Mashine za EFD sasa kutolewa bure na Serikali!

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Wanajamvi,

Kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara nchini waliokuwa wanalalamikia Serikali kwamba mashine za EFD's zinauzwa ghali, kwa sasa tatizo hilo limetauliwa kwani zitatolewa bure na Serikali.

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango, ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba mashine hizo za EFD hazitauzwa, wafanyabiashara nchini watapewa vifaa hivyo bure.

Nadhani sasa Serikali imeamua kujielekeza kuondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vinalalamikiwa ili kufanikisha zoezi la kukusanya mapato.
 
Tatizo sio mashine,, tatizo ni kodi inakatwa mpaka kwenye mtaji badala ya faida,,,magufuli badala ya kudeal na tatizo kubwa kama hili,,,anahangaika na vi small issues visivyokuwa na tija kwa taifa
 
Hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya habari ya channel ten iliyoripoti taarifa kutoka TRA
 
Na hao waliokwisha nunua warudishiwe mishiko yao
Na rais wa zamani arudishwe madarakani. ndo hayo watu wanaanza kusema kuhusu serikali iliyopita. tutafika kwa hayo yaliyotendeka huko?
ngoja afanye kuanzia anapoanzia. tumpe suport tu.
 
Hizi mashine zilileta mtafaruku mkubwa na kusababaisha ghasia kiasi baadhi ya maeneo.

Safi sana, matunda ya Magufuli hayo
 
]sasa walionunua watarejeshewa pesa yao?##Ikiwa hivyo na raid aliepita arudi madarkan kama haliwezekani lililopita limepita tugange lililopo
 
Safiiiii safiiiiiiii safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....

So, now wafanyabiashara watakuwa wanafurahi kidogo.... lilolobaki ni kuangalia kodi, je ni rafiki kwa mfanyabiashara.....? Usikute mtu aba turnover ya 20 mil kwa mwaka... alafu kodi ni 10 mil.. hapo utamuua na KUMZIKA KABISAAA MFANYABIASHARA....

EFD.. hii ni hatua kubwa sana kwa Magufuli kafanya vema... tumpongeze... kwenye ukweli tumpe CREDIT JAMANI...!!

👏👏👏👏👏👏
 
Itasaidia kukusanya kodi na kupunguza malalamiko, maana wafanyabiashara walikuwa wakizilalamikia zinauzwa kwa bei kubwa. Kazi ya kukusanya kodi itafanyika bila malalamiko. Tanzania ijengwe kwa kodi zetu pamoja na rasirimali zetu, kwa Dunia ya sasa hakuna msaada wa bure.
 
Will TRA make a refund for my old machine?
Magufuli anavamia syndicate kwa pupa. Matatizo ya uchumi wetu SI mashine hizi Ni watu kama Kinana, Ritz1, Ben etc
Ubavu Hana hata WA kuwaambia tra watumie network ya ttcl....
 
Hizi mashine zilileta mtafaruku mkubwa na kusababaisha ghasia kiasi baadhi ya maeneo.

Safi sana, matunda ya Magufuli hayo
 
Back
Top Bottom