Unachukuliaje masuala ya Kisiasa katika maisha yako?

  • A) Nafuatilia masuala ya kisiasa sababu najua umuhimu wake

  • B) Siasa haina umuhimu wowote kwenye maisha yangu, sifuatilii kabisa!

Results are only viewable after voting.

JF Toons

Digital Art by JF
Feb 19, 2024
32
66
Siasa.PNG

Maamuzi yote yanayohusu nchi hufanyika chini ya mwamvuli wa siasa, ni muhimu kwa kila raia kujua kinachoendelea ili kupata taarifa sahihi zitakazomuwezesha kufanya maamuzi sahihi pale anapochagua kiongozi.

Masuala ya kisiasa yana nafasi gani katika maisha yako?
 
Kwa bahati mbaya au nzuri kwa nchi yetu maamuzi ni yao ila kura ni zetu.
Sijawahi fanya siasa na sitokaa nifanye siasa. Sipo simba sipo Yanga ila ni Yanga.
 
Kwa hapa BONGO wengi wamafuatilia siasa kwa sababu ya kuboost self esteem, na hii hua inatokea automatic tu bila mtu kujua maana kuna kuwa na pande mbili CCM vs CHADEMA ko hapa utapata mashabiki wa pande mbili, hawa watu wao hata kama kiongozi wa upande wao akifanya jambo la hovyo wao humtetea kwa nguvu zote rejea ROWASA akiwa CCM na akiwa CHADEMA uone mashabiki wapande zote mbili walivyokua wakivutana. SIASA ZA TANZANIA ZITAPATA MVUTO TENA SIKU SIMBA NA YANGA zikipoteza mvuto.
 
Siasa ni maisha, kuanzia usajili wa vizazi Hadi usajili wa vifo, and EVERYTHING in BETWEEN Birth and Death. Kila kitu ni siasa 100%.
 
Changamoto kwetu ni kuwa hata ukifuatilia siasa utaona hakuna kinachobadilika 😂 so watu huamua tu kudeal na mambo yao binafsi, wao siasa haitawasumbua mpaka waguswe kweli, eg suala la umeme au maji ndio utaona watu wanamind, after that watu wanaendelea na mambo yao mengine
 
Ukweli ni kwamba siasa inagusa kila kitu, kila kitu ambacho hakiendi sawa ni pesa yako ndio inahujumiwa... ila mpaka mtu atoke damu kabisa ndio anaona hapa kweli nimeguswa?!
 
Ukweli ni kwamba siasa inagusa kila kitu, kila kitu ambacho hakiendi sawa ni pesa yako ndio inahujumiwa... ila mpaka mtu atoke damu kabisa ndio anaona hapa kweli nimeguswa?!
Unachosema upo sahihi, lakin sasa mambo yanakuwa mengi kwenye hii nchi, majukumu ni mengi pia kwa raia,

Ukisema utumie muda mwingi kupambania siasa, wanasiasa wakishapata keki hawakukumbuki na wanakugeuka huku niny hamjapata Chochote,
Yanaweza tangazwa maandamano, mkaacha kazi mkaenda huko, mwisho viongozi wakaitwa, wakapewa bahasha, wakasema tusubiri mpaka mwakani,

Unapambana mtu awe mbunge kwa sababu anaonyesha ana potential, akifika kwenye ubunge anakuwa kama wale wale tu 😂😂 na hii ni kwa both, CCM na Upinzani,

Sasa hii trend watu wamekuja kuona kuwa hii nchi siasa ni ajira za watu, kujipeleka kwenye siasa ni kwenda kuwa mtaji wa watu, thus why wanakimbia
 
Siasa ndio inaongoza maisha yetu ila ukiwa mfia-siasa bc hilo ni tatizo
 
Unachosema upo sahihi, lakin sasa mambo yanakuwa mengi kwenye hii nchi, majukumu ni mengi pia kwa raia,

Ukisema utumie muda mwingi kupambania siasa, wanasiasa wakishapata keki hawakukumbuki na wanakugeuka huku niny hamjapata Chochote,
Yanaweza tangazwa maandamano, mkaacha kazi mkaenda huko, mwisho viongozi wakaitwa, wakapewa bahasha, wakasema tusubiri mpaka mwakani,

Unapambana mtu awe mbunge kwa sababu anaonyesha ana potential, akifika kwenye ubunge anakuwa kama wale wale tu 😂😂 na hii ni kwa both, CCM na Upinzani,

Sasa hii trend watu wamekuja kuona kuwa hii nchi siasa ni ajira za watu, kujipeleka kwenye siasa ni kwenda kuwa mtaji wa watu, thus why wanakimbia
Hii ndio nafasi ya sisi tunaotengeneza hayo material yanayoenda kutugeuka kuungana, anazingua imetoka hiyo, hapati nafasi nyingine katika maisha yake. Lakini sasa tunakosa huo umoja, tunagawanyika. Hapa unakubali kwamba sisi wenyewe ndio tatizo?
 
Back
Top Bottom