ELIASANTE
JF-Expert Member
- Jun 6, 2014
- 330
- 67
Habari zenu wanajamvini,
Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.
Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.
ELIMU JUU YA UCHAGUZI WA MASHINE BORA YA KUTOTOLESHEA MAYAI YA KUKU(INCUBATOR).
Ni watu wengi wanaohitaji kufuga kuku na kuwa na kipato zaidi kwa kumiliki mashine zao wenyewe za kutotolesha mayai ya kuku. Lakini baadhi yao hukatishwa tamaa na baadhi ya watu ambao hawajui kuwapa ushauri mzuri juu ya uchaguzi wa mashine na jinsi ya kuitumia.
Kwa kawaida tunasema kama mashine ina trei tano za mayai;kila trei imetoa kifaranga kimoja;hilo ni kosa la mtumiaji wa mashine;ila mashine haina kasoro.
Mayai yanayowekwa ktk mashine yanatakiwa yasiwe yamekaa zaidi ya siku saba tangu kutagwa;yawe safi;yasitikiswe wala kunyanyuliwa kwa vidole wakati wa kugeuza.Joto la mashine lisishuke nyuzi joto 38'c.geuza mayai kila baada ya masaa nane;hakikisha kuna maji safi ktk mashine na hewa safi.
Geuza mayai mpaka siku ya 18;basi.
Ukifuata masharti hayo na mengine; utaifurahia mashine yako.
Wasiliana nasi:
Dsm 0784413039;Njombe 0787150720;Ruvuma 0784480931;KWA INCUBATOR BORA ZENYE UHAKIKA.