Marekani na ubeberu

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
Hizi ni zama za kugombea rasilimali chache zilizobaki hapa duniani,baada ya watu kuzidi kuongezeka sana, hususan Afrika, kufuatia UKIMWI kushindwa kuwafyeka Weusi wote kabisa.

Kuna madai kwamba Virusi vya Ukimwi vilitengenezwa katika Maabara za Kijeshi huko Marekani, chini ya usimamizi wa akina Henry Alfred Kissinger. Hili liliweke kiporo, tutalijadili baadaye.

Marekani inayojidai sana kuhimiza haki za binadamu, usawa wa kijinsia,haki za wanawake n.k ikiwa haijawahi kuongozwa na Mwanamke miaka takriban 240 tangu uhuru.

Sehemu nyingine ulimwenguni akina Yingluck Shinawatra wa Thai, wameongoza, akina Christina Kirchner huko Argentina, Ellen Johnson Sirlief na Joyce Banda hapa Afrika, akina Dilma Rousef huko Brazil, akina Christina Lagarde wanaoongoza Fuko la Fedha (IMF), Asha Rose Migiro amekuwa Naibu Katibu Mkuu UN, Michelle Bechelet amekuwa Rais Chile tangu Januari, 2006.

Wapo akina Angela Merkel, na Margaret Thatcher huko Ulaya, lakini Marekani mwanamke hajawahi kuchaguliwa kuwa Rais, na sasa wapo marais 44.

Demokrasia, husemwa kuanzia Ugiriki,lakini hata Wagiriki hawakuruhusu mwanamke kupiga kura wala kupigiwa kura, sembuse kuongoza?

Leo, demokrasia hiyo ya Kigiriki huonekana kuwa na viraka vikubwa sana kwa kuwanyima akina mama kuwa viongozi,na hata kuwakataza kupiga kura.

Ndivyo walivyofanya Taliban huko Afghanistan, wakaonekana wa ajabu sana! Kumbe, kuna namna nyingine ya ukandamizaji hata Ulaya na Marekani, lakini nani awaambie?

Wao huiona Afrika, Asia na Amerika Kusini kwamba ndiko kwenye mbinyo wa demokrasia, kumbe nyani haoni kundule!

Si bahati mbaya, ni kusudi kuikamata dunia na kuiburuza watakavyo.

Katika Ujnabii wa Biblia,katika Ufunuo wa Yohana 16:12 kumetabiriwa ‘Roho Tatu za Vyura’ ambazo ni ‘Utatu Mtakatifu’ bandia hapa duniani, zikitoka kinywani mwa Shetani na kuwalazimisha Wakuu (Marais, Mawaziri Wakuu, Wafalme n.k) kuandaa vita dhidi ya Mungu Mwenyezi.

Chura ni alama ya uchafu katika Misri ya kale, ambayo sasa tunaona jeshi likipindua demokrasia, kwa risasi za moto mkali kushinda hata zama za Saddam, Gaddafi na madikteta wenzao.

Chura alikuwa nembo ya mungu mke, Heget, aliyeaminiwa kuwa chimbuko la uhai kwa watoto wanaozaliwa-vijana.

Huu Utatu Mtakatifu(Evil Trio) wenye sura ya vyura wa Misri, unavaa umizimu,uasi wa kidini, na ile hali ya vijana kuona DHAMB I(Uasi wa sheria ya Mungu) kama si kitu kikubwa!

Watoto wa siku hizi wenye haki za Kimarekani za kutokanywa wafanyapo makosa (Haki za Watoto), haki bandia za akina mama n.k huleta uhuru dhidi ya Mungu.

Mungu angejulikana mji anaokaa vijana wangeandamana hadi mlangoni,ili kumdai ajiuzulu na afungwe jela kwa kuweka sheria (kandamizi?) za kuwanyima uhuru wa kufanya wapendavyo!

Watu kama Obama na kina David Cameroon wanajiona vijana sana wa siku hizi, hata hawaoni ushoga na usagaji kuwa ni tatizo, bali tatizo ni watu kunyimwa haki,uhuru na demokrasia!

Mila za Afrika zinaheshimu sana ndoa ya watu wa jinsia tofauti (Heterosexual couples), wanaamini Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu mwaka 4004 BC kwa sababu na maakusudi muhimu ya kuanzisha familia.

Roho Tatu za vyura zinapinga kwa dhati ndoa kuwa ya mume na mke tu, bali hata ya mume na mume au mke kwa mke,mradi wamekubaliana-huu ni Uhuru kamilifu!

Akina Obama,David Cameron,Blair na wenzao, waliwapongeza sana wanaume waliofunga ndoa na waume wenzao kwa uhuru wao wa kikatiba, na hata walilazimisha Afrika ibadili katiba ili kuruhusu ushoga na usagaji kama inajitakia mema kwa mataifa haya.

Naam, kama Afrika inataka uchumi wake ukue na kuwe na amani na usalama kisiasa, kijamii na kiuchumi. na kiroho bila shaka.

Siku hizi watoto huzaliwa kwenye chupa za maabara (test tube babies) na mwanaume aweza kubadili jinsi kwa operesheni akawa mwanamke, akaolewa akazaa!

Hii huitwa transgender, na kuna sayansi ya human cloning, sasa Mungu naye wa nini sheria zake?

Leo, Afrika wazee ni wachache,vijana wanaotazama mitandao ya twitter na face book ndiyo wengi, ikipigwa kura ya kumkataa Mungu, inafanikiwa na inazidi kufanikiwa sana.

Akina Thomas Batie waliozaliwa Hawaii mwaka 1974 wakiwa wanawake,wakiitwa Tracy Logondino, walishabadilika na kuwa baba,sasa unasemaje? Demokrasia.

Kibaya zaidi, demokrasia ya Ulaya na Marekani hulazimishwa kufuatwa na ulimwengu wote.

Ukitaka kubadili jinsi unachomwa sindano zenye hormone (testosterone injections) kama ni msichana unapata sauti nzito, nywele fupi, unawekewa uume kwa operesheni, basi unakuwa dume jike!

Unaondolewa matiti kwa operesheni (Mastectomy), ukitaka uke au uume unaondolewa basi –ndiyo uhuru huu.

Hapa Afrika, kuna NGOs nyingi za kutetea mambo haya,serikali inapopinga inaonekana ya Kiimla, isiyojali Haki za watu na vijana wanaanza kuandamana na kupinga serikali, kama huko Misri, Libya, Tunisia, Yemen n.k

Na viongozi wanaopinga sera za Ulaya wanapinduliwa na kuswekwa rumande kwamba mafisadi, wananyimwa misaada, uchumi unakuwa mbaya sana,vijana wana ‘riot’ nguvu iitwayo ya Umma inafanya kazi!

‘Nguvu ya Umma’ aghalabu ni Nguvu ya Utatu Mtakatifu (Evil Trio); nguvu hiyo husukumwa na umizimu wa kutisha-spiritualism.

Uhuru wa ngono, picha za uchi, wanawake kujiuza, ukahaba wa kutisha, ushenzi ndiyo uhuru unaopendwa mno na vijana, na uhalifu; hawa wangependa magereza yasiwepo, hata kodi hawataki kulipa, ila waishi maisha ya raha bila kujua pesa zitatoka wapi?

Kwa akili hizi za kukosekana uzalendo,zama za utandawizi,hakuna mzalendo atakayezaliwa Afrika, bali kufanyika weusi wa Magharibi (Westernization), na watu vijana wametimka vijijini kujaa mijini (Urbanization) ili iwe rahisi kuwateka kwa kampeni za wanasiasa na NGOs za Ulaya na Marekani!

Hamkani si shwari katika nchi za Kiarabu(Unrest in Arab Countries) huashiria Yemen, Misri, Libya, Syria, Irak, Oman, Mauritania, Saudia, Jordan, Tunisia n.k asiwepo wa kupinga utandawazi kwa kisingizio cha dini n.k.

Nchi ambazo hakuna migogoro kama Qatar, Kuwait, UAE, Lebanon na Bahrain ujue viongozi wake wameafiki kimya kimya ajenda za wakubwa wa dunia, na raia hawana ubishi.

Rasilimali na kila kitu kinakwenda Ulaya bila taabu, inapotokea shida vita huanza na vijana hutumika kupinga serikali na kuanzisha ghasia na machafuko nchi nzima.

Marekani siku hizi huhimiza sana uhuru na demokrasia, FREEDOM of worship, freedom of speech, rule of law, equal rights for all-ndiyo ushoga na usagaji!

Sasa ikianzishwa dini ya kusali vijana na wasichana wakiwa uchi wewe ujidai kuikataa na kuwatia mbaroni uone. Tuendako hakutakuwa na ndoa tena,bali ni ngono holela tu na kuzaa vitoto visivyo na baba na mama zao walishakwenda danguro kujiuza,basi shetani analetea NGOs fedha za kulea yatima,zinaliwa, serikali ikisema inapingwa!

Sitetei mafisadi na wauza unga wa serikalini, bali nazungumza NGOs zinazojidai kutetea wanahabari kwa mfano, zinaombwa fedha nyingi Ulaya, vinaanzishwa vijiwe vya siasa kuipinga serikali maana inabinya demokrasia (ushoga, usagaji, uchafu) waandishi wa habari wametumika kuwabeba hawa migongoni mwao, siku hizi wana fedha, wana magari ya fahari kwa wizi na utapeli, ili mradi serikali ipingwe, Wazungu walete hela.

Dunia inaandaliwa kwa vita iitwayo Armageddon (tazama Zaburi sura ya 2).

“Anti Christ” and His Western Allies, wanajiandaa kwa vita dhidi ya haki halisi na ukweli,nchi zote na watu wote hawana budi kukubali.

Siasa ni Ulaya na Marekani,uchumi wa Kimarekani, rasilimali ziende Marekani, maisha na lugha, mila na desturi vya Ulaya na Marekani, na viongozi wawe wale wanaopendwa na Ulaya na Marekani!

Nchi zetu zimebinafsishwa Marekani na Ulaya, na akina mama hawataki uafrika tena, mara ‘makalio ya Kichina’ mawigi ya Magharibi, wanakula Kimagharibi siku hizi Mwafrika halisi kama Mandela hayupo!

“Middle East” the focal point of the World damu yao itatiririka kama mto ili kuwavua akili za Kikomunisti (Ukomunisti ni ile hali ya rasilimali zote kumilikiwa na jamii,nchi na serikali ina dhibiti uchumi), na akina sisi tulielekea Usoshalisti (mfumo ambao uliipa nafasi jamii nzima kuwa wabia ama wamiliki wa rasilimali na njia kuu za uchumi kama usafiri n.k).

Akili zetu zinaondolewa kutoka ukomunisti na usoshalisti,ili tuishi kutazama kila kitu kutoka Ulaya, Marekani, tukiwadhania wajomba na ndugu, sisi tulishasahau kujitegemea-ni michongo tu, rushwa, ufisadi na ‘kupiga hela’ bila kujua zinatoka wapi?

Halafu kelele na kushabikia kila ujinga kutoka kwa wanasiasa, Ulaya, Marekani n.k mradi kimesemwa,na hakuna tafakuri tunduizi!

Kufuatia hali hii,nchi inabaki haina kitu,mali inakwenda,viongozi nao wanakuwa watumwa wa sera za Ulaya, raia wanavaa mawigi na kutamani wawe Wachina au Wazungu!

Majina kama ya akina Mandela sasa yanapigwa marufuku, unazaa motto unamwita jina la Mzungu, makalio ya Kichina, nywele za Kizungu, kuongea lugha isiyoeleweka, nguo za Masela wa Kimarekani, wabwia unga, Malaya!

Taifa gani tunajenga? Akili gani hii, yaku compromise na Mzungu (hata Mzungu wa unga) hata hatuna chetu?

Akitokea kiongozi wa kuwapinga Wazungu, anapingwa sana kwa maaandamano ya umma huku tukisema ni nguvu ya umma, anakamatwa na kuwekwa kizuizini, watu wanashangilia, misaada inamwagwa-tunacheka!

Vema tukaanza kufanya mapinduzi yakifikra ili tutambue wapi tunakwenda? Tuna viongozi sampuli gani? Raia wa akili gani hawa, jamii gani hii tunajenga sasa?

Halafu tutajua kuipinga Marekani na ubeberu wake wa kutaka kutupora tangu rasilimali hadi tamaduni, mila na kila tulichonacho!
 
Africa is a valley of dry bones. It needs some serious fixing: To save her, we need people who do not think and act like ordinary African elites.
 
Mtoa Mada ;
Unataka Marekani Rais awe Mwanamke ata kama hana vigezo ? kwani hao wanawake wa Amerika kuna siku waliwahi kusema kua wanazuiwa kushinda kua Rais wa Marekani ? kwenye malalamiko ya Hillary Clinton alisema kua Marekani amna haki ya Mwanamke kua Rais ?

Kwani wewe leo ukiamua kuolewa na mke wako unataka Serikali ya Magufuli ikukamate na kukuweka gerezani ?

Afrika tunapoambiwa kua baadhi ya sheria zetu ni kandamizi na zimepitiwa na wakati tunakua wakali lakini wakati huo huo tunawaomba msaada kutatua matatizo yaleyale yaliyoletwa na sheria kandamizi.

Kiongozi wako anaiba pesa za mradi wa kuangamiza mazalia ya Mbu wanaoeneza ugonjwa wa Malaria na pesa anazitunza humo Ulaya ; Baadae mkianza kuangamizwa na Malaria serikali ya nchi za Ulaya wanachukua pesa hizo mlizotunza wanawakopesha au kuwasaidia kutibu Malaria alafu bado mnawalaumu nchi za Ulaya.

Bado kuna wengine wanawatetea akina Mugabe na Viongozi wengine kama Al Bashir and Company.

Utaki demokrasia vuta kabisa mfumo wa vyama vingi kwenye katiba yako..utaki wageni na wewe usitembelee wengine.

Kama kiongozi anaongoza kwa kukandamiza haki za Rais anastaili kupingwa kwa nguvu zote tena ata bila msaada wa Marekani. Leo kiongozi kisa ni waziri hana biashara anazofanya lakini ameficha mabilion kwenye Benki na wananchi wanakosa maji ya kunywa alafu wananchi wakiandamana Anadai wanatumwa na nchi za Ulaya.

Hayo Mambo ya Tamaduni kwa kuwaita majina ya watoto wetu majina ya kizungu ni ujinga wenu huko mnajiita Wasomi. Mtu yupo Hapo Tandale anamwita mtoto wake Thomson lakini uwezi mkuta Huyo Thomson akamwita mwanae Simba.
 
Naona hujaelewa mada

Kwahiyo miaka yote hiyo marekani haina mwanamke mwenye vigezo kuongoza?
 
Demokrasia haina maana ya kuchagua watu dhaifu kuongoza au wajinga kuwakilisha.
Pamoja na kuhakikisha uwepo wa demokrasia, ni lazima vigezo na masharti kuzingatiwa kwa mustakabali mwema wa jamii au taifa.
 
Hizi ni zama za kugombea rasilimali chache zilizobaki hapa duniani,baada ya watu kuzidi kuongezeka sana, hususan Afrika, kufuatia UKIMWI kushindwa kuwafyeka Weusi wote kabisa.

Kuna madai kwamba Virusi vya Ukimwi vilitengenezwa katika Maabara za Kijeshi huko Marekani, chini ya usimamizi wa akina Henry Alfred Kissinger. Hili liliweke kiporo, tutalijadili baadaye.

Marekani inayojidai sana kuhimiza haki za binadamu, usawa wa kijinsia,haki za wanawake n.k ikiwa haijawahi kuongozwa na Mwanamke miaka takriban 240 tangu uhuru.

Sehemu nyingine ulimwenguni akina Yingluck Shinawatra wa Thai, wameongoza, akina Christina Kirchner huko Argentina, Ellen Johnson Sirlief na Joyce Banda hapa Afrika, akina Dilma Rousef huko Brazil, akina Christina Lagarde wanaoongoza Fuko la Fedha (IMF), Asha Rose Migiro amekuwa Naibu Katibu Mkuu UN, Michelle Bechelet amekuwa Rais Chile tangu Januari, 2006.

Wapo akina Angela Merkel, na Margaret Thatcher huko Ulaya, lakini Marekani mwanamke hajawahi kuchaguliwa kuwa Rais, na sasa wapo marais 44.

Demokrasia, husemwa kuanzia Ugiriki,lakini hata Wagiriki hawakuruhusu mwanamke kupiga kura wala kupigiwa kura, sembuse kuongoza?

Leo, demokrasia hiyo ya Kigiriki huonekana kuwa na viraka vikubwa sana kwa kuwanyima akina mama kuwa viongozi,na hata kuwakataza kupiga kura.

Ndivyo walivyofanya Taliban huko Afghanistan, wakaonekana wa ajabu sana! Kumbe, kuna namna nyingine ya ukandamizaji hata Ulaya na Marekani, lakini nani awaambie?

Wao huiona Afrika, Asia na Amerika Kusini kwamba ndiko kwenye mbinyo wa demokrasia, kumbe nyani haoni kundule!

Si bahati mbaya, ni kusudi kuikamata dunia na kuiburuza watakavyo.

Katika Ujnabii wa Biblia,katika Ufunuo wa Yohana 16:12 kumetabiriwa ‘Roho Tatu za Vyura’ ambazo ni ‘Utatu Mtakatifu’ bandia hapa duniani, zikitoka kinywani mwa Shetani na kuwalazimisha Wakuu (Marais, Mawaziri Wakuu, Wafalme n.k) kuandaa vita dhidi ya Mungu Mwenyezi.

Chura ni alama ya uchafu katika Misri ya kale, ambayo sasa tunaona jeshi likipindua demokrasia, kwa risasi za moto mkali kushinda hata zama za Saddam, Gaddafi na madikteta wenzao.

Chura alikuwa nembo ya mungu mke, Heget, aliyeaminiwa kuwa chimbuko la uhai kwa watoto wanaozaliwa-vijana.

Huu Utatu Mtakatifu(Evil Trio) wenye sura ya vyura wa Misri, unavaa umizimu,uasi wa kidini, na ile hali ya vijana kuona DHAMB I(Uasi wa sheria ya Mungu) kama si kitu kikubwa!

Watoto wa siku hizi wenye haki za Kimarekani za kutokanywa wafanyapo makosa (Haki za Watoto), haki bandia za akina mama n.k huleta uhuru dhidi ya Mungu.

Mungu angejulikana mji anaokaa vijana wangeandamana hadi mlangoni,ili kumdai ajiuzulu na afungwe jela kwa kuweka sheria (kandamizi?) za kuwanyima uhuru wa kufanya wapendavyo!

Watu kama Obama na kina David Cameroon wanajiona vijana sana wa siku hizi, hata hawaoni ushoga na usagaji kuwa ni tatizo, bali tatizo ni watu kunyimwa haki,uhuru na demokrasia!

Mila za Afrika zinaheshimu sana ndoa ya watu wa jinsia tofauti (Heterosexual couples), wanaamini Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu mwaka 4004 BC kwa sababu na maakusudi muhimu ya kuanzisha familia.

Roho Tatu za vyura zinapinga kwa dhati ndoa kuwa ya mume na mke tu, bali hata ya mume na mume au mke kwa mke,mradi wamekubaliana-huu ni Uhuru kamilifu!

Akina Obama,David Cameron,Blair na wenzao, waliwapongeza sana wanaume waliofunga ndoa na waume wenzao kwa uhuru wao wa kikatiba, na hata walilazimisha Afrika ibadili katiba ili kuruhusu ushoga na usagaji kama inajitakia mema kwa mataifa haya.

Naam, kama Afrika inataka uchumi wake ukue na kuwe na amani na usalama kisiasa, kijamii na kiuchumi. na kiroho bila shaka.

Siku hizi watoto huzaliwa kwenye chupa za maabara (test tube babies) na mwanaume aweza kubadili jinsi kwa operesheni akawa mwanamke, akaolewa akazaa!

Hii huitwa transgender, na kuna sayansi ya human cloning, sasa Mungu naye wa nini sheria zake?

Leo, Afrika wazee ni wachache,vijana wanaotazama mitandao ya twitter na face book ndiyo wengi, ikipigwa kura ya kumkataa Mungu, inafanikiwa na inazidi kufanikiwa sana.

Akina Thomas Batie waliozaliwa Hawaii mwaka 1974 wakiwa wanawake,wakiitwa Tracy Logondino, walishabadilika na kuwa baba,sasa unasemaje? Demokrasia.

Kibaya zaidi, demokrasia ya Ulaya na Marekani hulazimishwa kufuatwa na ulimwengu wote.

Ukitaka kubadili jinsi unachomwa sindano zenye hormone (testosterone injections) kama ni msichana unapata sauti nzito, nywele fupi, unawekewa uume kwa operesheni, basi unakuwa dume jike!

Unaondolewa matiti kwa operesheni (Mastectomy), ukitaka uke au uume unaondolewa basi –ndiyo uhuru huu.

Hapa Afrika, kuna NGOs nyingi za kutetea mambo haya,serikali inapopinga inaonekana ya Kiimla, isiyojali Haki za watu na vijana wanaanza kuandamana na kupinga serikali, kama huko Misri, Libya, Tunisia, Yemen n.k

Na viongozi wanaopinga sera za Ulaya wanapinduliwa na kuswekwa rumande kwamba mafisadi, wananyimwa misaada, uchumi unakuwa mbaya sana,vijana wana ‘riot’ nguvu iitwayo ya Umma inafanya kazi!

‘Nguvu ya Umma’ aghalabu ni Nguvu ya Utatu Mtakatifu (Evil Trio); nguvu hiyo husukumwa na umizimu wa kutisha-spiritualism.

Uhuru wa ngono, picha za uchi, wanawake kujiuza, ukahaba wa kutisha, ushenzi ndiyo uhuru unaopendwa mno na vijana, na uhalifu; hawa wangependa magereza yasiwepo, hata kodi hawataki kulipa, ila waishi maisha ya raha bila kujua pesa zitatoka wapi?

Kwa akili hizi za kukosekana uzalendo,zama za utandawizi,hakuna mzalendo atakayezaliwa Afrika, bali kufanyika weusi wa Magharibi (Westernization), na watu vijana wametimka vijijini kujaa mijini (Urbanization) ili iwe rahisi kuwateka kwa kampeni za wanasiasa na NGOs za Ulaya na Marekani!

Hamkani si shwari katika nchi za Kiarabu(Unrest in Arab Countries) huashiria Yemen, Misri, Libya, Syria, Irak, Oman, Mauritania, Saudia, Jordan, Tunisia n.k asiwepo wa kupinga utandawazi kwa kisingizio cha dini n.k.

Nchi ambazo hakuna migogoro kama Qatar, Kuwait, UAE, Lebanon na Bahrain ujue viongozi wake wameafiki kimya kimya ajenda za wakubwa wa dunia, na raia hawana ubishi.

Rasilimali na kila kitu kinakwenda Ulaya bila taabu, inapotokea shida vita huanza na vijana hutumika kupinga serikali na kuanzisha ghasia na machafuko nchi nzima.

Marekani siku hizi huhimiza sana uhuru na demokrasia, FREEDOM of worship, freedom of speech, rule of law, equal rights for all-ndiyo ushoga na usagaji!

Sasa ikianzishwa dini ya kusali vijana na wasichana wakiwa uchi wewe ujidai kuikataa na kuwatia mbaroni uone. Tuendako hakutakuwa na ndoa tena,bali ni ngono holela tu na kuzaa vitoto visivyo na baba na mama zao walishakwenda danguro kujiuza,basi shetani analetea NGOs fedha za kulea yatima,zinaliwa, serikali ikisema inapingwa!

Sitetei mafisadi na wauza unga wa serikalini, bali nazungumza NGOs zinazojidai kutetea wanahabari kwa mfano, zinaombwa fedha nyingi Ulaya, vinaanzishwa vijiwe vya siasa kuipinga serikali maana inabinya demokrasia (ushoga, usagaji, uchafu) waandishi wa habari wametumika kuwabeba hawa migongoni mwao, siku hizi wana fedha, wana magari ya fahari kwa wizi na utapeli, ili mradi serikali ipingwe, Wazungu walete hela.

Dunia inaandaliwa kwa vita iitwayo Armageddon (tazama Zaburi sura ya 2).

“Anti Christ” and His Western Allies, wanajiandaa kwa vita dhidi ya haki halisi na ukweli,nchi zote na watu wote hawana budi kukubali.

Siasa ni Ulaya na Marekani,uchumi wa Kimarekani, rasilimali ziende Marekani, maisha na lugha, mila na desturi vya Ulaya na Marekani, na viongozi wawe wale wanaopendwa na Ulaya na Marekani!

Nchi zetu zimebinafsishwa Marekani na Ulaya, na akina mama hawataki uafrika tena, mara ‘makalio ya Kichina’ mawigi ya Magharibi, wanakula Kimagharibi siku hizi Mwafrika halisi kama Mandela hayupo!

“Middle East” the focal point of the World damu yao itatiririka kama mto ili kuwavua akili za Kikomunisti (Ukomunisti ni ile hali ya rasilimali zote kumilikiwa na jamii,nchi na serikali ina dhibiti uchumi), na akina sisi tulielekea Usoshalisti (mfumo ambao uliipa nafasi jamii nzima kuwa wabia ama wamiliki wa rasilimali na njia kuu za uchumi kama usafiri n.k).

Akili zetu zinaondolewa kutoka ukomunisti na usoshalisti,ili tuishi kutazama kila kitu kutoka Ulaya, Marekani, tukiwadhania wajomba na ndugu, sisi tulishasahau kujitegemea-ni michongo tu, rushwa, ufisadi na ‘kupiga hela’ bila kujua zinatoka wapi?

Halafu kelele na kushabikia kila ujinga kutoka kwa wanasiasa, Ulaya, Marekani n.k mradi kimesemwa,na hakuna tafakuri tunduizi!

Kufuatia hali hii,nchi inabaki haina kitu,mali inakwenda,viongozi nao wanakuwa watumwa wa sera za Ulaya, raia wanavaa mawigi na kutamani wawe Wachina au Wazungu!

Majina kama ya akina Mandela sasa yanapigwa marufuku, unazaa motto unamwita jina la Mzungu, makalio ya Kichina, nywele za Kizungu, kuongea lugha isiyoeleweka, nguo za Masela wa Kimarekani, wabwia unga, Malaya!

Taifa gani tunajenga? Akili gani hii, yaku compromise na Mzungu (hata Mzungu wa unga) hata hatuna chetu?

Akitokea kiongozi wa kuwapinga Wazungu, anapingwa sana kwa maaandamano ya umma huku tukisema ni nguvu ya umma, anakamatwa na kuwekwa kizuizini, watu wanashangilia, misaada inamwagwa-tunacheka!

Vema tukaanza kufanya mapinduzi yakifikra ili tutambue wapi tunakwenda? Tuna viongozi sampuli gani? Raia wa akili gani hawa, jamii gani hii tunajenga sasa?

Halafu tutajua kuipinga Marekani na ubeberu wake wa kutaka kutupora tangu rasilimali hadi tamaduni, mila na kila tulichonacho!
Sijakuelewa kabisaaaa!

Unaongelea mwanamke kuwa kiongozi????

Vyura uchafu??

Ama unaongelea mambo ya dini??

Ama Marekani kuongozwa na mwanamke?????

Unatuchanganya bhana, tuweke wazi, na tena fupisha mada yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anataka kujifanya anajua kila kitu. Propaganda za zamani sana hizi, hueleweki kama unalaumu au unaelekeza, unaongea siasa au imani. Sijui darasani essay writing ulikuwa unapata alama ngapi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom