Matajiri wa Tanzania ni Mabepari Wanyonyaji?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi, kwa kawaida huwa siangalii kipindi cha Ze Comedy Original cha kina Joti kinachorushwa na TBC kwa vile niliwaona kama waopuuzi puuzi fulani hivi, lakini leo imetokea niko mahali wao the comedy ndio kwao hivyo kujikuta naangalia.

Joti akaibuka analalamika jinsi wanavyomtumikia tajiri mmoja ambaye ni hodari kutoa misaada huku waajiriwa wake wakilia njaa kuwa wanalipwa mishahara midogo!.

Jee hoja ya Joti inaukweli wowote?. Jee hawa matajiri wetu nchini ni mapepari wanyonjaji wenye nia ya kujineemesha wao kwa kuwanyonya wengine kama wale tuliowakataa wakati wa Azimio la Arusha?!.
Au ni matajiri wenye nia ya kuwasaidia Watanzania kuboresha maisha yao kwa kutoa maslahi bora kwa watumishi wao?!.

Angalizo: Kwa vile Ze Comedy hawakutaja majina, naombeni wachangiaji msitaje majina ya hawa matajiri wetu!.
 
siku zote matajiri ni mabepari yaani wanyonyaji, ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu
 
Mkuu Pasco.
Ni kweli matajiri wetu ni wanyanyasaji sana halafu kwa picha ya nje uwa wanaoneka kama maraika..

Kuna tajiri mmoja Tanzania uwa anamilikiki vyombo vya habari.

Anawanyanyasa sana wafanyakazi wake mara hawakate mishahara wengine anawapunguzia mishahara, wengine anawafukuza bila kuwapa chochote.

Cha ajabu uwa anawakusanya viwete na kupata nao lunch huku kamera zikiwamulika!.
 
Mkuu Pasco.
Ni kweli matajiri wetu ni wanyanyasaji sana halafu kwa picha ya nje uwa wanaoneka kama maraika..

Kuna tajiri mmoja Tanzania uwa anamilikiki vyombo vya habari.

Ananyanya wafanyakazi wake mara hawakate mishahara wengine anawapunguzia mishahara, wengine anawafuza bila kuwapa chochote.

Cha ajabu uwa anawakusanya viwete na kupata nao lunch huku kamera zikiwamulika!.

hivi ni tajiri au alikuwa tajiri
nasikia anafilisika so fast....
 
Tajiri mnayomzunguzia si ndo huyu Mh.Machache? Haaaaaa kipindi kizima wamem-diss yeye,kuhusu anacopy majina ya vyombo vya habari vya nje anakuja kuweka kwake eg radio moko,kapitale tv,chaneli gwala,the gajian newz paper,ai tivii etc,pia amezungumzia kwamba tajiri gani mgonjwa? Anaenda kuflashiwa damu kila mwezi.
 
King Kong III, hilo la vituo vya Tv kuitwa majina ya kuibilizia nililisikia ila sikuconnect, bali nikajikuta nafanya mapitio karibu vituo vyote vya TV vilivyoko Dar es Salaam, vinatumia majina ya kizungu isipokuwa Tumaini.
 
itv ipo uk
the guardian ipo uk...
wamemponda Mengi kwa kuwa a franchisee na sio yeye kuwa na a franchise......
 
Inatakiwa itokee end of bujuazii kama ya urusi. Nilipita mlimani vijana ndio wazo lao inatisha
 
King Kong III, hilo la vituo vya Tv kuitwa majina ya kuibilizia nililisikia ila sikuconnect, bali nikajikuta nafanya mapitio karibu vituo vyote vya TV vilivyoko Dar es Salaam, vinatumia majina ya kizungu isipokuwa Tumaini.

Na Iman TV
 
Tajiri mnayomzunguzia si ndo huyu Mh.Machache? Haaaaaa kipindi kizima wamem-diss yeye,kuhusu anacopy majina ya vyombo vya habari vya nje anakuja kuweka kwake eg radio moko,kapitale tv,chaneli gwala,the gajian newz paper,ai tivii etc,pia amezungumzia kwamba tajiri gani mgonjwa? Anaenda kuflashiwa damu kila mwezi.

Kama wanafikiri kuna bepari asiyemnyonya mtumishi wake warudi wafundishwe kidogo mfumo wa kibepari. Kina Joti wanaweza kucomedisha wanavyoweza, ukweli, ni Mengi ndiye aliyewaweka mjini na hakuna haja ya kukaa wanasumbuana na mtu kwani kwa sasa wana maisha yao yanayoendelea (tena vizuri!!!!)

Long live bepari unayepondwa, uma na kupuliza inavyowezekana
 
itv ipo uk
the guardian ipo uk...
wamemponda Mengi kwa kuwa a franchisee na sio yeye kuwa na a franchise......
The Boss, niliomba tusitaje majina!. Ila hata kama ni kweli jinsi ze comedy wanavyoiweka, wanaiweka ki bifu bifu kitu ambacho sio kizuri haswa kwa kuzingatia ndiko walikoibukia!. Ukiondoka mahali ondoka kwa heshima ile kesho ukirudi ufunguliwe mlango!. Sio mahali panakutoa halafu wewe kila kukicha ni kukashifu na kukandia, sio fresh!. Huo ni ukosefu wa shukrani.
 
siwaungi mkono hata mimi
bila kutajana majina itakuwa ngumu kueleweshana
hata tofauti ya franchise na franchisee sijui kama inaeleweka kwa wengi...
hata hiyo yeye yale maji yake ni franchise...analipwa na cocacola....
 
Ukiwaona wanapenda sifa,wanapenda kupigiwa makofi,wanakaa viti vya mbele....utawajua tu kwa hulka zao lakini ndani mwao ni sawa na makaburi kwa ndani
 
King Kong III, hilo la vituo vya Tv kuitwa majina ya kuibilizia nililisikia ila sikuconnect, bali nikajikuta nafanya mapitio karibu vituo vyote vya TV vilivyoko Dar es Salaam, vinatumia majina ya kizungu isipokuwa Tumaini.

oh,na mlimani nao jina lao ni la kizungu Kumbe,
 
hata dtv ni Daresaalam television...
channel ten- ni tanzania entertainmen network...
 
wakuu hebu tukiangalie hiki:focus:

Tajiri mwema ni wewe mwenyewe pale usipoila ganji nafsi yako, ukishaajiri basi ndo unakutana na vibweka vya kina joti
 
Kama halipi workers c wakamshtaki au waache job? Cio muda wa kutafuta huruma ya solid majority wakutetee!
 
Back
Top Bottom