Mauaji Itigi: Msemaji wa Polisi asema kulitokea vurugu na inadaiwa Askari wa Wanyamapori ndiye aliyefyatua risasi

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,307
19,171
Nilijua hili litatokea, maana ni kawaida ya polisi. Jana nilisikiliza clip ya ofisa wa polisi akiongea waziwazi kuwa Mkurugenzi alimpiga risasi ya kichwa raia na kumuua. Akalaani sana kitendo hicho huku akisema kilikuwa wazi na kushuhudiwa.

Sasa Msemaji wa jeshi la Polisi amekuja na maelezo yake. Yeye anasema ilitokea kutoelewana na vurugu na askari wa wanyama pori walifyatua risasi ikamjeruhi raia, na akafa. Kwa hiyo alieua si Mkurugenzi kama watu wanavyosema, au ailivyosema ofisa wa Polisi kule Itigi.

Maelezo haya ya msemaji wa Polisi ni kauli nzito sana ambayo kwa kiasi fulani yanaweka mwanzo wa muuaji wa huyu raia kutochukulwa hatua. Wenye akili tunaelewa hii picha inaelekezwa wapi - kwamba risasi ilipigwa kwa kuwa kulikuwa na vurugu - huenda hata Mkurugenzi alikuwa akishambuliwa na ikabidi alindwe na wale askari wa wanyama pori - self defence.

Haya, yetu macho na masikio. Lakini nimeshaanza kuona hili suala linapelekwa wapi, indiketa zimeshapigwa kuashiria kona itakatwa hivi karibuni. NI wazi jela si kwa ajili ya kila mtu.

Habari Kamili.....
WATU watano, akiwamo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, wakituhumiwa kusababisha kifo cha mfugaji Peter Chambalo, anayedaiwa kupigwa risasi akiwa kanisani.

Akizungumza na Nipashe jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alikiri kutokea kwa tukio hilo juzi na kueleza kuwa mpaka sasa, wanaoshikiliwa ni watu wa watano akiwamo mkurugenzi huyo.

Msangi alitaja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni askari wanyamapori wawili, mmoja kutoka Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) na mwingine kutoka Halmashauri ya Ipigi, mwanasheria na mtendaji wa kata.

“Ni kweli tukio limetokea, lakini siyo kweli kuwa askari wa Jeshi la Polisi wamehusika na tukio hilo," Msangi alisema, "kwanza hawakuwapo kwenye tukio hili.

"Waliokuwapo ni askari wanyamapori, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, mwanasheria wake na mtendaji wa kata. Kilichotokea ni kwamba, walipofika katika kijiji cha Kazikazi, Kata ya Kitaraka, Tarafa ya Itigi, kulitokea kutoelewana, hivyo kusababisha vurugu," alisema.

Aliongeza kuwa, wakati wa vurugu hizo, inadaiwa askari walifyatua risasi na kumjeruhi mtu huyo ambaye alifariki dunia.

“Uchunguzi wa tukio hili unaendelea na hivi sasa Mkuu wa Mkoa huo, Kamanda wa Polisi wapo eneo la tukio kupata maelezo zaidi, hizi ndizo taarifa nilizonazo hadi sasa,” Msangi alisema.

Chanzo: Nipashe

Sehemu ya hotuba ya anaesemekana kuwa RPC wa Singida katika kuwatuliza wanacnhi alipotembelea eneo la tukio pale kanisani;

"Na mpaka nashindwa kuelewa huyu Mkurugenzi alikusudia nini. Alikuwa anatafuta nini. Hasa kwenye kipindi hiki. Na kwa nini uende kwenye nyumba ya ibada. Kwa nini uende nyumba ya ibada. Na uje ufanye mambo kama haya. Sasa tulikuwa tunaongea hatujafika kwenye eneo latukio. Sasa nimefika nimejionea mwenyewe. Wananchi mimi naendelea, na waumini wote kwa ujumla, naendelea kuwapa pole. Kitendo hiki kilichofanyika hakuna anaekubaliana nacho. Kama nilivyokwishasema pale barabarani, tutachukua hatua zinazostahili. Kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria. Hakuna aliye juu ya sheria. Hakuna aliye juu ya sheria. Suala hili ukiliangalia halikuwa na utashi wa busara hata kidogo. Hata matumizi yenyewe ya silaha , hata waliopiga mie nasema kwamba, sijui, huo ni ugaidi kwa kweli. Katika hali ya kawaida tunaojua ni watu wa namna gani, hawana silaha wala..."

Update:

Baba mzazi wa kijana aliyepigwa risasi, ambaye alikuwapo kwenye tukio, amesema yafuatayo;
1549438296739-png.1014803

Msemaji wa Polisi, ambaye hakuwapo kwenye tukio, anasema sio Mkurugenzi aliyepiga risasi ila askari wa Wanyama pori.

Sasa amua mwenyewe kile tunacholishwa na Polisi, na ni kwa lengo gani.

NB: Habari zisizothibitishwa zinasema DED aliyehusika katika tukio hili ni mtoto wa dada yake Raisi Magufuli.

Update: Polisi"Wamchomoa" Mkurugenzi tukio la mauaji Itigi

1549525660251.png
 
Write your reply...

Hawajasema kiwa

Kuwa risasi ilikata kona na kumfuata marehemu
Ila wewe nawe ulitegemea waseme kua DED ndo kauwa kapuku
Huwa hawasemi moja kwa moja Mkuu. Watasema kulikuwa na kutoelewana, kisha vurugu, askari wakapiga risasi hewani, na mtu mmoja kanisani akajeruhiwa, kisha akafa.

Huwa wako smart sana, wanaenda hatua kwa hatua kama mwendo wa pole kwenye gwaride!
 
Nilijua hili litatokea, maana ni kawaida ya polisi. Jana nilisikiliza clip ya ofisa wa polisi akiongea waziwazi kuwa Mkurugenzi alimpiga risasi ya kichwa raia na kumuua. Akalaani sana kitendo hicho huku akisema kilikuwa wazi na kushuhudiwa.

Sasa Msemaji wa jeshi la Polisi amekuja na maelezo yake. Yeye anasema ilitokea kutoelewana na vurugu na askari wa wanyama pori walifyatua risasi ikamjeruhi raia, na akafa. Kwa hiyo alieua si Mkurugenzi kama watu wanavyosema, au ailivyosema ofisa wa Polisi kule Itigi.

Maelezo haya ya msemaji wa Polisi ni kauli nzito sana ambayo kwa kiasi fulani yanaweka mwanzo wa muuaji wa huyu raia kutochukulwa hatua. Wenye akili tunaelewa hii picha inaelekezwa wapi - kwamba risasi ilipigwa kwa kuwa kulikuwa na vurugu - huenda hata Mkurugenzi alikuwa akishambuliwa na ikabidi alindwe na wale askari wa wanyama pori - self defence.

Haya, yetu macho na masikio. Lakini nimeshaanza kuona hili suala linapelekwa wapi, indiketa zimeshapigwa kuashiria kona itakatwa hivi karibuni. NI wazi jela si kwa ajili ya kila mtu.

weka hiyo clip tuone acha kufundisha watu kazi au kulisha watu maneno unayo yafikilia wewe.
 
Clip gani sasa unataka wewe mkurupukaji?

Kama ni ile ya ofisa wa polisi Itigi mbona ilishaondolewa saa nyingi! Nitakuwachia picha tu hapa chini. POlisi wanajua wanalosema au kufanya bwana. Nenda kwenye hii post uone kama utaipata -ilishazuiliwa!

Singida: Mkurugenzi(DED) wa Halmashauri ya Itigi adaiwa kumuua mwananchi kwa risasi - JamiiForums

Huyu aliyekuwa akizungumza hapo kwenye video clip ni ofisa wa polisi? Kama ni ofisa wa polisi kibarua chake kinaweza kuwa mashakani.
 
Nilijua hili litatokea, maana ni kawaida ya polisi. Jana nilisikiliza clip ya ofisa wa polisi akiongea waziwazi kuwa Mkurugenzi alimpiga risasi ya kichwa raia na kumuua. Akalaani sana kitendo hicho huku akisema kilikuwa wazi na kushuhudiwa.

Sasa Msemaji wa jeshi la Polisi amekuja na maelezo yake. Yeye anasema ilitokea kutoelewana na vurugu na askari wa wanyama pori walifyatua risasi ikamjeruhi raia, na akafa. Kwa hiyo alieua si Mkurugenzi kama watu wanavyosema, au ailivyosema ofisa wa Polisi kule Itigi.

Maelezo haya ya msemaji wa Polisi ni kauli nzito sana ambayo kwa kiasi fulani yanaweka mwanzo wa muuaji wa huyu raia kutochukulwa hatua. Wenye akili tunaelewa hii picha inaelekezwa wapi - kwamba risasi ilipigwa kwa kuwa kulikuwa na vurugu - huenda hata Mkurugenzi alikuwa akishambuliwa na ikabidi alindwe na wale askari wa wanyama pori - self defence.

Haya, yetu macho na masikio. Lakini nimeshaanza kuona hili suala linapelekwa wapi, indiketa zimeshapigwa kuashiria kona itakatwa hivi karibuni. NI wazi jela si kwa ajili ya kila mtu.
Ndio maana baadaya ya siku tatu ndo wanatoka mafichoni,hapo walikua wanapima kwanza upepo wa mamraka ya utezi.

walitegemea tanagu juzi kwamba msigwa wa ikulu angekua ashafanya yake ila wameona kimyaaaa kama hakijatokea kitu vile.

AMINI kuambia yule afisa wa police wa kule itigi anaweza ondolewa kwenye nafasi yake.
 
Nilijua hili litatokea, maana ni kawaida ya polisi. Jana nilisikiliza clip ya ofisa wa polisi akiongea waziwazi kuwa Mkurugenzi alimpiga risasi ya kichwa raia na kumuua. Akalaani sana kitendo hicho huku akisema kilikuwa wazi na kushuhudiwa.

Sasa Msemaji wa jeshi la Polisi amekuja na maelezo yake. Yeye anasema ilitokea kutoelewana na vurugu na askari wa wanyama pori walifyatua risasi ikamjeruhi raia, na akafa. Kwa hiyo alieua si Mkurugenzi kama watu wanavyosema, au ailivyosema ofisa wa Polisi kule Itigi.

Maelezo haya ya msemaji wa Polisi ni kauli nzito sana ambayo kwa kiasi fulani yanaweka mwanzo wa muuaji wa huyu raia kutochukulwa hatua. Wenye akili tunaelewa hii picha inaelekezwa wapi - kwamba risasi ilipigwa kwa kuwa kulikuwa na vurugu - huenda hata Mkurugenzi alikuwa akishambuliwa na ikabidi alindwe na wale askari wa wanyama pori - self defence.

Haya, yetu macho na masikio. Lakini nimeshaanza kuona hili suala linapelekwa wapi, indiketa zimeshapigwa kuashiria kona itakatwa hivi karibuni. NI wazi jela si kwa ajili ya kila mtu.

CHADEMA wanaofahamika hapo wajiaandae; kesi hiyo tayari wanayo.
 
Hongera! sikujua kama ww ni mtu wa harakati hizi, ila si kila mtu yupo kama unavyodhani eti ataku- spy ww, hasha sisi wengine tupo duniani hapa ili siku ipite..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, bado uko na mimi tu? Ni wana JF wangapi humu ndani umeomba wakupe namba yao ya simu ili muwasiliane kwa WhatsApp wakakupa? Labda wale wa Lumumba buku 7.
 
Back
Top Bottom