MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Nimekuwa nikisikia minong'ono ya chini chini ambayo sasa imeanza kupazwa sauti na wagombea wa CCM kuwa ahadi za mgombea urais wa Chadema, Dr W Slaa, ni za uongo na hazitekelezeki. Kuna watu ambao ninawafahamu kuwa hawaipendi CCM lakini sasa wanaanza kuwa na mashaka na ahadi za Chadema kuwa kikingia madarakani kitatoa huduma za elimu na afya bure na pia kuwa kila kitu kitafanyiwa kazi ndani ya siku 100.
Ninashauri Chadema waanze kujibu haya maswali kwa kutoa vielelezo vya namna ambavyo wataweza kutoa elimu na afya bure, nawashauri watoe takwimu za idadi ya wanafunzi katika kila ngazi na gharama za kumsomesh mwanafunzi mmoja au kundi la wanafunzi 100 na waonyeshe ni namna gani watapata mapato ya kugharimia huduma hizi, kwa kusema tu jumla jumla kuwa kuna fedha inapotea kwenye misamaha ya kodi bila kutoa vielelezo watapoteza kura nyingi za watu ambao wangewapigia kama watapewa maelezo na vielelezo vinavyojitosheleza. Ikiwezekana waanze sasa kutupa hata mfano budget ya serikali yao kwa muhtasari.
Hii itawaziba midomo akina Kinana, Makamba, Kikwete na wengine kusema kuwa haya wanayoahidi Chadema na Slaa ni uongo. Pia itatoa fursa kwa watu makini kupima na kuona kuwa inawezekana watoto wao wakapata huduma bure na bora wakiwachagua Chadema. Nadhani kila mtu anataka kupata huduma bora na kwa gharama nafuu.
Kingine cha msingi ambacho nawashauri waanze kufanya ni kutoa maelezo ya namna ambavyo watatekeleza hayo wanayoyaahidi, nadhani hakuna Mtanzania leo hii ambaye hajui kuwa CCM ni genge la wahuni wasipoteze muda wao uliobaki kuelezea haya wajikite kwenye namna watakavyoshugulikia ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu na vipeperushi. Naamini hii itawasaidia zaidi kuliko kupoteza muda wao kulipua makombora ya namna ambavyo Kikwete anaendesha nchi hii kama shirika la ukoo wao, tunajua na tunaelewa yote haya. Tunaomba tupatiwe majibu ya namna tutakavyotoka hapa
Nadhani bado hujawaelewa CHADEMA na itakuchukua muda mrefu kuwaelewa. Hili linatokana na ufinyu wa elimu yako, kwani inaonekana dhahiri kwamba HUKUFUNDISHWA kufanya tathmini (analysis) kwa mambo ya kiuchumi na kisiasa. Ahadi za CHADEMA zinatekelezeka. Ngoja nikupe mifano miwili tu!
1) Bunge la Jamhuri lililopita, lilipitisha bajeti ambayo ni dhahiri kwamba haikidhi mahitaji ya wananchi kutokana na ufinyu wake na upendeleo kwa matumizi yasiyo na lazima. Hili linatokana na kwamba Bunge hilo lilikuwa ni la chama kimoja, CCM, ambacho kilikuwa na idadi kubwa ya wabunge, na wabunge wachache wa upande wa upinzani. Hivyo, CHADEMA wasingeweza kufanya maamuzi yoyote yale kwa manufaa ya taifa.
2) Iwapo Dr. Slaa atachaguliwa kuwa Rais, ataweza kuunda Serikali yenye wizara chache, hivyo kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, na kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya mawaziri na manaibu waziri. Chukua idadi ya mawaziri na manaibu waziri waliopo sasa, weka (kwa mfano) thamani ya wastani wa Toyota LandCruiser VX (mpya) kuwa TZS Milioni 200, kisha fanya hesabu. Kama idadi inazidi mawaziri na manaibu waziri 40, hesabu za haraka ni TZS Mil. 200 x 40 ambapo unapata jumla ya TZS 8,000,000,000, yaani, TZS Bilioni 8. Slaa ameahidi kuunda Serikali yenye mawaziri na manaibu waziri 20 tu! Kwa hiyo, ukiondoa nusu ya hao mawaziri na manaibu utapata jumla ya TZS Bilioni 4 kwa magari yao tu, hivyo tayari atakuwa ameokoa TZS Bilioni 4. Lakini hili litafanyika ENDAPO kiwango cha magari ya mawaziri na manaibu waziri kitakuwa ni Toyota LandCruiser VX, ambayo kwa kweli ni gari kubwa na ya anasa! Je, haiwezekani mawaziri na manaibu hawa kununuliwa, kwa mfano, gari zuri kama vile Toyota Rush (ambayo ina engine ndogo ya 1,500 CC na pia ni gari zuri sana), au magari mengine kama vile Toyota RAV4 model mpya? Lazima tuweke vipaumbele kwenye matumizi sahihi ya fedha za walipakodi.
Hii ni mifano miwili tu, ya mambo ambayo YANATEKELEZEKA kwa muda wa siku 100. Bunge la kwanza la Serikali mpya litakaa kikao chake Dodoma wakati huo, na sheria za kurekebisha bajeti (baada ya kuundwa kwa baraza la mawaziri na manaibu - iwapo italazimika kuwaweka - wachache, na kuwaapisha) ili tuwe na bajeti yenye TIJA, si HASARA na UFISADI!
Tuweke kipaumbele kwenye elimu, afya, miundombinu (kwa manufaa ya Watanzania wengi). Kuwasomesha watoto wetu bure, kuanzia chekechea hadi Form VI INAWEZEKANA. Tunakusanya kodi nyingi sana (trilioni kadhaa kwa mwezi!), lakini faida yake haionekani.
Jana nimeona picha ya mtu akipelekwa hospitali, hoi, kwa machela yaliyoundwa kwenye baiskeli! Halafu bado wanadai ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI? Za kuifilisi nchi?
Msinitie kichefuchefu asubuhi yote hii! Tena leo Ijumaa!
-> Mwana wa Haki