Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,588
Hivi kuna huduma yoyote inayofanana na mapquest Tanzania?
Hivi kuna huduma yoyote inayofanana na mapquest Tanzania?
Sidhani kama itakuwepo, maana kuna mitaa mingi haina majina halafu pale uhindini wahindi wamebadilisha majina ya mitaa mingi na kuweka majina ya kihindi bila hata ya kuwa na kibali cha jiji.
Mitaa hipi tena BAKSidhani kama itakuwepo, maana kuna mitaa mingi haina majina halafu pale uhindini wahindi wamebadilisha majina ya mitaa mingi na kuweka majina ya kihindi bila hata ya kuwa na kibali cha jiji.
Mitaa hipi tena BAK
Hivi kuna huduma yoyote inayofanana na mapquest Tanzania?
Majina ya mitaa Dar yabadilishwa kinyemela
Na Happy Wamanyamba
BAADHI ya mitaa maarufu katikati ya Jiji la Dar es Salaam imebadilishwa majina, huku uongozi wa Jiji na Manispaa ya Ilala ukidai kutokuwa na taarifa za mtu aliyebadili majina hayo.
Baadhi ya mitaa iliyobadilishwa majina ni Mtaa wa Kisutu ambao hivi sasa unajulikana kwa jina la Mtaa wa Pramukh Swami, na mwingine ni mtaa uliopo jirani na mitaa ya Jamhuri na Zanaki, ambao sasa umebadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Hazrat Abbas (A.S).
Viongozi wa Jiji na Manispaa ya Ilala ambao walizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wote walikwepa kuzungumzia suala, wakidai kuwa si wahusika.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Alhaji Adam Kimbisa , alipoulizwa kuhusu taratibu zilizotumika katika kubadilisha majina ya mitaa hiyo, alisema wahusika wakuu ni Meya wa Manispaa ya Ilala na si yeye.
"Waulize mameya wa manispaa husika wao ndio wanajua wanatumia taratibu gani, kwani kila manispaa inataratibu zake, hivyo mimi sijui ni taratibu gani zimetumika katika kubadili majina hayo," alisema Kimbisa.
Mbali ya Kimbisa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, ambako mitaa imebadilishwa majina na kupewa majina ya wageni, naye alikwepa kuzungumzia mabadiliko hayo.
"Ni mitaa gani imebadilishwa? Mbona mimi siijui? Hata hivyo taratibu zilizotumika katika kubadili majina ya mitaa sizijui, labda watafute madiwani na wenyeviti wa mitaa husika ili waweze kueleza sababu za kubadilisha majina ya mitaa hiyo, ila mimi sifahamu," alisema Jumaa.
Kubadilishwa kwa mitaa hiyo kiholela kumekuwa kukisababishia baadhi ya watu, hasa wageni, kupata usumbufu, kutokana na majina yaliyozoeleka kubadilishwa.
Kwa kawaida, majina ya mitaa hubadilishwa na manispaa zinazohusika, na mara kwa mara, majina ya watu maarufu katika taifa au hata maeneo ya kihistoria na mambo kama hayo, hutumika kupata majina ya mitaa.
Ha ha ha!What have you been thinking?
ama kweli SHAMBA LA BIBI........hadi mitaa inabadilishwa watu hawana habari.......
Basi ipo kazi, kwani wahusika haswa ni nani... Serikali za mitaa au serikali kuu.Majina ya mitaa Dar yabadilishwa kinyemela
Na Happy Wamanyamba
BAADHI ya mitaa maarufu katikati ya Jiji la Dar es Salaam imebadilishwa majina, ...ni Mtaa wa Kisutu ambao hivi sasa unajulikana kwa jina la Mtaa wa Pramukh Swami, na mwingine ni mtaa uliopo jirani na mitaa ya Jamhuri na Zanaki, ambao sasa umebadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Hazrat Abbas (A.S)...
Basi ipo kazi, kwani wahusika haswa ni nani... Serikali za mitaa au serikali kuu.