Mapokezi maalum kwa Maalim Seif kisiwani Pemba kutoka Airport yarindima barabarani

Ibra,
Katika mambo ambayo nayaona hapa jamvini ni haraka ya
watu kuandika tena kuandika ufedhuli.

Wingi ni lazima ufananishe.
Cairo kwa wakati fulani mchana mjini watu wake ni milioni 12.

Umati wa mji huu ukikusanyika ni umati mkubwa.

Tanta ni mji mdogo sana kwa Cairo hivyo umati wake ukikusanyika
utakuwa mdogo ukifananisha na Cairo.

Lakini haifanyi kuwa Tanta ikawa kuwa haiwezi kuwa na umati katika
mji.

Naamini umeelewa.

Na umati ule ni alfariri , Maalim aliingia Pemba Alfajiri
 
Tutaishia hapohapo kwa kuita rais,rais na wataendelea kutuongoza hao tunaodai wanatawala kwa nguvu!!
Lukesam,
Hapana.

Hayo yote unayoshuhudia akifanywa Maalim Seif na wananchi
ndiyo mambo ''hayajaishia,'' yanaendelea.

Si kuwa anatawala kwa nguvu.

Ingependeza kama ungesema kuwa alishindwa uchaguzi hapo
ingekuwa umesema vizuri.
 
M

Maigizo yanendelea sasa ni zamu ya pemba kufurahia maigizo ya Maalimu wa matamko,kamwe Maalimu hatakuwa raisi wa Zanzibar yeye ni Besigye wa Zanzibar hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Mfianchi,
Kuwa au kutokuwa si muhimu.
Muhimu ni historia ya Maalim Seif.

Maalim kashinda kila uchaguzi aloshiriki kuanzia 1995.
Muhimu ni hii heshima ambayo leo Wazanzibari wanampa.
 
Labda kwa wewe ilieambulia au kumwelewa mleta hoja Maalim Seff atakua amewasili kutoka Dar au Unguja? Ina maana ni kwa kipindi kirefu kiasi gani toka awepo Pemba hadi apokewe hivyo?Huu sio utaratibu unaokubalika jukwaa hili uzi kama taarifa au majibizano kwani wote hatuko kwenye kichwa cha mleta uzi kujua aliyo nayo kichwani kwake.Kifupi ni uzi wake haujitoshelezi.


Uzi unaeleweka vizuri mbona hajatumia lugha ya mafumbo
 
Mfianchi,
Kuwa au kutokuwa si muhimu.
Muhimu ni historia ya Maalim Seif.

Maalim kashinda kila uchaguzi aloshiriki kuanzia 1995.
Muhimu ni hii heshima ambayo leo Wazanzibari wanampa.
Weka ushahidi hapa kama Maalim ameshinda kila uchaguzi kuanzia 1995
 
Weka ushahidi hapa kama Maalim ameshinda kila uchaguzi kuanzia 1995
Mfianchi,
Ikiwa wewe hii leo unaniomba mimi ushahidi wa Maalim
kushinda kila uchaguzi basi wewe hujui historia ya Zanzibar.

Sasa ikiwa huijui sijui kwa nini unataka kufanya ubishi kwa
kitu usichokijua.

Katika uchaguzi wa 1995 baada ya Salmin Amour kushindwa
urais wa Zanzibar na Maalim, Ali Ameir aliandika barua Tume
ya Uchaguzi kukataa matokeo yale.

Huu ni ushahidi wa kwanza.

Soma huu fanya utafiti wako na waulize wajuzi kisha rejea hapa
jamvini tuendelee na mjadala nikupe ushahidi mwingine.
 
WIN.jpg

 
Mi nilisema humu, watu wasilinganishe siasa za bara na siasa za zanzibar! Wenzetu wana uzalendo wa ukweli, moyo wanaouonyesha wapemba sasaivi....ni moyo uleule walioonyesha wazalendo wa s.afrika kwa mandela" na
sehem nyingi ambapo wazalendo walishikamana, bila kujali hali iliopo" walipinga kile walichokiona kwenye jamii yao ni dhulma, na walifanikiwa" kisiasa visiwani wanajielewa zaidi kuliko sisi wabara"
Siasa zilizoko bara ni za kistaarabu sana na huwezi linganisha na siasa za visa na visasi za kizanzibar. Zanzibar wanachukulia siasa kama vile kabila, sawa tu na utusi na uhutu. Namna hii hawatafika popote na siku wakiwa nje ya muungano lazima watoane uhalo.
 
akiwa na magari na ulinzi wa serikali asiyoitambua maalim seif ni msanii wa kisiasa kama kawaida anawaadaa wananchi wa pemba kuwa Dr. Shein hawezi kumaliza muda wake ni porojo ambazo zimekuwa zikijirudia ni heri angegomea kugombea urais lakini akaruhusu wanachama wake wagombee uwakilishi
 
Kuna shetani ameingia Afrika Mashariki. Tanzania, huko Zanzibar, CCM imepora ushindi wa CUF, Burundi Nkuruzinza amedharau katiba na kusababisha mauaji ya Warundi, Uganda Museveni kaamua kuendelea kuwa Rais kwa mkono wa chuma, DRC Rais Kabila mtu aliyekulia Tanzania, kwa jeuri tu ameamua kutoitisha uchaguzi, Rwanda Kagame ameamua kubadilisha katiba ili aendelee kuwa Rais wa maisha. Rais wetu ameamua kushikamana na wang'ang'ania madaraka wa siku nyingi, sijui wanampa uzoefu gani!!!

Afrika Mashariki kuna giza nene.
 
Mi nilisema humu, watu wasilinganishe siasa za bara na siasa za zanzibar! Wenzetu wana uzalendo wa ukweli, moyo wanaouonyesha wapemba sasaivi....ni moyo uleule walioonyesha wazalendo wa s.afrika kwa mandela" na sehem nyingi ambapo wazalendo walishikamana, bila kujali hali iliopo" walipinga kile walichokiona kwenye jamii yao ni dhulma, na walifanikiwa" kisiasa visiwani wanajielewa zaidi kuliko sisi wabara"
Kwa nini hakujiapisha kama Besije angalau akapata raha ya Kuala kamama Rais Na maburula wakamshangilia hata kama ni Rais comedy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom