Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Vita baina ya Israel na Vikundi vya Kihafidhina vinavyotafsiriwa na watu wa Magharibi kama vya kighaidi vya HAMAS, HEZBOLLAH na HOUTHI vinaelekea kusambaa na kuamsha INTIFADA YA DUNIA ambayo tayari imegawanyika kufuatia vita hiyo.
Vita hivi vilianza kama vya kujihami baina ya mahasimu wawili IDF na HAMAS na sasa vimebadilika kuwa vita vya maslahi ambavyo vimevutia mataifa makubwa na kambi 2 za kujihami duniani kutumia vita hivyo kama fursa.
Duniani leo vita ni biashara na fursa nyingine lukuki, kama hakuna hivyo viwili hakuna vita inaweza kupiganwa.
Wakati hayo yakiendelea ni wazi kuwa IDF inatanua wigo wa medani kujumuisha Lebanon (Hezbollah), Yemen (Houthi) na Syria inajipanga kwa sababu Hezbollah wakielemewa watakimbilia Syria na lazima IDF itawafuata huko hivyo Syria italazimika kukabiliana na IDF.
IDF ikiwaelemea Hezbollah wataokimbilia Syria ni wazi kuwa Hezbollah hao watahamia Jordan hii pia itahusu wapiganaji wa Ukingo wa Magharibi, Jordan italazimika kuingia kwenye medani na IDF. Mduara huo utafika Yemen kukabili HOUTHI.
Dunia inapaswa kujitafakari upya kwa faida, mustakabali na hatma ya vizazi vijavyo.