfano, watawa Wabudha wameweka nadhiri kutomgusa mwanamke. Hivyo, kwa heshima, wanawake huwa waangalifu wasiwakaribie sana watawa hao. Desturi za kidini huathiri watu pia wanaposafiri kwa basi. Mtu wa nchi ya Magharibi aweza kushangazwa anapoona ishara kwenye basi inayosema hivi: “Tafadhali usimuulize dereva tutafika lini.” Je, ishara hiyo imewekwa kwa sababu madereva hukasirishwa na abiria wenye haraka? La. Wabudha wa huko huamini kwamba akina nat (roho) watakasirishwa na swali hilo na huenda wakachelewesha basi.

Nchi ya Myanmar imekuwa na majiji mengi makuu katika karne zilizopita. Kwa mfano, katikati ya Myanmar, utapata jiji la Mandalay ambalo kwa kawaida huitwa Jiji la Kidhahabu. Jiji hilo lenye minara mingi ya kila aina inayoitwa pagoda, lina watu 500,000 nalo ndilo lililokuwa jiji kuu kabla ya Waingereza kumiliki nchi hiyo. Mfalme Mindon alifanya jiji la Mandalay kuwa jiji la kifalme alipojenga jumba kubwa la kifalme huko mnamo mwaka wa 1857 kwa ajili yake na malkia zake. Jiji hilo la kale lenye ukubwa wa kilometa za mraba 4 limezingirwa na ukuta wenye kimo cha meta 8 na upana wa meta 3. Handaki la maji lenye upana wa meta 70 huzunguka ukuta huo.

Mnamo mwaka wa 1885, Waingereza walimpeleka mwandamizi wa Mindon, Mfalme Thibaw, uhamishoni huko India, lakini hawakuharibu jumba hilo la kifalme. Hata hivyo, jumba hilo la kifalme liliteketezwa kabisa kwa moto wakati wa Vita ya Pili ya Ulimwengu. Watu wa Myanmar hawakukata tamaa, bali walijenga tena jumba jingine la kifalme lililofanana kabisa na lile la kwanza pamoja na majengo yake ya mbao ya rangi nyekundu na ya dhahabu kwenye eneo hilohilo. Watu wanaweza kutembelea jumba hilo.

NINI CHIMBUKO LA MAUAJI YA KIMBALI DHIDI YA WAISLAM HUKU MYNMAR?

669d7c7cc9192e236cb0a28180aeede1.jpg


Mauaji unayoyaona yanaendelea leo huko Myanmar yanatokana na kile kinachoitwa “Operation ya kufyeka magaidi wa mipakani” lakini sasa katika Oparesheni ya Jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu ilishika kasi mwezi Okotoba mwaka jana kwa kisingizio cha kuwasaka watu wenye silaha waliodaiwa kufanya hujuma katika vituo vya mpakani nchini humo. Tokea ilipoanza imesema wakuu wa serikali na maafisa wa kijeshi nchini Myanmar wanawaua kwa umati Waislamu nchini humo mbali na kutekeleza jinai zinginezo zilizo dhidi ya binadamu.
Kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha utafiti cha haki za binadamu kimeripoti kuwa kuna uwezekano vitendo vya jinai wanavyofanyiwa Waislamu hao na uwezekano wa kutokea mashambulizi mengine makubwa dhidi yao, vikahesabiwa kuwa ni uhalifu wa kitaasisi na ni jinai dhidi ya binadamu. Serikali ya mabudha huko Myanmar inawanyima Waislamu haki yao ya kuwa raia na wanadai eti Waislamu hao ni wahajiri wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria wakati Waislamu wanasema kuwa wamekuwa wakiishi nchini Myanmar kwa karne nyingi na hawajui nchi kuwa nchi yao isipokuwa Myanmar.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya Waislamu laki moja wa kabila ya Rohingya walilazimika kukimbia makazi yao katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa Myanmar baada ya mabudha wenye misimamo mikali kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya Waislamu hao mwaka 2012. Shilika hilo la HRC limesema wakuu wa serikali na maafisa wa kijeshi nchini Myanmar wanawaua kwa umati Waislamu nchini humo mbali na kutekeleza jinai zinginezo zilizo dhidi ya binadamu.

Shirika hilo limesema, idadi kubwa ya Waislamu wa Myanmar wanalazimika kukimbia nchi yao kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Serikali ya nchi jirani ya Bangladesh inasema, Waislamu 70,000 Warohingya wameingia nchini humo tokea mwezi Oktoba mwaka jana, wakitokea Myanmar. Shirika hilo limesema, idadi kubwa ya Waislamu wa Myanmar wanalazimika kukimbia nchi yao kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Serikali ya nchi jirani ya Bangladesh inasema, Waislamu 70,000 Warohingya wameingia nchini humo tokea mwezi Oktoba mwaka jana, wakitokea Myanmar.

Ripoti hiyo imetangazwa wakati ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti habari ya kuongozeka ukatili, mauaji, na ubakaji wa Waislamu mikononi mwa jeshi la Myanmar. Ni kwa sababu hii ndio sababu masaibu wanayopitia Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar yakatajwa kuwa ni maangamizi au mauaji ya kimbari yaani genocide. Kudhulumiwa na kuuawa kwa umati Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar katika mkoa wa Rakhine kunaendelea wakati ambapo serikali ya nchi hiyo inadai kuwa oparesheni za kijeshi zimemalizika katika mkoa huo.
operesheni hiyo ya kikatili na kinyama mkoani Rakhine, mashahidi wanasema wanajeshi wamewanajisi wanawake Waislamu, wameteketeza kwa moto nyumba zao na kuwaangamiza kwa umati Waislamu hao. Ripoti za ukatili na unyama huo zimeumiza nyoyo za walimwengu hasa Waislamu ambao wamelaani sera za maangamizi ya kimbari ambazo zinatekelezwa na utawala wa mabudha wa Myanmar.

Kuendelea mauaji na unyama wa jeshi la mabudha wa Mynamara dhidi ya Waislamu kunajiri wakati ambapo mshauri wa usalama wa taifa nchini humo amedai kuwa, kila kitu ni shwari na eti Waislamu hawadhulimiwi tena. Serikali ya Myanmar inajaribu kuwahadaa walimwengu wakati ambapo ni jambo lililo wazi kuwa Waislamu nchini humo wanaendelea kutendewa ukatili usio na kifani katika mkoa wa Rakhine. Ili kuficha ukweli kuhusu jinai zake, serikali ya Myanmar imewapiga marufuku au kuwawekea vizingiti waandishi habari na wawakilishi wa mashirika ya haki za binadamu wanaotaka kufika Rakhine. Kwa njia hiyo wakuu wa Myanmar wanataraji watawazuia walimwengu kupata habari za mauaji ya kimbari ya Waislamu katika nchi hiyo. Hivi sasa ripoti zilizochapishwa kuhusu hali ya mambo huko Rakhine zimetolewa na Waislamu waliotoraka Myanmar na kuingia nchi jirani hasa Bangladesh

bf61fc947bfcb29b1b58d1869d4ed486.jpg


Mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada Myanmar wanaongoza kampeni ya kuwaangamiza Waislamu Waislamu wa Myanmar hawauawi na kuteswa tu na vikosi vya serikali, bali hata Mabuda wenye misimamo ya kufurutu ada nao pia, kwa himaya ya vikosi vya usalama, wamehusika katika uhasama na ukatili mkubwa dhidi ya Waislamu hao katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.

Pamoja na kuwa walimwengu wamelalamika na kuonyesha hasira zao kuhusu mauaji ya umati na kudhulumiwa Waislamu wa Myanmar lakini Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijaonyesha kuchukizwa na yanayojiri Myanmar. Hii ni katika hali ambayo ni jukumu la baraza hilo kulinda na kudumisha amani ya kimataifa. Walimwengu wanataraji kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litachukua hatua za haraka kuushurutisha utawala wa Myanmar usitishe kikamilifu na mara moja ukatili dhidi ya Waislamu. Mbali na hilo taasisi za kisheria duniani hasa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inapaswa kuchukua hatua za kuwafikisha kizimbani wale wote wanaohusika na mauaji ya kimbari na jinai nyinginezo dhidi ya Waislamu wa Myanmar.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
9dd69bd72dd74fba60f62cfc1fbc52c0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ndio ukweli ambao hata Huyu mleta mada amejitahidi kuuficha, ukweli hujitenga. waislam wa Burma wataishi kwa Amani wakiheshimu desturi na imani za wa BURMA
Ndio zao
998d6b5efe3a32cd0296c737877d403d.jpg
+ taqya
 
Comrade Mbwana umetoa maelezo mazuri kuhusu mgogoro huo unaoendelea. Hata hivyo umeshindwa kutoa ukweli wote hususani chanzo cha mgogoro huo. Naomba niongezee machache kama ifuatavyo:-
Kihistoria mgogoro huu umeanzia kipindi cha 1947/1961 kwa watu wa kabila la Rohingya ambao wengi wao ni Waislamu kuunda vikundi vya " local mujahedeen " na kuanzisha vita dhidi ya Serikali wakiwa na lengo na kujitenga na kuwa sehemu ya nchi ya Bangladesh. Kipindi hicho Bangladesh yenye Waislamu wengi ilikuwa bado ni sehemu ya Pakistan. Jamii hii ya watu wa Rohingya inapatikana eneo la Magharibi ya nchi hiyo katika jumbo la Rakhine.
Hata hivyo waasi hao katika miaka ys 1950 hadi 1960 waliamua kujisalimisha kwa Serikali baada ya kukosa nguvu katika mapambano. Hata hivyo waasi hao wa Kiislamu walianzisha tena mashambulizi dhidi ya Serikali mwaka 1970. Serikali nayo ilijibu vikali kwa kuanzisha operesheni King Dragon mnamo mwaka 1979.
Waasi hao wameendeleza harakati zao kwa kushambulia vituo vya police,vituo vya jeshi na kusababisha mauaji na uharibifu wa mali. Maeneo ya mpaka na Bangladesh ndio yamekumbwa sana na madhambulizi hayo.
Makundi makubwa ya waasi hao ni pamoja na kundi la Rohingya Solidarity Organisation na kundi jipya laHarakah al- yaqin.
Watu wa jamii hii ndogo wanajihesabu kuwa ni uzao wa Wafanyabiashara wa Kiarabu waliowahi kuishi hapo karne nyingi zilizopita. Aidha Serikali imewanyima uraia jamii hiyo kwani wanahesabiwa kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh. Ieleweke kuwa sio kweli kuwa waislamu rote wananyimwa uraia wa nchi hiyo Bali zipo jamii za waislsmu zinazotambuliwa na kupewa uraia.
Kwa hiyo wadau kimsingi watu wa jamii hiyo wanalengo moja tu la kujitenga na kuwa sehemu ya Bangladesh. Pia wana mahusiano ya karibu sana na watu wa Bangladesh hasa kiimani. Niongezee tu kuwa waislamu nchini humo no asilimia 4 ya wakazi wote.
NB: Hakuna uthibitisho wowote wa mauaji ya halaiki dhidi ya jamii bali kilichopo ni tuhuma zisizo na uthibitisho.Uthibisho uliopo ni waasi kutoka jamii hiyo kufanya mashambulizi dhidi ya Serikali.Serikali za Bangladesh na Pakistan zimekuwa zikijihusisha katika mgogoro huu mara kwa mara!
 
Comrade Mbwana umetoa maelezo mazuri kuhusu mgogoro huo unaoendelea. Hata hivyo umeshindwa kutoa ukweli wote hususani chanzo cha mgogoro huo. Naomba niongezee machache kama ifuatavyo:-
Kihistoria mgogoro huu umeanzia kipindi cha 1947/1961 kwa watu wa kabila la Rohingya ambao wengi wao ni Waislamu kuunda vikundi vya " local mujahedeen " na kuanzisha vita dhidi ya Serikali wakiwa na lengo na kujitenga na kuwa sehemu ya nchi ya Bangladesh. Kipindi hicho Bangladesh yenye Waislamu wengi ilikuwa bado ni sehemu ya Pakistan. Jamii hii ya watu wa Rohingya inapatikana eneo la Magharibi ya nchi hiyo katika jumbo la Rakhine.
Hata hivyo waasi hao katika miaka ys 1950 hadi 1960 waliamua kujisalimisha kwa Serikali baada ya kukosa nguvu katika mapambano. Hata hivyo waasi hao wa Kiislamu walianzisha tena mashambulizi dhidi ya Serikali mwaka 1970. Serikali nayo ilijibu vikali kwa kuanzisha operesheni King Dragon mnamo mwaka 1979.
Waasi hao wameendeleza harakati zao kwa kushambulia vituo vya police,vituo vya jeshi na kusababisha mauaji na uharibifu wa mali. Maeneo ya mpaka na Bangladesh ndio yamekumbwa sana na madhambulizi hayo.
Makundi makubwa ya waasi hao ni pamoja na kundi la Rohingya Solidarity Organisation na kundi jipya laHarakah al- yaqin.
Watu wa jamii hii ndogo wanajihesabu kuwa ni uzao wa Wafanyabiashara wa Kiarabu waliowahi kuishi hapo karne nyingi zilizopita. Aidha Serikali imewanyima uraia jamii hiyo kwani wanahesabiwa kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh. Ieleweke kuwa sio kweli kuwa waislamu rote wananyimwa uraia wa nchi hiyo Bali zipo jamii za waislsmu zinazotambuliwa na kupewa uraia.
Kwa hiyo wadau kimsingi watu wa jamii hiyo wanalengo moja tu la kujitenga na kuwa sehemu ya Bangladesh. Pia wana mahusiano ya karibu sana na watu wa Bangladesh hasa kiimani. Niongezee tu kuwa waislamu nchini humo no asilimia 4 ya wakazi wote.
NB: Hakuna uthibitisho wowote wa mauaji ya halaiki dhidi ya jamii bali kilichopo ni tuhuma zisizo na uthibitisho.Uthibisho uliopo ni waasi kutoka jamii hiyo kufanya mashambulizi dhidi ya Serikali.Serikali za Bangladesh na Pakistan zimekuwa zikijihusisha katika mgogoro huu mara kwa mara!
Asante kwa kuongeza but mauaji yoyote ya binadamu ni unyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aseee nimetoka kuichek hii vita huk YOUTUBE aseeeee watu wana chanjana kama nyama buchani wazeeeeee usiombee mpaka vitoto vya below 5 yrs old vinachanjwa kama nyama buchani aseeeeee. dah ama kweli UDINI SIYO KABISA
 
Back
Top Bottom