Maswali na majibu kuhusu Biblia (bible): Tukutane hapa

Hepatis B

Senior Member
Feb 11, 2013
184
130
Nimekuwa na maswali mengi kuhusu biblia pindi navyoisoma na kukosa majibu au mtu wa kumuuliza kwa wale ambao Mungu amewapa uwezo wa kutafsiri kitabu hiki kitakatifu ninaomba mtupe majibu yenu hapa.

Kwa kuanzia naomba niulize swali. Bible inasema Mungu alimuumba Adam na Hawa. Ila ukija kusoma katika bible unaona kama walikuwepo watu wengne duniani kwa mfano katika Mwanzo 4. Adamu na Hawa walikuwa na watoto wawili Kain na Habili baada ya Kain kumuua Habili mazungumzo kati ya Mungu ya Kaini yaliashilia kuna watu wengine zaidi ya Adam na Hawa.

Mwanzo 4: 1-15.

1 Adam akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, "nimepata mtoto mwanaume kwa bwana."
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, "Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde."
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, "Twende uwandani" Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, "Yuko wapi Habili ndugu yako?" Akasema, "Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"
10 Akasema, "Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia katika ardhi!
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao dunian."
13 Kaini akamwambia Bwana, "Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua."
15 Bwana akamwambia, "Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipiziwa kisasi mara saba." Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

Swali langu ni hili, hao watu ambao wangemzulu Kaini ni watu gani ni wazazi wake Kaini ambao ni Adamu na Hawa au kulikuwa na watu wengine ambao Kaini alikuwa anawaofia? Na kama ni wazazi wake kwanini biblia haijaweka wazi kuwa walikuwa wanawazungumzia Adam na Hawa? Naombeni msaada kwa watu ambao mmeelewa icho kifungu mnisaidie. Natunguliza shukrani.
 
Ni sawa biblia haijaandika kila kitu.
Kuna mengi tu hayajawekwa mf uzao wa kainibuliendelezwa na nani? Maana haitajwi kama Eva alizaa mtoto wa kike.

Pale Mungu alivyo mwambia vile Kaini vile.... Ilimaanisha kwa vizazi vijavyo ile laana itakuwa palepale
 
Hiyo nchi ya Nodi watu wake waliumbwa na nani? Mr Mushi92
 
Attachments

  • 1442649392087.jpg
    1442649392087.jpg
    64.3 KB · Views: 3,359
Last edited by a moderator:
Mungu aliumba wayahudi wengine walishakuwepo kwa mabilioni ya miaka.
 
Tukiachana na mambo ambayo hayakuandikwa kwenye bibilia ila tukumbuke kwamba watoto wakike hawakuhesabiwa katika bibilia hivyo basi kuna uwezekano mkubwa kwamba adam na hawa walikuwa pia na watoto wa kike.

Sawa. Na vipi kusema mungu ni mmoja na hana mshirika? Check hapa👇anasemaje?
 
Attachments

  • 1442650779913.jpg
    1442650779913.jpg
    63.8 KB · Views: 3,052
Punguza ukali wa maneno. Hawachelewi kuingia mitini
Bibilia inaposema "umelaaniwa wew katika ardhi" inamaana kubwa sana kwamba ardhi na vitu vilivyopo juu ya ardhi havitakukubali ni pamoja na wanyama wa mwituni ukisoma bibilia ya kiengereza inawezakuwa na tafsiri nzuri kidogo...yeyote atakae muona kaini sio lazima awe mtu hata mnyama wa porini
 
Ndugu ndetia naona wewe unajitahidi kajibu maswali ya watu. Je? Utakuwa tayari kajibu maswali magumu yatakayoulizwa?
 
Last edited by a moderator:
Sawa. Na vipi kusema mungu ni mmoja na hana mshirika? Check hapaanasemaje?
Yes mungu ni mmoja na hana mshirika ila wapo malaika anaposema"huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya"alikuwa anawaambia malaika, hata pale nyumban kwako yupo baba, mam na watoto ila baba nafasi yake ni ya pekee haina ushirika
 
Kwanini mungu mwenye uwezo wote, upendo wote, muumbaji wa vyote na aliyeko kila mahali aliumba ulimwengu unaowezekanika kufanyika mabaya ya kila aina?
 
Bibilia inaposema "umelaaniwa wew katika ardhi" inamaana kubwa sana kwamba ardhi na vitu vilivyopo juu ya ardhi havitakukubali ni pamoja na wanyama wa mwituni ukisoma bibilia ya kiengereza inawezakuwa na tafsiri nzuri kidogo...yeyote atakae muona kaini sio lazima awe mtu hata mnyama wa porini

Kwasababu we ni hodari wa kujibia watu sasa tuanzie hapa

Na tumfanye mtu kwa mfano wetu....
Sasa hapo Mungu anamwambia nani??? Na alikuwa na nani????
Kabla hatujasonga mbele zaidi napenda kujua kuwa unywaji wa pombe ni dhambi au sio dhambi???
Hayo ya laana naona umeenda mbali sana ambako wala hakunihusu.... Twende hatua kwa hatua ili na wengine wajifunze.
Asante in advance.
 
Acha kuitetea. Eleza kizazi cha Kaini kiliendeleaje

Punguza ukali wa maneno. Hawachelewi kuingia mitini

Hiyo nchi ya Nodi watu wake waliumbwa na nani? Mr Mushi92

Tukiachana na mambo ambayo hayakuandikwa kwenye bibilia ila tukumbuke kwamba watoto wakike hawakuhesabiwa katika bibilia hivyo basi kuna uwezekano mkubwa kwamba adam na hawa walikuwa pia na watoto wa kike.

Mungu aliumba wayahudi wengine walishakuwepo kwa mabilioni ya miaka.

Eh! Hao wengine waliumbwa na nani

Yes mungu ni mmoja na hana mshirika ila wapo malaika anaposema"huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya"alikuwa anawaambia malaika, hata pale nyumban kwako yupo baba, mam na watoto ila baba nafasi yake ni ya pekee haina ushirika

kwa ufupi. Biblia ni kitabu cha hadithi kama hadithi zingine kama Lord of the Rings, Harry Potter, na kadhalika tofauti kubwa ni kuwa biblia ilitumika kama silaha ya kuwatawalia watu. Binadamu tuna ualisia wa kuogopa vitu tusivyovitambua kwa hiyo watu wachache wenye maarifa wakatumia hilo kuwatawala wenzao.

Na kuna maswali mengine kama haya.
Kama yesu alikuwa na nia njema nasi na alikuwa na uwezo wa kuponya upofu kwanini asiondoe upofu.
Kama Mungu yupo na yeye ndo yote ya yote kulikuwa na haja gani ya Yesu kuteswa ili tukombolewe.
na mengine mengi yapo.
 
Kwasababu we ni hodari wa kujibia watu sasa tuanzie hapa

Na tumfanye mtu kwa mfano wetu....
Sasa hapo Mungu anamwambia nani??? Na alikuwa na nani????
Kabla hatujasonga mbele zaidi napenda kujua kuwa unywaji wa pombe ni dhambi au sio dhambi???
Hayo ya laana naona umeenda mbali sana ambako wala hakunihusu.... Twende hatua kwa hatua ili na wengine wajifunze.
Asante in advance.
mungu,malaika ni mfumo wa kihoro...ambayo haifi anaposema tufanye mtu kwa mfano wetu anawambia malaika,huyo awe kwenye mfumo wa roho,sis binadamu tumegawanyika katika sehem mbili kuna mwili na roho,mwili ndio unaozikwa ila roho haifi ila mbuzi yeye ana mwili wa nyama akifa mbuzi ndio basi,binadamu tunaishi sehemu mbili kwa wakati mmoja tunaishi kwenye ulimwengu wa roho na ulimwengu huu wa dunia,naona naenda mbali ila cha msingi ni kwamba binadamu tumeumbwa kwenye mfumo ule wa malaika na mungu...wa roho isiyokufa.
 
kwa ufupi. Biblia ni kitabu cha hadithi kama hadithi zingine kama Lord of the Rings, Harry Potter, na kadhalika tofauti kubwa ni kuwa biblia ilitumika kama silaha ya kuwatawalia watu. Binadamu tuna ualisia wa kuogopa vitu tusivyovitambua kwa hiyo watu wachache wenye maarifa wakatumia hilo kuwatawala wenzao.

Na kuna maswali mengine kama haya.
Kama yesu alikuwa na nia njema nasi na alikuwa na uwezo wa kuponya upofu kwanini asiondoe upofu.
Kama Mungu yupo na yeye ndo yote ya yote kulikuwa na haja gani ya Yesu kuteswa ili tukombolewe.
na mengine mengi yapo.

Huko kote nitampitisha anijibu vizuri. Huwezi kumtesa mwanao atekeleze kitu fulani wakati uwezo wa kukiamrisha na kikatekelezeka unao.
 
Huko kote nitampitisha anijibu vizuri. Huwezi kumtesa mwanao atekeleze kitu fulani wakati uwezo hata wa kukiamrisha na kikatekelezeka unao.
kwenye kanuni za kimungu sadaka ni muhimu ili jambo lifanyike na hata kwa shetani pia lazima utoe sadaka ili upate uchokitaka, ndio maana mungu aliamua kumtoa yesu kristo kwa ajili yetu kama ambavyo hata yeye anaagiza utoaji wa sadaka kwetu,lakini pia hapo ndipo imani ya kikiristo ilipojengwa kwenye kufa na kufufuka kwa yesu
 
Mungu anamtolea nani sadaka? Maana kwa majibu wa uwezo wake, hahitaji chochote ili awe hai. Pia kwenye mipango yake hahitaji chochote ili aitekeleze. Tukubali kwamba pasipo sadaka mungu hawezi sio?
 
Back
Top Bottom