Marekani yaishutumu serikali ya Tanzania kupitisha barabara hifadhi ya taifa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Taarifa ya habari katika Television ya National Broadcasting Company (NBC) ya Marekani jana saa kumi alasiri ilitangaza kuwa Serikali ya tanzania iliopo madarakani sasa imekazania kujenga barabara ya lami kupitia hifadhi ya mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti. Hatua hiyo ni kuharibu mazingira yanayofanya wanyama pori kuvuka kwa shida na hivyo kuhatarisha wanyama hao kukimbia sehemu hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kusema ingawa baadhi ya vyama vya siasa kupinga ujenzi wa barabara hiyo kupitia hifadhi ya taifa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi zilizopita, lakini serikali haitilii maanani ushauri wa kitaalam na hivyo kuna uwezekano wa wanyama kuondoka sehemu hiyo iwapo barabara itajengwa.

Taarifa hiyo imekuja wakati kuna fununu kuwa tajiri tishio duniani yupo ndani ya mbuga hizo kuona rasilimali za tanzania zilizofichika kwa miaka mingi.
 
Back
Top Bottom