Marufuku ya Trump kwa nchi saba, ni funzo katika imani zetu za kidini

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Lengo la uzi huu si udini, lengo ni kujaribu kujitafakari sisi wanadamu na Imani zetu

Hii ni siku ya nne, kama sikosei, tangu Trump apige marufuku nchi saba za ambazo wengi wao ni Waislam kuingia marekani. Pia amepiga marufuku kupokelewa kwa wakimbizi kutoka nchi hizo ambazo ni Iraq, Syria, Somalia, Yemen, Libya, Sudan na Iran.

Tangu marufuku hiyo kumekuwa na maandamano na mashinikizo makubwa kutoka kwa wanasiasa na raia wa kawaida wa nchi za Magharibi, mfano Canada wamesema wale wote waliozuiwa kuingia Marekani, wanakaribishwa Canada. Bila shaka nchi za Magharibi asilimia kubwa ni wakristu, nimekuwa nikiangalia katika mitandao ya kijamii huko nchi za Magharibi, wako wengi ambao wametumia vifungu vya Biblia kumwambia Trump kuwa anachokifanya hakiendani na Ukristo.

Mimi kwangu napata funzo kubwa sana hapa, Ukristo katika nchi za Kiislam ni vigumu sana kutekelezeka, katika hizo nchi ambazo zimepigwa marufuku kuingia Marekani, na zingine za Kiislam, bila shaka ukijaribu kujenga kanisa litalipuliwa katika hatua ya msingi, pia wewe kama ni Mkatoliki ukajaribu kuonesha ishara ya msalaba ndani ya muda mfupi utafanywa mfu.

Hapa mimi napata funzo, kwamba kupitia hiki kinachoendelea sasa, bila shaka wale waislam wa itkadi kali, pamoja na chuki na kuwaita Wakristo makafiri, kulipua makanisa yao, wajue kuwa daima mbegu ya UPENDO iliyopandwa na YESU, itatawala dunia milele.
 
Mimi naamini hata wao wenyewe waislam hawapendani, Hivi kwa nini wasikimbilie Dubai, Oman, Iran au Saudi Arabia. Manake naona wanazing'ang'ania nchi za makafiri (hapo ndio mkae mkijua hamna imani yenye upendo wa hali ya juu kama ukristo).
 
Nkobe nimekuelewa sana ndugu kwa ujumla upendo walio nao wakristo ni waukweli wala si wakinafki, majina yote mabaya wameitwa wao, lakini wamesimama sawia kuwatetea wale wanaowatukana na kuwaudhi ili waishi kwa uhuru na kuilingania imaini yao.
 
Wewe uko dunia gani?Au huangalii TV?Makanisa yapo nchi nyingi tu zenye waislamu wengi,na wala hawajafanyiwa fujo wenye hayo makanisa.
 
Mimi naamini hata wao wenyewe waislam hawapendani, Hivi kwa nini wasikimbilie Dubai, Oman, Iran au Saudi Arabia. Manake naona wanazing'ang'ania nchi za makafiri (hapo ndio mkae mkijua hamna imani yenye upendo wa hali ya juu kama ukristo).
Kuwa na akili hata nchi hizo za kiarabu wazungu na wakristo pia wapo,tena wengi sana.Na ndio maana kuna International airport,katika nchi za kiarabu,zinazolingana na nchi za ulaya.
 
Back
Top Bottom