Diehard
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 467
- 347
Nikiwa katika kipindi hiki cha Noeli kama wengine wasemavbyo nilibahatika kupita katika jiji la Mbeya, nilivutiwa kutembelea jiji hili kwani niliwahi kuishi huko miaka ya 80.
Kubwa lililonitatiza ni kuhusiana na masoko mawili makubwa yaliyoungua.
Soko la mwanjelwa niliwahi kujipatia mitumba enzi hizo liliungua Desema 2006 na soko kuu la uhindini hapa nilikuwa napata nyama choma uwanja wa fisi liliungua Desemba 2010.
Cha ajabu masoko yoyte baada ya kuungua serikali ya mkoa na ile ya halmashauri ya jiji zimetoa amri na marufuku ya kuwazuia wafanyabiashara kukarabati au kuendelea na biashara katika maeneo husika.
Jambo hili limewaacha wafanyabiashara ndogondogo pamoja na wale wafanyabiashara kubwa wasijue pa kwenda kwani maeneo mbadala hayajatengwa kwa wao kufanyia biashara.
Ikumbukwe hapajakuwa na taarifa rasmi ya nini vyanzo vya moto huo.
Swali ni je ni serikali ndio chanzo cha moto huo maana inaonyesha kila moto ukitokea polisi huwepo standby na kuwaibia walengwa ipasavyo, na pia yaonyesha kila moto ukiunguzwa ndio matumizi mbadala ya masoko hujitokeza.
Wito wangu kwa wanahabari za kichunguzi kujaibu kutuchunguzia sakata hili.