Mashabiki Mazuzu Yanga SC: Hata kama hatutakuwa Mabingwa wa CAFCC, ila bado Medali tutavaa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,197
110,662
Kwahiyo kumbe muda Wote mlioshiriki Mechi zenu za CAFCC Lengo lenu Kuu ( Mama ) lilikuwa siyo kuwa Mabingwa bali kuwa Washindi wa Pili na mvae Medali za Fedha badala ya zile za Dhahabu za Mabingwa?

GENTAMYCINE muda Wote nilikuwa simwelewi aliyekuwa Msemaji wa Simba SC ( sasa ni Mhamasishaji Mkuu ) katika Klabu ya Yanga Haji Manara pale aliposema ( tena kwa Kujiamini kabisa ) kuwa Yanga SC nzima na duniani kote wenye Akili ni Wawili tu Baba yake Mzazi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Kikwete na waliobakia Wote ni Majuha ( hawana Akili ) kabisa hivyo sasa namuamini.

Sasa kama mmeshajua kuwa USM Alger FC watakuwa Mabingwa wapya wa CAFCC kwa Msimu huu wa 2022 / 2023 na nyie mtaambulia tu Medali mnazozitaka ili Kuwaringishia nazo Kishamba wana Simba SC kwanini msimwambie Mama ( Rais Samia ) asipoteze muda wake kuwapeni Ndege Kubwa na hiyo ghsrama ikasaidie Sekta zimgine katika Suala la Maendeleo?

Kisha nyie mumtume tu mwana Yanga SC Rafiki yangu Mohammed Bhiinda akawachukulie huko Algiers nchini Algeria kisha azilete Kwenu Avic Town Kigamboni mvalishane na pia muwataarifu CAF Makao Makuu huko Egypt ( Misri ) kuwa hamtoenda na mmekubali kuwa kwa kipigo cha Jana cha Goli 2 kwa 1 kwa Mkapa hamna Ubavu wa Kuwafunga USM Alger FC Kwao hata Mroge Usiku Kucha?

Hovyooooooo...!!.

Cc: Kinengunengu
 
Huu ni utumwa, aisee yanga, jamani ndege yenu, na ushindi wenu lakini kombe mwarabu, huu ni utumwa?
 
Back
Top Bottom