Mashirika ya matangazo ndio yanaua vyombo vya habari

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Tokea kuibuka kwa Radio nyingi binafsi kufunguliwa mlango mwanzoni mwa miaka ya 90s. Kukaibuka na kampuni za kijanja za kutengeneza na kusimamia pamoja na kusambaza matangazo ya biashara nazo zikaibuka.

Na upigaji ukawa mkubwa. Shirika ama Wizara zikaingia mkumbo wa kununua matangazo kwenye vyombo vya habari kupitia hawa mawakala, shirika linalipa wakala ambaye nae anakata commision yake ndipo nae analipa chombo cha habari.

Hivi karibuni ukifuatilia ukapa katika kuendesha vyombo vya habari umeshika hatamu na kufanya baadhi ya mashirika ama kampuni za habari kufunga vituo vyao. Lakini ukiangalia ni hawa mawakala ndio chanzo cha kushindwa kuzilipa kwa muda vyombo vya habari.

Karibu vyombo vingi vya habari vinadai mamilioni ya pesa kwenye haya makampuni ya uwakala wa matangazo. Ni muda sasa kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuja na matamko ya kulipwa kabla ya huduma kuliko hili la sasa la kutegemea malipo baada ya siku 45 mara baada ya kupeleka Ankara ya malipo.

Bila kuwepo na mabadiliko hali ya njaa katika vyombo vya habari kamwe haiwezi kuisha.
 
kwani si kunakuwa na makubaliano (mkataba) yenye kuainisha namna malipo yatakavyofanyika na hatua za kuchukua ikiwa kuna ucheleweshaji ulio nje ya muda uliopangwa?
 
Back
Top Bottom