Maswali tata kuhusu utekwaji na upatikanaji wa Mohamed Dewji MO

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,505
31,176
1. MO ametekwa katika maeneo salama sana Tz

2. MO ameachiwa katika maeneo salama na bora sana Tanzania

3. Watekaji wa MO wamekuwa na safe exit na safe entrance katika maeneo salama sana Tanzania

4. Kwanini àachiwe baada ya press ya Sirro?

5. Alikuwa ndani ya epicenter/radius isiyozidi km 10 toka eneo alipotekewa

6. Maeneo yote ya matukio ni impenetrable bila vyombo kujua unless tuambiwe tz is no more a safe place

7. Mamlaka zinajua kila kitu swali ni je why MO and whose next

....endeleza maswali yako yenye wasiwasi juu ya misheni hii ya kishamba
swali.jpeg

Dp3vxMkWwAEVUy1.jpg

Gari iliyooneshwa kwa Wanahabri VS Gari iliyotelekezwa na watekaji

1. Familia inasema ni mzima kwa 100%. Mmeshafanya medical check up kujiridhisha hilo?

2. Mmesema alipiga simu nyumbani, mwanzoni ilisemekana alidondosha funguo za gari na simu. Vipi ni simu gani ametumia? Ilishindikana Ku trace hiyo namba siku zote hizi? Kwa siku zote simu haikuisha chaji?

3. Gari iliyoonekana kwenye pic Jana ulikuwa na sehemu ya kufunga spear tyre. Mbn hii haina?au walikata

Tumshukuru Mungu kapatikana

La msingi sana ni kuwa Mo amerudi.hili ni jambo kubwa na maana sana kwetu. Haya maswali kadhaa sasa yanahitajika majawabu. Sidhani kama askari sasa wamefunga file la kesi ya kutekwa/kuchukuliwa Mo.kwa kuwa amerudishwa.
1. Lengo la hao watekaji au wachukuaji lilikuwa nini?

2. Je wamefanikisha walichotaka na kama ndiyo kwa kiasi gani?

3. Ujasiri wao mkubwa wa kumteka pale alipokuwepo bila kujali eneo husika kuwa ni eneo lenye ulinzi wa cctv camera ulichochewa na nini?

4. Makubaliano gani wamefikia na Mo ili wasije mteka tena au sasa kusitokee hali ya mashaka kwa matajiri wengine?

5. Lile gari na zile picha alizoonesha kamanda yeye alipiga hizo picha gari likiwa wapi?na je sasa ataweza kuonesha picha za cctv cameras ili kuwaondoa mashaka watanzania?

6. Ni kosa gani alilifanya Makonda before ambalo waliamua lisitokee tena na kumtaka sasa anyamaze asizungumzie tena suala hili kwnye Jiji lake yeye akiwa Mwenyekit wa Usalama?

7. Jitihada za polisi zilifikia wapi mpaka kufikia hatua ya jana jamaa waliomchukua kuamua kumrudisha.

8. Wale waliotajwa kukamatwa je wanahusika vipi na tukio hilo na umma ufaham mwendelezo wa kesi zao mahakamani.

9. Tetesi nyingi za kuhusishwa serikali zitaondolewa vipi na kwa nini wananchi wahusishe serikali yao na ugaidi?

10. Je kamanda alijuaje kuwa waliomteka ni wazungu na hali walivaa mask.lakini maelezo ya mo yanasema wanaongea kwa lafudhi ya lugha mojawapo ya South Afrika. Je ye Mo anajuaje kuwa ni ya South Afrika na si sehemu nyingine ya Tz Au Dunia? Simu aliyoitumia Mo kutoa Taarifa kwao aliipata wapi? Na kwa nini jeshi liiifuatilie?


Sasa watanzania tusiishie kusherehekea kupatikana kwa Mo. Twendeni ndani zaidi ukweli uanikwe ufahamike wazi.

Hii tabia ya kupanga njama mnatekana kwa faida ya kuwatesa wengine iishe mara moja.

Maswali yangu ni kama yafuatayo,
1. Mo alipata wapi simu ya kupiga nyumbani?
Alipewa na watekaji? Kwamba watekaji walikuwa wanamuonea huruma?

2. Kwanini Mo anamshukuru Rais?
Mbona siasa inaingizwa hapa mtu fulani kukuzwaa?

3. Kwanini Inaonekana Jeshi la Polisi halishughuliki na waliomteka Mo?
Kupatokana kwake ndio biashara Imekwisha?


4. Kama hawa watu waliingia kupitia mpakani hakuna rekodi zao pale?

Mo Hukutekwaa, wewe na bashite acheni kutuchezea michezo michafu.

Tajiri mkubwa unakuwa na mambo ya kiswahili.

Na Malisa GJ anaandika.

Namshukuru Mungu kwamba MO ameachiwa huru kutoka mateka alipokuwa kwa muda wa siku 9. Mimi ni mmoja wa watanzania wengi waliomuombea apatikane akiwa salama, kama navyomuombea kila siku swahiba wangu Ben Saanane, Azory na wengine.

Pamoja na kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa 'KAZI KUBWA' waliyofanya kumpata MO bado kuna maswali machache ya kujiuliza;

1. Mtu aliyetekwa akipatikana hatua ya kwanza si huwa anapelekwa hospitali kuchunguzwa afya yake then polisi kutoa maelezo. Au ni nyumbani kwake kunywa nae chai na kumuuliza anajisikiaje?

2. Kutokea Viwanja vya Gymkhana alipotupwa MO hadi 'Ikulu' ni kama kilomita 1.5 hivi. Bila shaka eneo lote hili lina Ulinzi mkali sana. Sasa ni nani anayejiamini amteke MO na kwenda kumtupa eneo la aina hiyo? Maana hapo watekaji wamejirisk, wangeweza kukamatwa muda wowote.

3. Kama 'SisiTv' zilionesha watekaji walielekea maeneo ya Kawe, kwanini hawakumtupa Tegeta, Mabwepande, au Kawe beach ambako ni 'safe' kwao kuliko kuja kumtupa Gymkhana ambapo wangeweza kukamatwa kirahisi? Watekaji hao wanajiamini kiasi gani?

4. Taarifa za awali za jeshi la Polisi zilisema MO alidondosha simu yake na ufunguo wa gari wakati akipambana kujiokoa alipotekwa. Sasa hii simu aliyoitumia jana kuwapigia wazazi wake alipata wapi? Je alikua na simu nyingine? Je watekaji walimuacha nayo? Je walimuwekea na chaji? Maana siku 9 alizokaa mateka ingekua imeisha charge. Kama ndivyo basi hawa watekaji ni 'walokole'. Somebody say 'amen'.

5. Kutokea 'keepleft' cha Kawe hadi viwanja vya Gymkhana ni kama kilomita 18 hivi. Eneo lote hili lina askari wa doria usiku kucha. Ukitoka posta kuanzia saa 7 usiku unaweza kupishana na gari ya doria pale Salender kuelekea UN road, ukifika Ubalozi wa Ufaransa unakutana na nyingine, St.Peters nyingine, Polisi Oysterbay nyingine, hadi ufike Kawe utakutana na nyingine kama 3. Je wote hawa hawakuiona gari ya watekaji tangu inatoka Kawe hadi Gymkhana?

6. Kwanini gari ileile waliyoitumia kumteka MO ndio gari hiyohiyo wameitumia kumrudisha nayo? Ina maana hawakuogopa kwamba gari yao inajulikana? Yani walichofanya ni kubadili namba tu? Hawa watekaji watakua na akili ndogo sana. Sema amina.!

7. Halafu kwanini waitelekeze hiyo gari hapo Gymkhana? Kama waliweza kumchukua nayo MO, wakakaa nayo kwa siku 9, wakamrudisha nayo, kwanini hawakuondoka nayo baada ya kumfikisha Gymkhana? Ina maana waliogopa wangekamatwa? . Kwanini wahofie kukamatwa wakati wa kurudi na sio wakati wa kuja? Kama ni hofu ya kukamatwa ilitakiwa wawe nayo wakati wanaitumia kumpeleka MO Gymkhana, lakini baada ya kumdrop hawakupaswa kuwa na hofu yoyote.

8. Usiku huo wa manane waliondokaje pale Gymkhana kama gari waliiacha? Waliondoka kwa mguu, kwa bodaboda, au walikuja na gari nyingine? Kama walikuja na gari nyingine kwanini waache silaha kwenye gari waliyoitelekeza? Si wangezihamishia tu kwenye hiyo gari nyingine then waache hiyo Surf hapo Gymkhana bila kitu.

9. Kama watekaji wanaweza kumteka mtu na kumtelekeza just kilometa moja na nusu tu kutoka Ikulu na wasijulikane, hii si habari njema. Ina maana Ikulu inalindwa na watu ambao hawawezi kujua tukio la kilometa moja na nusu tu kutokea walipo? This is shocking. Marekani walinzi wa WhiteHouse wanamonitor kila kitu kwenye mzingo wa kilomita 100 kutoka ilipo ikulu. Hapa kwetu just kilomita moja na nusu askari hawajui?

10. Je, nia ya watekaji ilikua nini? Maana hawajadai Ransom. Je ni kumkomoa MO? Je ni kuleta taharuki kwa taifa? Je ni Kuonesha kwamba wana nguvu za kumteka mfanyanyabiashara mkubwa jirani na nyumba ya Makamu wa Rais halafu wakamrudisha jirani na makazi ya Rais bila kukamatwa? Lengo lao hasa lilikuwa ni nini?

Malisa GJ
 
HZ CONSIPIRACY theory tuwaachie mbele wabongo hatuwez hata chembe,

Jf Kennedy alikula chuma mbele ya kamera, mbele ya raia, mbele ya secret service, mbele ya jesh, mbele ya polisi, mbele ya FBI na mbele ya raia zaid ya 1000, lakn mhusika mkubwa mpk leo n kitendawili, kila aliekua anajua ukweli akielekea kubainika nae anakula chuma mapema sana, Kuanzia Osward, Jack Rubby, R. kennedy n.k, walikula chuma watu zaid ya 16 in raw with no delay,
Mpk leo hakuna anaejua moja kwa moja nani alihusika, Wengne wanasema Cuba, wengne Mafia, Wengne Rais johnson, wengne upinzan, wengne wazungu wabaguzi waliokua wanapnga usawa, wengne Urusi, na wengine serikali n.k n.k, Warren Commission walichunguza wakajichokea mwishowe wakasema basi tuhitimishe kwa kusema 'Muuaji ndo Muuaji' yan kwa ufup kama hupat hata dot ya kumuunganisha muuaji n mwingne basi hamna jinsi utasema muuaji alikua mwenyewe,
BTW hatuna hata uhakika kama hata huyo Osward kweli alihusika, haya imagine Rais anakula chuma mbele za watu tena live kwenye Tv lakn muuaji humjui.

Angalia huku futuhi land sasa,
Nyerere alikua smart sana alipokua anafanya mambo yake, utaishia kudhania tuu, he never leave any room of proof upart from common minor doubts(this is human nature) to majority.
Ipo siku watalipa maovu yao hata isiwe hapa, walioshka nch wamekosa roho za utu kbsa, burshit....
 
HZ CONSIPIRACY theory tuwaachie mbele wabongo hatuwez hata chembe,

Jf Kennedy alikula chuma mbele ya raia, kila aliekua anajua ukweli akielekea kubainika nae anakula chuma mapema sana, Kuanzia Osward, Jack Rubby, R. kennedy n.k
Mpk leo hakuna anaejua moja kwa moja nani alihusika Warren Commission walichunguza wakajichokea mwishowe wakasema basi tuhitimishe kwa kusema 'Muuaji ndo Muuaji' yan kwa ufup kama hupat hata dot ya kumuunganisha muuaji n mwingne basi hamna jinsi utasema muuaji alikua mwenyewe,
BTW hatuna hata uhakika kama hata huyo Osward kweli alihusika.

Angalia bongo land sasa,
Wazee Nyerere alikua smart sana alipokua anafanya mambo yake, utaishia kudhania tuu, he never leave any room of proof upart from minor doupts to majority.
Mungu akutafutie shida ujue shida ya wenzio
 
Back
Top Bottom