Matokeo rasmi ya Uchaguzi mdogo wa mitaa Magu: CHADEMA yaigalagaza CCM

Safiiiiii sana hii ndio chakula ya masikio yangu aisee!!!!Nape wewe endelea kuiota CDM ukiamka utafanya yale yaliyofanywa na yule waziri wa Sadam akisema majeshi ya Marekani yamefukuziliwa mbali yalitaka kuuchukua uwanja wa ndege kumbe yapo katikati ya jiji la Bagdad.
 
14 bila kupingwa kwa vyenu vingapi?

Mnaleta hesabu nusu nusu, mnamdanganya nani zaidi ya nafsi zenu?
 
Fanya hivi: cc Nape Nnauye ili aweze kupata ujumbe mara apatapo muda. Wajuha tena, huyu ni mtu mzito mara nyingi ametingwa na majukumu mepesi hasa haya mapya ya kuthibitisha vyeti vya Mh. John Mnyika
Mkuu umeniacha hoi asee dah! Jf kuna watu.
 
Last edited by a moderator:
ccm ni kama wale wajenzi wa mnara wa babeli, sasa wanavuna matokeo ya kiburi chao!
 
Kaka Ritz,huo sio utamaduni wa mtanzania,njoo uwapongeze CHADEMA kwa ushindi wao bhana

cc Ritz
 
Matusi na unafiki wa kuidhalilisha CHADEMA unakimaliza CCM maana watu wanajua mti wenye matunda ndo hutupiwa mawe!
 
Fanya hivi: cc Nape Nnauye ili aweze kupata ujumbe mara apatapo muda. Wajuha tena, huyu ni mtu mzito mara nyingi ametingwa na majukumu mepesi hasa haya mapya ya kuthibitisha vyeti vya Mh. John Mnyika

Ha haa haaa,eti majukum mazito
 
Last edited by a moderator:
kama vile nimechelewa kuipata hii habari njema namna hii...Ngoja niende kwenye uzinduzi sasa....
 
Kulikuwa na uchaguzi mdogo wa mitaa miwili, vijiji 6 na vitongoji 37... Pia nafasi 120 za wajumbe wa serikali za vijiji.

CHADEMA kimeendelea kuitesa CCM ambapo kimezoa mitaa yote miwili (Bank & Ihimbili), vijiji vinne kikiwemo cha Nyahanga kata ya Sukuma ambapo Mbunge wa sasa wa Magu anatokea (viwili wamegawana CCM+UDP), wajumbe wa serikali za mitaa 80, vitongoji 16 kati ya 20 walivyosimamisha wagombea (2 CCM, 1UDP & 1CUF).

CCM imeanza kuaga pole pole!

MIZENGWE YA CCM itendelea kuifanya CDM kuimaarika zaidi sehemu zote za nchi hii.
 
RAHAAAA...UTAMUUUU.....HONGERENI SANA WANANCHI WA MAGU, NA MAKAMANDA WOTE MLIOFANIKISHA HUO USHINDI MNONO, TUKO NANYI DAIMA KWA MAOMBI. ''chadema ni chama cha wachagga???"
 
teh,teh,teh.......mbona unaongelea uvunguni?

Mimi au nyinyi, watu huweka matokeo kamili.

CCM ?

Chadema ?

UDP ?

CUF ?

Nyie mnawadanganya misukule wenzenu. Hata Urais mliwaambia mmeshinda! Ubunge mliwambia mmeshinda, tukifika bungeni tunaona hata robo ya bunge hamfiki. Kulikoni?
 
Back
Top Bottom