Mashindano ya viroba valuu yachukua uhai wa mtu

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
2,151
1,417
Pombe kali hasa hizi za bei nafuu zimekuwa na tatizo kwa vijana.
Hivi karibuni kijana mmoja amepoteza maisha kwa kunywa pombe aina ya valuu kupita kiasi. Alifikisha idadi ya viroba 18, lakini kilichofuatia ni mauti.

Serikali ilitazame hili jambo hasa kwa bidhaa hizi zinazoathiri nguvu kazi ya taifa.
Source; Rafiki aliyepo Ruvuma.
 
Maskini ameshindana na nyongo kiruuu.. Valuu si ya kunywa ujakula ohooo unaweza anza kuonana na marehebu ukiwa hai... Ile kitu sijui inafanyaga nini mapigo ya moyo .. Alale kwa amani tu aisee
 
RIP Jamaa....

Valuu ni habari nyingine kwa walevi....huku mtaani kwetu ,kulikuwa ubishi kati ya vijana wa bodaboda..kuhusiana na nani anaweza kunywa kofii na Chaja nyingi....

mwisho wa ubishi haukuwa mzuri....

mshindi wa kwanza alianguka ghafla na kufariki hapo hapo...wa pili alifarki hospitalini muda mchache baada ya kufikishwa hapo akiwa hajitambui...

Hii ni habari ya kweli .....Viroba hivi ni hatari kwa vijana wenzetu...hasa bodaboda....

tusipokuwa makini...tutaendelea kupoteza nguvukazi kwa vidang'a .....
 
Kuna marehemu wengine mtu unatamani uwafufue uwatandike hata makofi mawili matatu
 
Jamaa alijitakia... please please nakuomba GODFATHER mfanye upendavyo huyo raia... AMEN
 
R.I.P mzee wa viroba nakumbuka rafiki yangu alishawahi kulazwa kisa utumbo umejisokota kisa unywaji wa viroba kupita kiasi bila kula chakula
 
Kiroba,gongo(chang'aa) ni hatari kwa afya yako,kiburudisho pekee,ni bange tu,ambayo huweza kukuongezea utulivu wa mawazo,na ubunifu na udadisi katika ubongo wako
 
Pombe kali hasa hizi za bei nafuu zimekuwa na tatizo kwa vijana.
Hivi karibuni kijana mmoja amepoteza maisha kwa kunywa pombe aina ya valuu kupita kiasi. Alifikisha idadi ya viroba 18, lakini kilichofuatia ni mauti.

Serikali ilitazame hili jambo hasa kwa bidhaa hizi zinazoathiri nguvu kazi ya taifa.
Source; Rafiki aliyepo Ruvuma.

Ni kheri kuruhusu bhangi ila sio hii Kitu ya kiroba sijui gunia sijui nini sijui:mad:
 
Back
Top Bottom