omugabire
Senior Member
- Jun 17, 2019
- 128
- 174
Katika hali ya kushangaza mwanafunzi mmoja mkoani Mara amegoma kuendelea na elimu ya kidato cha kwanza kwa madai kwamba hana akili.
Mwanafunzi huyo amesema anashangaa kwanini amefaulu wakati alifanya mtihani vibaya kwa makusudi. Katika hatua nyingine mwanafunzi huyo amedai yuko radhi akamatwe na jeshi la polisi kuliko kwenda shule.
Nini maoni yako?
=====
Mwanafunzi agoma kwenda kidato cha kwanza kwa madai kuwa hana akili
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 jina tunalihifadhi aliyefaulu kwenda kidato cha kwanza kwa wastani C katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu wilaya ya Musoma mkoa wa Mara amegoma kwenda shule kwa kile anachodai hana akili ya kusoma masomo ya sekondari huku akitamka mbele ya mkuu wa wilaya kuwa yuko tayari kufungwa na si kusoma.
Akizungumza na ITV akiwa nyumbani kwao mwanafunzi huo amesema alifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana vibaya ili asifaulu lakini anashangazwa na matokeo yanayoonyesha amefaulu na kudai hayuko tayari kusoma huku akiomba akajifunze kushona cherehani kwani anataka kuwa mwanamitindo
ITV imewatafuta wazazi wa binti huyo na kuzungmza nao ambapo wamesema wamesikitishwa na uamuzi wa mtoto wao na kudai kuwa binti yao ametoweka kusikojulikana tangu tarehe 25 mwaka jana na kumtafuta kila mahali lakini baada ya mkuu wa wilaya juzi kutangaza kuwakamata na kuwafunga wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shule ndipo mwanafunzi huyo alipoibuka na kuwataka wazazi wake wampeleke kwa mkuu wa wilaya ili akamueleze kuwa hataki kusoma.
Chanzo: ITV
Sent using Jamii Forums mobile app