Mapishi ya Samaki Wabichi Chukuchuku

Gongolo

Member
Oct 21, 2010
83
18
Mapishi ya Samaki Wabichi Chukuchuku

Samaki wabishi wawili
Kitunguu saumu kimoja
Kitunguu maji kimoja
Nyanya mbili kubwa
Tangawizi kidogo
Ndimu mbili
Pilipili ndefu (nyekundu) moja
Chumvi half teasp
Maji vikombe vitatu

Safisha samaki vizuri na kama ni wakubwa kata vipande viwili
Menya kitunguu maji
Menya kitunguu saumu
Menya Tangawizi
Weka kwenye blender kitunguu maji, Tangawizi, nyanya na saumu na pilipili usage viwe laini
Chukua samaki weka kwenye sufuria
Weka mchanganyiko wa kitunguu maji,Tangawizi, saumu, nyanya na pilipili kwenye sufuria
Weka chumvi kwenye mchanganyiko
Kata ndimu na uzikamulie kwenye mchanganyiko
Ongeza maji
Chemsha mchanganyiko huu ukiwa umefunikwa kwa dakika15 kwa moto wa polepole
maji yakiwa nusu palia mkaa juu kama vile unapalia wali
Acha uchemke huku ukiangalia kila mara mpaka samaki wabadilike
Ukifungua utakuta samaki wamekuwa brown na mchuzi unaladha nzuri kwelikweli.


Chakula hiki hakina mafuta hata kidogo. Unaweza ukala na ukali, chapati n.k. upendavyo.
 
Nadhani ww ni mkerewe maana ndivyo wanavyopika ej sato. Kwa kumsaidia msomaji hakikisha samaki awe mkavu au mbichi anapikwa mda mrefu kama nyama. Samaki akiiva mchuzi huwa kama maziwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom