Mauaji ya Daudi Mwangosi: Ushuhuda wa kilichotokea hadi kifo chake

Tusubiri Tume, sorry, Kamati ya Nchimbi nayo ituletee taarifa yake, tuone kama itafanana/tofautina na hii.

NB: Camera na laptop ya marehemu viko wapi? Inawezekana Daudi Mwangosi ali-film kifo chake mwenyewe!
yeah! hili nalo ni jambo la kuhoji, yawezekana kuna baadhi ya matukio aliyadaka mwenyewe hasa yale mazungumzo ya mwisho na KAMANDA MUUAJI.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hongera ndugu yangu kwa kuitendea haki jamii forum . Mungu ailaze mahala pema roho ya ndugu yetu .Jeshi letu la polisi linahitaji mabadiliko ya dhati .
 
nijambo la kushtua sna na lakuhuzunisha sana ni jambo linalotakiwa kukemewa kwa nguvu zote na nijambo ambalo linatakiwa lizidi kuwa chahcu ya kyfahamu ni nini hasa haki za binadamu hususani Africa zinatakiwa zipewe nakuongezewa nguvu kali sana ili kuweza kulinda dhamani na utu wa mtu
 

Wakati askari wakijiandaa kuwafuata wana CHADEMA katika ofisi zao, alitokea mtu aliyevaa shuka na kujifunga kitambaa kichwani ambaye baadaye alijitambulisha kama mkuu wa upelezi mkoa (RCO), akawaamuru wenzake waende katika ‘target' lakini wasithubutu kutumia nguvu bila amri.
Mpango madhubuti uliopangwa kabla
Baada ya kuwasili kwa RPC Kamuhanda, Kamanda wa FFU, Mnunka alienda akamnong'oneza jambo. Pale pale, Kamuhanda akaonekana kukasirika. Akaagiza CHADEMA wasimamishe shughuli yao mara moja.
Ninaamini kwa kumkosa Dr Slaa
Wakati askari wakiwa wanapita walikuwa wakisema Dk. Slaa anatokea eneo la Wami.
Lengo kuu la operesheni. Mungu tu amemwokoa
Ghafla, RPC akatoa amri ya kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa katika ofisi yao. Baada ya amri hiyo, wanachama wa CHADEMA waliokuwa pale wote walikaa chini wakinyoosha mikono juu.
Amalizie hasira
Wakati nikiwa naendelea kuchukua picha, nilimwona askari mmoja akinyoosha mkono juu na mwingine aliyevaa kiraia akiwa ameshika bastola yake kuelekeza juu, huku wengine wakiwa wanaendelea kumpiga Mwangosi aliyekuwa anajitahidi kuinuka kwa kumshika mmoja wa askari wale.

Katika harakati za Mwangosi kujinasua, nilimshuhudia mmoja wa wale askari akiwa kama anainama akaelekeza mtutu wa bunduki usawa wa tumbo la Mwangosi aliyekuwa katika hali ya kutaka kusimama huku akipiga kelele "msiniuee, msiniuee…"
Raha ya milele umpe Mwangosi ee Bwana
 
Du hii ndio picha kamili hakuna anayeweza kubisha, POLISI walifanya kazi kichuki zaidi
 
so sad, nimesoma mwanzo mpk mwisho nimesikitika sana. malipo ni hapahapa duniani. . .
 
Mpango madhubuti uliopangwa kabla

Ninaamini kwa kumkosa Dr Slaa

Lengo kuu la operesheni. Mungu tu amemwokoa

Amalizie hasira

Raha ya milele umpe Mwangosi ee Bwana

Clever!
Tukishajua tunachukua hatua gani, maana this is too much.
Mkishafika 99 mnistue nijiunge, haki huwa haibembelezwi.
 
Baada ya kuwasili kwa RPC Kamuhanda, Kamanda wa FFU, Mnunka alienda akamnong’oneza jambo. Pale pale, Kamuhanda akaonekana kukasirika. Akaagiza CHADEMA wasimamishe shughuli yao mara moja............. Wakati askari wakiwa wanapita walikuwa wakisema Dk. Slaa anatokea eneo la Wami.
IMG_1875.JPG
IMG_1878.JPG

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alipoongea na wanahabari siku ya tukio mkoani Iringa, picha zote zinaonyesha akiwa mwenye mawazo mazito yenye kuashiria jambo zito litatokea.

RPC Michael Kamuhanda ndiye aliyesimamia zoezi zima la kuuawa Mwanahabari Daud Mwangosi na kushuhudia kwamba kazi ya kuuawa imekamilika ndipo akaondoka.

Niliandika kwa ufasaha kabisa hapa kwamba siku hiyo aliyekusudiwa ni Dr. Slaa, lakini iliondolewa na mod. Tuamini intelijensia ilifanya kazi ya ziada siku hiyo, vinginevyo mauaji yangekuwa zaidi ya hayo ya Mwangosi.

Kinachoshangaza suala dogo la kufungua matawi ya chama kijijini RPC awepo, wakati hata mikutano mikubwa inayofanyika mjini huwa hahudhurii, na hata RCO huhudhuria kwa nadra sana.

Timu nzima ya uongozi wa Mkoa ilikamilika kijijini Nyororo
RPC - Kamanda wa polisi Mkoa
RCO - Kamanda wa upelelezi mkoa na pia makamu wa RPC
OCD - Kamanda wa polisi wilaya (aliyejeruhiwa)
OCS - Kamanda wa upelelezi Wilaya
___ - Kamanda wa FFU Mnunka
Kikosi cha askari wenye silaha mbalimbali toka mkoani na nje ya mkoa.​

Nvuvu yote hii kuanzia RPC hadi walenga shabaha ni jambo lililopangwa, na intelijensia ilifanya kazi kumvuta koti Dr. Slaa asiende kwenye tukio hilo. Hata usitishaji wa mwendelezo wa mikutano hiyo huko Iringa na kurudi kujipanga upya Dar kwa kuanza na mkutano wa kamati kuu ya chama, ni njia moja wapo ya intelijensia ilivyofanya kazi, kwani kazi waliyokusudia haija kamilika, mpiganaji Mwangosi ilikuwa kumalizia hasira tu. Mlengwa Dr. Slaa hawakufanikiwa kumpata.

Ukitazama picha ya RPC Chamuhanda siku ya tukio alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari na kuwaambia wamejiandaa kwa lolote, macho yake yalionekana mekundu pyuuuu kuashiria yamechanganyika na kitu fulani ambacho hujulikana kama under influence hali ambayo mtu mwenye timamu na utashi hutumia kikolezo ili akili kuipumzisha na kuhama kwa muda na kuwa hali isiyo yake hasa kwa wenye malengo fulani ili utashi wao kufanya yaliyokusudiwa.

NB:

  1. [*=1]Kuna uwezekano mkubwa kwamba siri waliokuwa nayo ni viongozi wa juu wa mkoa, ndio maana OCD alikuwa anafanya ziada ya kumwokoa bila mafanikio ni kuishia kujeruhiwa.



  1. [*=1]Kuna uwezekano mkubwa kwamba ndani ya kundi la FFU kuna waliochomekewa wakika katika mpango kamili nani afanye nini wakati wengine katika kundi wasijue kinachoendelea.
 
Huu ndio ushahidi wenye ukweli wa tukio zima, ndio first hand data SIO ZILE SIMULIZI ZA MAGGID MJENGWA!

mjengwa is too full of himself. usishangae kwenye ***** wake akianza kuwasifu wanae na sijui bi mkora, mara kisamvu.
 
Hakika inasikitisha sana, ila akina Nape na Mwigulu bado wanabisha na kusisitiza kuwa CDM ni chanzo. Yana mwisho haya!
 
Back
Top Bottom