Elections 2010 Mashabiki wa Kikwete Tuambieni!!!

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Ni dhahiri sasa kwamba serikali ya awamu ya nne inatumia nguvu mno kutaka kutuaminisha imedeliver au kwa lugha nyingine imeleta mafanikio. Cha ajabu ni kwamba what is on the ground is completely different. Na mengi yanayosemwa ni mafanikio ya serikali ya awamu ya nne ni majukumu ya kawaida ya serikali. Mfano uendelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara, kuandikisha watoto kujiunga na elimu ya msingi ofcourse hata idadi ya watu imeongezeka pia, kuongeza idadi ya wafungwa etc.


Kwa kifupi alichofanya JK na serikali yake kingeweza kufanywa almost na mtu yeyote yule ambaye angechaguliwa kuwa raisi in 2005. Na probably the net effect is close to zero or even negative.


Sasa basi kwa kifupi na bila kuunga-unga kama inavyofanyika sasa tunaomba mashabiki wa Kikwete mtutajie mafanikio ya JK, objectively,one sentence na pia specific. Things that will be in history kwamba vililetwa na serikali ya awamu ya nne. Or else some radical changes that identify the character of Kikwete as a leader.

Nitatoa mifano ya awamu zilizopita kwa hiyo na nyie mtupe ya awamu ya nne.

AWAMU ZA NYERERE

1. Alitoa elimu na afya bure

2. Alitaifisha shule zote za dini na kuzifanya za serikali

3. Alijenga mabwawa ya umeme ya Mtera, Kidatu, Pangani.

4. Alifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa

5. Alijenga Dar es Salaam airport etc. etc.

Note: Hii ilikuwa ni awanu ya kulijenga taifa from scratch.


AWAMU ZA MWINYI

1. Aliruhusu umiliki na uendeshaji wa vyombo binafsi vya habari.

2. Alianzisha mradi wa umeme Kihansi

3. Alijenga barabara ya Kahama mpaka mpakani mwa Burundi na Rwanda

4. Aliruhusu makampuni binafsi kununua mazao ya biashara kutoka kwa wakulima.

5. Aliruhusu uchumi kuendeshwa na uchumi wa soko, pia maduka binafsi ya kubadilisha fedha. etc. etc.

AWAMU ZA MKAPA
1. Alianzisha ujenzi wa barabara za lami nyingi kuliko awamu yeyote ile tena kwa hela zetu( Dar - Mwanza, Kibiti - Lindi, Busisi - Kagera, Kupanua barabara ya Dar - MIKUMI etc. etc.

2. Alijenga daraja la Mkapa

3. Alijenga uwanja mpya wa kisasa wa michezo, of its kind in East Africa.

4. Alifuta ada ya shule za msingi

5. Alianzisha ujenzi wa daraja la urafiki kati ya Tanzania na Mozambique

Note: Mkapa pia aliendeleza ujenzi wa barabara za kipindi cha Mwinyi kama ile ya Moro -Dar, Mbeya - Kasumulu, Chalinze Segera. Lakini hatukumsikia mwaka 2000 on his re-election bid akisimamia umaliziaji wa barabara hizi kama mafanikio ya awamu ya uongozi wake.

AWAMU YA KIKWETE

1. ..........................................................................

2. ..............................................................................

3. ............................................................................

4. ..................................................................................

5.......................................................................
 
awamu ya nne
1.ongezeko la mafisadi
2.ongezeko la mfumuko wa bei
3.ongezeko la umaskini
4.ufnguzi wa barabara,madaraja aliyojenga mkapa
5.ongezeko la ada za shule,vyuo
 
Amejenga MACHINGA COMPLEX..mbona yako mengi tu...! tumeona mawaziri wakining'inizwa mahakamani....
 
AWAMU YA KIKWETE:
1. Alitoa mabilioni ya JK kwa wateule wachache wenye nazo, fedha hizo zilipotea bure na hazikufanya chochote
2. Alisafiri kuliko Rais yeyote Afrika
3. Alishindwa kuelewa dhana ya MKUKUTA iliyoanzishwa na Mkapa kwa kudai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni Maskini,
4. Amefanya Ikulu kuwa ni mali ya familia,
5. Mfumuko wa bei umepanda toka 4% hadi 12%
6. Wafanyakazi wameambiwa hata wagome miaka 8 hawataongezewa mishahara,
7. Amewasafisha mafisadi na kudai ni watu wazuri tu watashinda kesi zao,
8. Shule za Kata zinaongoza kwa kufelisha wanafunzi,
9. ...
 
6.Kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri
7.Kuwa na baraza kubwa la mawaziri kuliko vipindi vyote vilivyotangulia
8.Kuruhusu mjadala wa Mahakama ya Kadhi Bungeni
9.Kuandikisha Watoto wa shule za kata kwa wingi zaidi.
10.Kuwatisha wafanyakazi wanapodai haki zao.
11.Kuweka hadharani baada ya kufanya utafiti wa mimba za mahuleni kuwa ni kutokana na kiherehere
 
AWAMU YA KIKWETE

.Amepiga picha na Boys two men
. Ailonyesha jinsi ya Kubembea
.Alimwajiri Yahaya Husein kuwa mlinzi wake na famikia yake -
. Amejenga studio ya kurekodi muziki kama za akina Master J, Majani , nk
. Alipeleka serikali yote Ngordoto kula bata akiita ni semina elekezi
. Alisema wanafunzi wanaopata mimba ni vihere here tu.
.Alisema walioambukizwa ukimwi ni vihere here
.Alisema hataki kura za wafanyakazi wa Tanzania
 
1. ameongoza serikali mbili ndani ya miaka mitano tofauti na maraisi wengine (i)serikali ya awamu ya nne chini ya lowasa ikiwa na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania na awanu ya nne na nusu chini ya pinda ikiwa na kauli mbiu ya kilimo kwanza.
 
AWAMU YA KIKWETE:
1. Alitoa mabilioni ya JK kwa wateule wachache wenye nazo, fedha hizo zilipotea bure na hazikufanya chochote
2. Alisafiri kuliko Rais yeyote DUNIANI
3. Alishindwa kuelewa dhana ya MKUKUTA iliyoanzishwa na Mkapa kwa kudai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni Maskini,
4. Amefanya Ikulu kuwa ni mali ya familia,
5. Mfumuko wa bei umepanda toka 4% hadi 12%
6. Wafanyakazi wameambiwa hata wagome miaka 8 hawataongezewa mishahara,
7. Amewasafisha mafisadi na kudai ni watu wazuri tu watashinda kesi zao,
8. Shule za Kata zinaongoza kwa kufelisha wanafunzi,
9. ...

Nimeedit hapo kwenye bold red mkuu
 
AWAMU YA KIKWETE
1.Amejenga Chuo Kikuu Cha Dodoma
2.Barabara ya Kilwa Road
3.....

Chuop kikuu dodoma ni mradi uliobuniwa na serikali ya mkapa yeye akaja akadandia kwa kuwa alikuwa amepewa pesa haramu kwa masharti ya kibaguzi wengi wanajua hatuna haja kuongea maana ni kichefuchefu cha ze komedi
 
Ameleta uhuru wa kuongea na ndiyo maana walevi wanamwaga pumba bila ya kusumbuliwa. :becky:
 
Awamu ya nne
Watoto wengi mitaani
watoto kupata mimba
wazee na vilema kuachwa bila uanagalizi wa serikali
hasira ya wananchi kuongeza ,kuchuna ngozi,kuuza albino na kubaka watoto kwa imani za ushirikana kutokana na umaskini uliokithiri
Siri za serikali kuvuja kama kichwa cha mwendawazimu kitu kinachoonesha nchi yetu usalama wake umepungua
Askari wengi kujinyonga au kujipiga risasi kuliko kipindi chochote
vichaa wengi wameongezeka kutokana na wananchi kuwa na msongo wa akili
 
AWAMU YA KIKWETE
1.Amejenga Chuo Kikuu Cha Dodoma
2.Barabara ya Kilwa Road
3.....

Huu sasa ni utani, barabara amabayo haifiki hata km 10, nayo inahesabiwa ni mafanikio ya miaka mitano ya awamu ya nne??????
 
Back
Top Bottom