Matangazo ya biashara zetu ni kama mzaa

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
WAKUU salamu
mimi katika pita pita yangu hapa kwenye jamvi na kwenye website nyingi za wafanya biashara
maelezo ya biashara au matangazo yana maswali mengi kuliko msaada kwa mteja,

mambo kama bei na info za kutosha ni tatizo kubwa na vitu vingi bei zake sio fixed ni
mjadala.
nchi nyingi zilizo endelea bei za kujadiliana zimesababisha kampuni kukosa wateja na hivyo
kampuni nyingi zinaweka kila kitu wazi na hakuna kujadiliana bei maana muuzaji (cahier) hana mamlaka ya kubadilisha
bei yeye ni 'CUSTOMER SERVICE' tu

sasa basi kwa nini Tanzania makampuni yanaficha bei?
huu sio ukwepaji wa kodi kweli, au kumuibia mteja?
ni vitu vipi tuwashauri wenye makamupuni kama wateja waviweka mmoja kwa mmoja kwenye maelezo ya biashara zao?
serikali ina nafasi ya ku play katika hii michezo ya wafanya biashara?

nitakupa mfano wa matangazo hapo JF
Lingo ni kuwekana sawa sio kila siku tunalia tu na wachina mara wakenya yawezekana tunatatizo kubwa sehemu
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/145115-solar-power-kwa-bei-nafuu-2.html

https://www.jamiiforums.com/busines...947-nauza-computers-kwa-anayetaka-nyingi.html


https://www.jamiiforums.com/busines...-real-estate-development-partners-wanted.html

hiyo ni mifano tu karibu mambo yote ya biashara yanayoletwa hapo na kwingineko yanamapungufu makubwa sana ya taarifa.
nini chanzo au tatizo?
 
Matangazo ya biashara TZ ni masikhara. Kuna lile IVORI Tomato Sauce, yule mwanamke anadai kaletewa shampoo aoshe nywele.
 
Back
Top Bottom