Matrekta ya 'Kilimo Kwanza' yanaozea Dodoma

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Kama ilivyo kawaida serikali yetu huanzisha mipango kabambe ambayo kwa sababu moja au nyingine utekelezaji wake huwa mgumu.Miaka michache iliyopita serikali ilikuja na mpango wa KILIMO KWANZA. Ili kukamilisha azma hiyo power tilers na matrekta yaliagizwa kwa wingi nchini ili wakulima waweze kuyanunua.

Jambo la kusikitisha ni kwamba yale yaliyopelekwa kwenye 'yard' ya Dodoma ni mengi na hayanunuliwi. Kwa sasa yamesongwa na kufunikwa na nyasi ndefu. Inasikitisha, na pengine naweza kusema serikali ilikurupukia mpango huo.
 
Tumeshawazoea,siasa kwanza utalaamu baadae! Hakuna kitakacho fanikiwa kwa mtindo huu.
 
Kumbuka matrekta yote sio ya serikali mengine yaliagizwa na watu binafsi kwa mkopo wa mashirika ya fedha ya kimataifa ( IMF na World bank) wakiwa moja ya wadhamini kwa ajili ya kilimo kwanza. Una uhakika gani kwamba yard hiyo inatunza matreta ya kilimo kwanza yaliyoagizwa na serikali?
 
Tuletee picha tuthibitishe siku hizi siasa nyingi

Mkuu hata picha sizihitaji maana haya ni kawaida tu TZ!! Kilimo kwanza ilikuwa idea ya watu weengine kabsa, ambao walikuwa hata ku-craft hawajamalizia, JK & fiasco wakaivamia kwa kasi...

Sasa hivi hata kuiongelea hatuwasikii, haiko hata synchronized kwenye mpango wowote ule wa maendeleo!! Ali muradi tu walishasema wanaacha yaende yenyewe!! Sasa hivi kavamia DAVOS na story zake za kawaida, blah blah bla.....sijui masive foreign investment...blah blah blah...baadaye anakinga bakuli, na kukunua suti anarudi na nguo mpya!!

My poor prezidaa...
 
Niko Dodoma ni mji mdogo mbona sijaona matrekta hayo yapo eneo gani la Dodoma na mimi nikajionee sasa hivi kama ni kweli. Nitauliza na wahusika kama nitawakuta
 
Kumbuka matrekta yote sio ya serikali mengine yaliagizwa na watu binafsi kwa mkopo wa mashirika ya fedha ya kimataifa ( IMF na World bank) wakiwa moja ya wadhamini kwa ajili ya kilimo kwanza. Una uhakika gani kwamba yard hiyo inatunza matreta ya kilimo kwanza yaliyoagizwa na serikali?

Mkuu unajua unachokiongea?
 
Kama ilivyo kawaida serikali yetu huanzisha mipango kabambe ambayo kwa sababu moja au nyingine utekelezaji wake huwa mgumu.Miaka michache iliyopita serikali ilikuja na mpango wa KILIMO KWANZA. Ili kukamilisha azma hiyo power tilers na matrekta yaliagizwa kwa wingi nchini ili wakulima waweze kuyanunua.

Jambo la kusikitisha ni kwamba yale yaliyopelekwa kwenye 'yard' ya Dodoma ni mengi na hayanunuliwi. Kwa sasa yamesongwa na kufunikwa na nyasi ndefu. Inasikitisha, na pengine naweza kusema serikali ilikurupukia mpango huo.

Tafadhali, mtoa hoja uko wapi? Niko Dodoma sema yako wapi? Nikashuhudie na kuondoa kiwingu cha siasa hapa JF
 
Kumbuka matrekta yote sio ya serikali mengine yaliagizwa na watu binafsi kwa mkopo wa mashirika ya fedha ya kimataifa ( IMF na World bank) wakiwa moja ya wadhamini kwa ajili ya kilimo kwanza. Una uhakika gani kwamba yard hiyo inatunza matreta ya kilimo kwanza yaliyoagizwa na serikali?

na yale ya jeshi yaliyojazana pale lugalo ni ya watu binafsi?
 
Taarifa imejaa porojo, usanii ni kama imetoka mtaa wa mchikichini karikaoo kwa wauza mitumba.
 
Kumbuka matrekta yote sio ya serikali mengine yaliagizwa na watu binafsi kwa mkopo wa mashirika ya fedha ya kimataifa ( IMF na World bank) wakiwa moja ya wadhamini kwa ajili ya kilimo kwanza. Una uhakika gani kwamba yard hiyo inatunza matreta ya kilimo kwanza yaliyoagizwa na serikali?

Nadhani swala sio tu nani kayaagiza, je matrekata hayo yaliyopo yanatumikaje? Kilimo kwanza ni mpango wa serikali inapaswa kufuatialia utekelezaji wake na kuhamasisha kilimo hicho. Kam ni ya watu binafsi yaliyoagizwa kwa ajili ya kilimo kwanza kutokana na mpango wa serikali kuendeleza kilimo, bado matrekta ni mtaji ambao serikali inapaswa kuutumia vyema.
 
Wafuasi wa CCM na Chadema mnapambana hata kwa tuhuma za kuzusha. Thibitisha.

athibitishe nini? ukweli ndo huo. hata hapo dar es salaam karibu na kambi ya jeshi ya rugalo matrekta yanaoza. kama upo dar kaangalie mwenye rugalo. sio kubisha bisha kitu usicho kijua. Mia
 
Tuletee picha tuthibitishe siku hizi siasa nyingi

10_10_xt8j07.jpg
 
Mimi nipo Dodoma nathibitisha kwamba yapo. Area D barabara ya kwenda Morogoro sehemu inayoitwa Njedengwa. Yapo mengi sana tu.
Kimsingi mpango wa trekta ungeliwezesha taifa sana katika mambo ya uchumi. Lakini ugumu unakuja pale ambapo unalima halafu mipaka ya nchi inafungwa na hawa viwavi jeshi. Hivi ni nani anayetaka hasara. Mimi ninunue trecta huku nikijua kabisa, nachezea shilingi kwenye mdomo wa choo? Haiwezekani hata kidogo.
Wengi tunapenda sana kutumia mashine kwenye kilimo lakini sera za nchi hii ni kama moshi ndani ya tembe siku ya mvua kubwa. Sheria zinazunguka tu, hazieleweki kabisa.
Unajua miaka haifanani, serikali ingekuwa na sera za kuwalinda watu wake, mfano umelima mwaka wa kwanza na umepata hasara. Kimsingi kungekuwa na tathmini na serikali ione ni kwa namna gani inaweza kumsaidia mtu huyu lakini ndo kwanza wanachelea kumpokonya kila kitu. Haya ndiyo matokeo yake. Nakwambia watashusha bei lakini bado yataoza.
 
MwanaJf wa dodoma kauliza hapo juu yako wapi lakini bado hajajibiwa?

Mie sio mwenyeji Dodoma, lakini ayasemayo mleta thread ni kweli, Yapo along Dodoma - Morogoro road, kama watokea Dodoma ni mkono wako wa kulia.
 
"Kilimo kwanza" was never intended to help the Tanzanian peasant. Ni mpango ulioandaliwa na wafanyabiashara ili kujinufaisha na mafungu ya pembejeo. Hakuna utaalamu wa kilimo au mifugo uliohusishwa kwenye andiko lote la mpango huu. Wapo wanaojiita Agroeconomists (sio wataalamu wa kilimo wala mofugo bali wachumi wa kilimo na mifugo) na wale wanaojiita Entrepreneurs (S&M enterprises) na walaji wakubwa wa TCCIA.

Serikali iliingizwa mkenge nao wakaenda kichwa kichwa.
 
Back
Top Bottom