Mataifa Matatu Makubwa Duniani Kuongozwa Na Wanawake

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Ikiwa Hilary Clinton atafanikiwa kushinda uchaguzi wa Marekani ina maana mataifa matatu makubwa duniani yenye ushawishi wa kiuchumi na kijeshi yataongozwa na wanawake, mbali na Marekani kuna Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May na Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani.
Changamoto hawa kina mama watakaokutanao kwanza ni matatizo ya mashariki ya kati haswa kwa vita vya Syria na uhusiano wa mataifa hayo makubwa na taifa la Urusi.
Tukianza kuangalia uhusiano wa mataifa hayo na Urusi uko kwenye hali mbaya sana tokea kuangukaa kwa taifa la USSR imefikia hatua kwa mataifa haya kuonyeshana ubabe wa kijeshi mpaka kutaka kuanzisha vita vya tatu vya dunia.
Changamoto lingine ni matatizo ya Mashariki ya Kati wakati nchi hizi ikiwafurusha magaidi wa Islamic State kutoka Iraq, mataifa haya makubwa yanaunga mkono vikundi vya kigaidi nchini Syria katika kuendesha vita dhidi ya serikali ya Syria na hii ndio sababu kubwa ya kukosana na Urusi.
Mataifa haya pia yatakutana na changamoto ya kuchuana BRIC (Brazil,Russia,India and China) huu ni Muungano wa mataifa hayo kiuchumi na mataifa hayo yana mpango wa kuanzisha sarafu mbadala wa dola kwa matumizi ya kibiashara duniani.
Hilary Clinton akifanikiwa kushinda atakutana na matatizo makubwa ya kivita ambao yeye mwenyewe ndio alizianzisha akiwa Waziri wa Mambo ya nje ya Marekani (Syria na Libya).
Yetu macho tusubiri matokeo ya uchaguzi wa Marekani.
 
Hillary hawezi kushinda marekani sasa hivi anatakiwa mtu mbabe mtu wa vita akafyeke magaidi wa IS Lakini awe stand by maana mda wowote inawezekana kulipuka world war III
 
Dunia ya leo sio ya Vita vya silaha baina ya Nchi na Nchi, tunashuhudia miaka ya hivi karibuni technolojia zinazohusu zana za kijeshi zimekuwa za hali ya juu ukilinganisha miaka 20 iliyopita vita vikipiganwa maafa na uharibifu pande zote zitakuwa kwa kiwango cha kutisha , achilia mbali vita vya ndani vya uasi kama vya Syria , Iraq, Libya, Sudan ya kusini...

Hawa viongozi wa jinsia ya kike huenda wakatoa mchango mkubwa kuiweka dunia sehemu salama kwa maisha ya mwanadamu... huku nikimkumbuka magreth tacha aliyekuwa waziri mkuu wa uengereza the iron lady
 
Back
Top Bottom