Maswali na ushauri kwa Malinzi

Jamal Malinzi

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
710
650
2.jpg

Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii. Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri, namshukuru.

Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali, kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.

Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa JamiiForums.

Jamal Malinzi,

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu

Dar es Salaam

4 Februari 2014.
 
Tunakushukuru sana kuwa karibu na jamii unayoitumikia. Kwa kweli soka letu linahitaji kuondokana na dhana ya usimba na uyanga
 
Jamal
Tunakushukuru kwa kuungana nasi kwenye uzi huu ili tukupe ushauri na maswali.
Swali ;
Kumekuwepo na manung'uniko juu ya kuiendesha TFF kwa misingi ya ukabila, hasa ukipendelea watu wa Kabila lako. Unaweza kulisemea vipi jambo hili ili kuwahakikishia Watanzania soka lisilo na mizengwe?
 
Ni vizuri Jamal Malinzi ajibu hili swali kwani linajirudia mara kwa mara....Linakera!
 
Last edited by a moderator:

nitonye usimba na uyanga una faida na hasara zake.Ni kweli kuna vilabu vilikuwa na timu nzuri lakini uyanga na usimba ukawaponza na mfano mzuri ni Pamba ya kina George Masatu,Nico Bambaga na wenzao.Lakini upande wa pili hivi vilabu ni crowd puller na vilabu vyetu kimapato vinategemea sana mechi zao dhidi ya Yanga na Simba.Hata wadhamini wengi wanautaka mpira kwa sababu hii.Derby ya Tanzania ni moja ya derbies sita kubwa Africa kwa sasa,yaani mechi ya simba vs yanga.
 
Last edited by a moderator:
Jamal
Tunakushukuru kwa kuungana nasi kwenye uzi huu ili tukupe ushauri na maswali.
Swali ;
Kumekuwepo na manung'uniko juu ya kuiendesha TFF kwa misingi ya ukabila, hasa ukipendelea watu wa Kabila lako. Unaweza kulisemea vipi jambo hili ili kuwahakikishia Watanzania soka lisilo na mizengwe?

hsbaky kuna mtu alifungua thread humu jf kuhusu hili jambo nikajibu mpaka nikachoka,naomba utafute hiyo link utaipata.
Kimsingi mimi ninaangalia uwezo wa utendaji,malumbano ya ukabila tukianza kuya entertain kesho yatakuja ya udini matokeo yake tutapoteza mwelekeo,siko tayari kwa hilo.Na kimsingi sitazungumzia tena hili jambo.Nisamehe kwa hilo.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kipindi ulizuka mgongano wa kimaslahi kati ya tff na african lyon kuhusu kudhaminiwa na kampuni ya simu na tff waliwakatalia lkn inaonekana hiki kitu kinawatafuna nyinyi leo kwa ticket za electronic sbb huwezi kununua ticket kwa mtandao mwingine zaidi ya vodacom wakati wenye jukumu la kuuza yani crdb wanaweza kuungunisha huduma za kimtandao na mitandao mingine
Kwa nn msipotie hiyo mikataba na kuifanyia maboresho sbb naamini ipo siku matashindwa kuingia mkataba na kampuni za pombe kudhamini ligi sbb kati ya washirika wenu haruhusu pombe kwenye media yake wala uwanja wake
 
Ni vizuri Jamal Malinzi ajibu hili swali kwani linajirudia mara kwa mara....Linakera!

Dark City hakuna haja ya kuhangaika na jambo ambalo halina tija.Mambo ya msingi ya kujadili ni vipi tucheze Afcon Morocco mwakani,ni vipi tunaanda timu zetu za vijana na za wanawake,TFF ipate wapi vyanzo mbadala vya mapato ili yatumike kwenye miradi ya youth,tunazibaje mianya ya wizi wa mapato,tunajengaje mahusiano na vyama vya nchi zilizoendelea,ni mtaala upi utumike kufundisha mpira Tanzania,Academies zetu tunaziongezeaje uwezo wa kukuza na kulea vipaji na kadhalika.Tuachane na mambo ya personality tuhangaike na issues.Anayengang'ania ukabila kwa vyovyote vile ana lake jambo,tusimpuuze,tufuatilie tujue hidden behind kuna ajenda gani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JM.
TFF imejipanga vp kuuboresha uwanja wa taifa, kwa maana ya pitch? sababu katika mechi ya juzi uwanja umeanza kuonekana kuwa na vipara, wakati kulikuwa na takribani mwezi mzima wa kushughulikia hilo, kabla mzunguko wa pili haujaanza?
 
Ahsante sana mkuu Jamal Malinzi kwa kutoa majibu kuhusu hili jambo. Nakerwa sana na mijadala au mambo yanayojikitia kwenye ukabila, udini na upuuzi mwingine wa namna hiyo!

Kama ulivyosema, kuna mtu alianzisha uzi wakati uko likizo na bahati mbaya sikurudi kuangalia kama ulijibu. Naridhika na majibu uliyotoa hapa. Kwa sababu kama mko waangalifu na mnalifuatilia jambo hili basi hata katika utendaji mtatafuta tija badala ya kukimbizana na vivuli vya watu wa nje ambavyo lazima vingewatoa kwenye hoja/mstari.

Sasa kwa vile siku 100 za wewe kuwa madarakani zimeshatimia, unaweza kutueleza kwa ufupi utekelezaji wa ahadi zako ulizozipa kipaumbele katika muda huu??
 
Last edited by a moderator:
Mimi ningependa nijikite moja kwa moja kukuuliza maswali ya msingi.
1. Baada ya challenge Nairobi ulisema mnachukua maamuzi magumu kwenye benchi la ufundi lakini sijaona hayo maamuzi mpaka sasa wakati muda wa timu kuingia kwenye mashindano (AFCON) unazidi kusogea.
2. Hivi uteuzi wako wa wajumbe wa kamati za TFF unaangalia vigezo gani mbona watu ni wale wale walioshindwa kuufanyia chochote mpira wetu.
3. Mimi ni mfatiliaji mzuri wa Ligi daraja la kwanza (naamini ikiboreshwa italeta tija sana kwenye soka letu) kuna hili sakata la mechi kati ya STAND UNITED na KANEMBWA mbona mikanda ya video iko wazi wachezaji wa timu ya Kanembwa walimpa kisago mwamuzi je ni sahihi mechi hiyo kurudiwa? je sheria ndio inasema hivyo.
 
Kuna kipindi ulizuka mgongano wa kimaslahi kati ya tff na african lyon kuhusu kudhaminiwa na kampuni ya simu na tff waliwakatalia lkn inaonekana hiki kitu kinawatafuna nyinyi leo kwa ticket za electronic sbb huwezi kununua ticket kwa mtandao mwingine zaidi ya vodacom wakati wenye jukumu la kuuza yani crdb wanaweza kuungunisha huduma za kimtandao na mitandao mingine
Kwa nn msipotie hiyo mikataba na kuifanyia maboresho sbb naamini ipo siku matashindwa kuingia mkataba na kampuni za pombe kudhamini ligi sbb kati ya washirika wenu haruhusu pombe kwenye media yake wala uwanja wake

uko sahihi kabisa na hoja zako ni za msingi.Wakati wa contract reviews yote haya tutayazingatia.
 
Mkuu JM.
TFF imejipanga vp kuuboresha uwanja wa taifa, kwa maana ya pitch? sababu katika mechi ya juzi uwanja umeanza kuonekana kuwa na vipara, wakati kulikuwa na takribani mwezi mzima wa kushughulikia hilo, kabla mzunguko wa pili haujaanza?

Bahati mbaya viwanja hatuvimiliki,sisi tunakodi tu kwa ajili ya mechi.Tunaloweza kufanya ni kusimamisha matumizi ya uwanja husika hadi wamiliki waurekebishe.Ila tumeanza kukamata maeneo tukianzia na Tanga.
 
Je ndugu mwenyekiti Jamal Malinzi hauoni umuhimu wa kuongeza idadi ya timu kwenye ligi kuu ya Vodacom? Ligi yetu ina timu chache sana kiasi kwamba kunakuwa na mapumziko ya muda mrefu ambayo yanashusha viwango vya wachezaji na kuathiri vilabu pamoja na national team?
 
Mimi ningependa nijikite moja kwa moja kukuuliza maswali ya msingi.
1. Baada ya challenge Nairobi ulisema mnachukua maamuzi magumu kwenye benchi la ufundi lakini sijaona hayo maamuzi mpaka sasa wakati muda wa timu kuingia kwenye mashindano (AFCON) unazidi kusogea.
2. Hivi uteuzi wako wa wajumbe wa kamati za TFF unaangalia vigezo gani mbona watu ni wale wale walioshindwa kuufanyia chochote mpira wetu.
3. Mimi ni mfatiliaji mzuri wa Ligi daraja la kwanza (naamini ikiboreshwa italeta tija sana kwenye soka letu) kuna hili sakata la mechi kati ya STAND UNITED na KANEMBWA mbona mikanda ya video iko wazi wachezaji wa timu ya Kanembwa walimpa kisago mwamuzi je ni sahihi mechi hiyo kurudiwa? je sheria ndio inasema hivyo.

1.Tuko kwenye mchakato wa kuisuka upya idara ya ufundi.Taarifa zaidi zinakuja.
2.Uzoefu ,uwezo na uadilifu ni vigezo muhimu katika uteuzi wa kamati.Tuliowateua tunaamini watatusaidia.
3.Kamati ya utendaji imeagiza maamuzi kuhusu mechi ya kanembwa vs stand united yapitiwe upya na pia kamati ya nidhamu iwashughulikie wenye tuhuma za utovu wa nidhamu.
 
Jamal Malinzi sijuhi kama lishaulizwa au la.

Ni nini hatma ya Electronic Tiketi ?
mimi naziunga mkono kwani hizi zitasaidia kuhakikisha mapato yanapatikana yote bila kuibiwa pia itasaidia ukusanywaji wa kodi kwa TRA.

Juzi nimeona Tanga manager wa uwanja akilalamika lakini hakika kw akumuangalia usoni anacholalamikia ni ukosefu wa hela za kuiba maana mapato yote yanenda CRDB na hakuna habari ya kupokea hela mkononi.
 
Electronic ticketing kusema kweli Ndiye mkombozi wa mapato ya Milangoni.Ila kuna changamoto ambazo inabidi tukabiliane nazo.Tayari tumekaa na washirika wetu CRDB kutafuta namna ya kurekebisha taratibu zake,TFF haiko tayari kuhatarisha Maisha ya watazamaji,tuwe na subra.Imani yetu ni kwamba tutafikia mahali tuondoe kasoro zote kwa faida na usalama wa wadau wote wa mpira nchini mwetu.
 
Last edited by a moderator:
1.Tuko kwenye mchakato wa kuisuka upya idara ya ufundi.Taarifa zaidi zinakuja.
2.Uzoefu ,uwezo na uadilifu ni vigezo muhimu katika uteuzi wa kamati.Tuliowateua tunaamini watatusaidia.
3.Kamati ya utendaji imeagiza maamuzi kuhusu mechi ya kanembwa vs stand united yapitiwe upya na pia kamati ya nidhamu iwashughulikie wenye tuhuma za utovu wa nidhamu.

Kwa style hii RAIS utafanikiwa kujua mengi ni watendaji wako tu kuchapa kazi tulio wengi tunapenda kuona mabadiliko makubwa kwenye uendeshaji wa soka letu mimi binafsi naunga mkono baadhi ya maamuzi yako hasa suala la soka la vijana.

Ila niwe muwazi najua upo karibu na watu kama KABULU GEOFREY mwambie kabisa apunguze unazi wake wa wazi wazi kama ameamua kuwa ndani ya chombo kinachosimamia mpira kitendo alichoonesha mechi ya mtani jembe kinaleta taswira mbaya ameamua kuwa TFF apunguze unazi wa hadharani hawa ni watu wanaweza kuharibu taswira ya uongozi wako mapema.

Pia tunaomba uangalie jinsi ya kuandaa utaratibu wa kureview mikataba ya watangulizi wako hasa mikataba ya udhamini wa ligi kuu kwa maana mkataba na vodacom na azam kuna makungufu ni kuna kila dalili kuna robbing fulani ilifanyika pande zote hazikushirikishwa ipasavyo.
 
hsbaky kuna mtu alifungua thread humu jf kuhusu hili jambo nikajibu mpaka nikachoka,naomba utafute hiyo link utaipata.
Kimsingi mimi ninaangalia uwezo wa utendaji,malumbano ya ukabila tukianza kuya entertain kesho yatakuja ya udini matokeo yake tutapoteza mwelekeo,siko tayari kwa hilo.Na kimsingi sitazungumzia tena hili jambo.Nisamehe kwa hilo.

Mwanzo nilifikiri ni mwanamapinduzi wa soka letu lakini tokea uoneshe makucha yako kwenye swala hili sina imani na wewe na nitaungana na wale wote watakaoamua kukupiga vita.

Hivi unataka kutua ambia katika makabila mengine hakuna watu wenye uwezo katika hizo nafasi?

Usilete siasa katika mpira mkuu, humu sio FB, humu wapo watu wanaojua vitu na uelewa mpana wa mambo, hayo amajibu yako kwenye hoja nzito kama hii ni ya kitoto na uzito wake ni mdogo sana.

Ninachojifunza kupitia majibu yako ni uwezo wako wa kutukana makabila ya wenzio kwamba hayana uwezo wa kuongoza katika soka. Sio siri nime dispear sana na uongozi wako.

Nahisi machungu yangu ya TENGA wala hayajawezi kupoa tena ndio kwanza unazidi kuyaongeza.

Wape hi wahaya wenzio wenye uwezo wa kuongoza soka.
 
Dhana kwamba wahaya wenzie ndio wenye uwezo tu ni upuuzi uliopita mpaka. Kama Tenga angekuwa na mawazo finyu kama hayo, bila shaka angejaza wachaga wengi tu maana wenye sifa wapo lukuki.
Ukiwa kiongozi haya ni mambo ya kuzingatia. Hatuwezi kuwa kama nchi moja jirani wenye tabia ya kuwafikiria watu wa kabila zao tu.
Hoja kwamba tuwache wafanye kazi haina msingi maana tunaanza kujenga ukabila kuanzia kwenye mpira. Hayo tuwaachie wanasiasa. Ajabu ni kwamba hata wao wanajitahidi kukwepa hilo.
 
Back
Top Bottom