Masuala Yenye Utata - 1: Je; Kutoa Mimba Kuhalalishwe?

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu. Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.

Nini maana ya mimba kutoka (abortion)

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno ‘abortion‘ kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na ‘miscarriage‘ kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

Tanzania ni Nchi ambayo haijaridhia kuwa na Sheria Ya Kutoa Mimba na hivyo Kutoa Mimba ni kosa. Hata hivyo tumeshuhudia vitendo vya abortion vikizidi kuongezeka kwa wanawake wakiwemo wanafunzi wa shule au vyuo na wasio wanafunzi. Hii inaleta changamoto yenye utata juu ya nini hasa ni sahihi katika suala zima la utoaji mimba.

Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)

Utoaji mimba kinyume cha sheria ni usitishwaji wa maisha ya mimba au kutolewa kwa kiumbe kinyume na sheria za nchi husika zinavyoagiza. Katika mazingira kama haya, sababu dhahiri za kitaalamu hukosekana isipokuwa wahusika hutenda kulingana na sababu zao binafsi zikiwemo za kutoitaka mimba au kama ni muhusika ni mwanafunzi huogopa kufukuzwa shule.

Utoaji mimba kisheria kwa sababu za kitabibu (therapeutic abortion)

Utoaji mimba ulioidhinishwa kitabibu ni usitishwaji wa mimba kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama. Usitishwaji huu ni hufanywa kitaalamu na daktari. Sababu zinazoweza kufanya mimba ikasitishwa ni pamoja na:

- iwapo kiumbe kina mapungufu mengi ya kimaumbile (fetal anomally) ambayo yatamletea mtoto atakayezaliwa matatizo na hata kusababisha kifo chake

- iwapo mama mjamzito alipata ujauzito kwa kubakwa na asingependa kuzaa, au

- iwapo mama mjamzito ana kansa , kwa mfano, kansa ya kiwanda cha mayai ya kike (ovarian cancer), kansa ya damu (leukemia) au kansa ya tezi la goita (thyroid cancer
)

Je, utoaji mimba kwa kukusudia uruhusiwe?

Kama ndiyo uruhusiwe ni kwa nini?

Na kama hapana usiruhusiwe ni kwa nini?

Naomba kuwakilisha.
 
Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu. Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.

Nini maana ya mimba kutoka (abortion)

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno abortion kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na miscarriage kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

Tanzania ni Nchi ambayo haijaridhia kuwa na Sheria Ya Kutoa Mimba na hivyo Kutoa Mimba ni kosa. Hata hivyo tumeshuhudia vitendo vya abortion vikizidi kuongezeka kwa wanawake wakiwemo wanafunzi wa shule au vyuo na wasio wanafunzi. Hii inaleta changamoto yenye utata juu ya nini hasa ni sahihi katika suala zima la utoaji mimba.

Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)

Utoaji mimba kinyume cha sheria ni usitishwaji wa maisha ya mimba au kutolewa kwa kiumbe kinyume na sheria za nchi husika zinavyoagiza. Katika mazingira kama haya, sababu dhahiri za kitaalamu hukosekana isipokuwa wahusika hutenda kulingana na sababu zao binafsi zikiwemo za kutoitaka mimba au kama ni muhusika ni mwanafunzi huogopa kufukuzwa shule.

Utoaji mimba kisheria kwa sababu za kitabibu (therapeutic abortion)

Utoaji mimba ulioidhinishwa kitabibu ni usitishwaji wa mimba kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama. Usitishwaji huu ni hufanywa kitaalamu na daktari. Sababu zinazoweza kufanya mimba ikasitishwa ni pamoja na:

- iwapo kiumbe kina mapungufu mengi ya kimaumbile (fetal anomally) ambayo yatamletea mtoto atakayezaliwa matatizo na hata kusababisha kifo chake

- iwapo mama mjamzito alipata ujauzito kwa kubakwa na asingependa kuzaa, au

- iwapo mama mjamzito ana kansa , kwa mfano, kansa ya kiwanda cha mayai ya kike (ovarian cancer), kansa ya damu (leukemia) au kansa ya tezi la goita (thyroid cancer
)

Je, utoaji mimba kwa kukusudia uruhusiwe?

Kama ndiyo uruhusiwe ni kwa nini?

Na kama hapana usiruhusiwe ni kwa nini?

Naomba kuwakilisha.

uUruhusiwe ili tunaposema tuna uhuru iwe ni uhuru wa kweli wa kujiamulia mambo yanayokuhusu bila kuingilia na mtu. Najua kuna idadi kubwa ya watu wamekwishakutoa mimba katika hali ya kujificha. Binafsi sioni tatizo mtu anapoamua kutoa mimba nafikiri kwa hali dunia ilipofika ni vizuri ikahalishwa Na tukajaribu kuwaelimisha watu kama wasichana wadogo na ambao wako mashuleni juu ya kuwa na maadili na jinsi ya kujikinga na mimba kama vile tunavyotumia gharama kubwa kutoa elimu ya ukimwi
 
uruhusiwe ili kkupunguza watoto wasiotarajiwa na vifo vya kijingajinga:coffee:
 
USIRUHUSIWE!!!
Kutoa mimba ni sawa na kuua. Unaua kiumbe kilichopo tumboni. Kuua ni dhambi.
Labda tu kama mimba inahatarisha maisha ya mzazi, ndio iruhusiwe kwa shingo upande.
 
Haijahalalishwa tu spidi ipo juu. Je ikihalalishwa sijui itakuwaje.
Au ndio itakuwa mambo ya kuacha tunayoruhusiwa, kufanya tunayokatazwa.
 
images

hebu fikirieni......
 
sipendi tabia hii ya ukatili wa kutoa mimba, hiyo ni zaidi ya ufisadi wa DOWANS
 
Kisa cha kuua mtoto asiye na hatia!?Kama mtu hataki mimba either ajikinge nayo au aepuke kabisa tendo linalopelekea kupata mimba!Tamaa yako isiwe kifo cha mwingine!Fikiria wewe na mimi tungetolewa leo hii tungekuwepo hapa?Ahhh nachukia watu wanaopenda kutoa mimba...maana wengine hata zaidi ya mara tatu wanatoa tu bila wasiwasi!
 
Lizzy; kwa wale watoto mfano wa Primary au Secondari ambao walidanganywa na Wanaume au Walibakwa na kupata Mimba lakini hawana namna na uwezo wa kulea Mimba wala Watoto wafanye nini?
 
Hapo exception inakuwepo!Ila haihalalishi!Namjua msichana alibakwa akiwa na miaka 13 hakutoa mimba japo maisha yalikua magumu!Sasa hivi ana 20 na kitu..ameolewa na amepata mwingine!Huwezi amini anavyompenda huyo mtoto wake wa kwanza,na anashukuru Mungu kila siku hakutoa hiyo mimba!
 
KUhalalisha utoaji mimba itakuwa kosa kubwa sana.NAdhani wale madaktari wanaotoa mimba wapigwe fine kama tunataka kuokoa vichanga.MAdaktari wakipigwa faini na kunyang'anywa leseni zao watu wengi watajikinga kwani watakosa pakwenda kuzitoa.

Waruhusiwe kutoa wale ambao wamebakwa,kwani hawa hawakujitakia lazima tuwafikirie pia.
 
Lizzy; kwa wale watoto mfano wa Primary au Secondari ambao walidanganywa na Wanaume au Walibakwa na kupata Mimba lakini hawana namna na uwezo wa kulea Mimba wala Watoto wafanye nini?

Mambo yakizidi kuna vituo vya kulelea yatima au watoto wenye mazingira magumu. Wasiuawe wakiwa tumboni.
 
Kutoa mimba kwa makusudi wakati hakuna tishio la afya kwa mama ni jambo linalowafanya binadamu kuwa chini ya wanyama kiustaarabu.
 
Back
Top Bottom