Mapigano Wakulima na Wafugaji yaibuka tena Mvomero-Morogororo

Hebu sasa tuache sanaa...hii ishu hata kwenye kampeni za uchaguzi last year kila mgombea alitoa njia za kuhakikisha hili suala linapata ufumbuzi wa kudumu. JPM alitabainisha wapiga kura kuwa amebaini chanzo ni sehemu kubwa ya ardhi ya tanzania kutumika bila kupimwa. Sasa hili tukio ni la pili tangu aingie madaraka na pia akiwa ameshatangaza baraza la mawaziri. Je suala hili linapewa uzito unaostahili kulingana na ahadi za mh. Rais, uzalendo anaojitabainisha nao waziri husika pamoja na ukubwa wa athari wa haya matukio??
 
Simple and clear, mashamba yako stationary wakati mifugo inatembea kufuata mashamba. Wamasai hawa watiwe adabu. La sivyo wananchi wawashughulikie kadiri wanavyona ni sawa. Hakuna namna.
Na hao unaosema washughulikiwe wakiamua kushughulikia kutakalika?
Acha uchochezi
 
Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la "Mwanu"

Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu hekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya Kimasai

Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.

Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

Chanzo: Star Tv Online

View attachment 322058 View attachment 322059

KUUNDWE KANDA MAALUM YA KIPOLISI KAMA WALIVYOFANYA TARIME NA ROLYA
 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro na mkuu wa wilaya ya Mvomero wanatakiwa wawajibishwe, kama JPJM alivyo ahidi kufanya kwa wote ambao wanashindwa kutatua migogoro.
 
Ndugu zangu mie ni mzaliwa wa hayo maeneo. Kiukweli ugomvi kati ya wakulima na wafungaji ni wa muda mrefu sana zaidi ya 25 iliyopita. Hakuna watu wenye dharau na mazao kama wamasai kuanzia Dumila, Msowero, Mvomero, Magole, Mandel, Wame Dakawa, Wame Magereza, Wame Sokoine nimetaja maeneo makubwa kubwa tu ila ndani yake kuna vijiji vingi tu. Chuki zilianzia baada ya mkulima mazao yake yakiliwa atakimbilia police kesi ikishafika huko.hutopata haki yako mpaka utakata tamaa kwa hiyo nenda rudi. Serikali inalijua sana hili kuanzia Amos Makala, Sadiki Murad, Joeli Bendera, Mustafa Mkulo na wengine wengi. Na wilaya inayokumbwa na hizo shida ni Kilosa na Mvomero mkulima akikutwa na kosa huwajibishwa lakini si kwa mmasai japo sitetei uovu
 
  • Thanks
Reactions: nao
nilikuwa na shama maeneo hayo Masai kaingiza ng"ombe wake shambàni kwetu namuuliza ananiambia ikale wapi lakini Wa fugaji ni wamasai peke yao mbona wama ng"ati hawana ugomvi wapo pia wasukuma kule Kilombero mbona hakuna mapigano hawa wamasai Wa Dogo ,kiteto, Mvomero, sunya leiseri mbona wagomvi sana
Kwa asiewajua wamasai huwa wanajitanabaisha kuwa ni wapole na wenye upendo ila kwa kweli maasai siku zote ni mtu mwenye hila,ndumilakuwili,mwenye kujaa dharau.anaejinasibu na kulialia kuwa anaonewa,anaejiona mwenye haki ya kufanya analotaka na asiguswe.Hili nafikiri linachangiwa pia na silka yao kama kabila.Na tabia zao hizi ndio zimekuwa chachu ya kufanya migogoro hii kushamili kila kukicha.Hata kwenye national parks zilizopakana na vijiji vya jamii ya wamaasai wanakumbana na mitihani hiyo na huonekani wanyanyasaji ihali wamaasai ndio wavunjifu wa sheria.
 
Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la "Mwanu"

Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu hekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya Kimasai

Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.

Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

Chanzo: Star Tv Online

View attachment 322058 View attachment 322059
haiwezekani utaratibu wa ufugaji wa kichungaji kuendelea. wachungaji wanazurura nchi nzima na mifugo yao bila kujali mipaka ya ardhi za wakulima. idadi ya watu imeongezeka ufugaji huo wa kizamani utatuletea vita. uanzishwe utaratibu wa leseni za uchungaji zenye masharti ya eneo na wingi wa mfugo. si lazima kila mwanafamilia ya kichungaji kupata leseni wengine itafaa kufuata mfumo tofauti wa uchumi. nchi yote haiwezi kua shamba la wachungaji wa kimasai et al. eti wanasema kama raia wana uhuru wa kuishi popote nchini. ngombe sio raia kama kuna sheria au taratibu kuzuia makundi ya mifugo sehemu fulani inabidi kufuata sheria. uhuru wa raia kuishi popote sio uhuru wa kukwaza raia wengine.
 
Yanapotokea mapigano baina ya wakulma na wafugaji, mara zote wafugaji ndo chanzo
Sasa hivi afadhali unaonekana kidogo, asante JK, L46b7 mna-flow na nyuzi.

Ulishawahi kujiuliza chanzo haswa cha hii migogoro?
 
Mifugo wamekula nusu hekari tu, ambayo thamani yake sidhani kama inafika nusu million

Wao, wameua mbuzi na kondoo 200, ambao, kwa bei ya 50,000 mmoja, inafika takribani 10,000,000,

Na pili, mnyama hana akili, kwa nn ahukumiwe, tena kifo cha kikatili hivyo

Kwa nn wasikamate hiyo mifugo na kubinafsisha, kulingana thamani ya hasara waliyopata.

Hii ni chuki kubwa, tena ya kijinga kabisa, imeachwa imekuwa na kukomaa, imeota mizizi sasa
Ubarikiwe kaka kwa hekima na maono. Wale ni wanyama ni heri wangewakama wote na kuwauza hata kwa 15,000/= kwa kila mmoja. Hii ndo nchi ya amani Tanzania. Kuna watu ni makatiri kama roho ya mamba.
 
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Leo kumetokea mgogoro wa ardhi Wilaya ya Mvomero,ni week moja tu tangu Rais John Pombe Magufuli atoe kauli ya kuwa,Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wailaya wa eneo ambalo mauwaji au mapigano kati ya Wakulima na Wafugaji yatatokea,basi ajizulu haraka kabla ya kuwekwa kando.
Baada ya mgogoro huo kutokea huko Movemero Morogoro,hii ndio kauli za Waziri Mwigulu.

"Nipo Mvomero,Mgogoro wa wakulima na wafugaji,mbuzi zaidi ya 70 wamekatwakatwa.Haikubaliki,sheria na hatua za kudumu za tatizo hili zinakwenda kuchukuliwa haraka iwezekanavyo"....Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba
 
hapo ndio kwanza mapigano yanaandaliwa, hao mwanu wamepelekwa mafunzo ya jadi ili waweze kabiliana wafugugaji wanaolisha mifugo mashambani. hiki kikundi cha vijana kimechangishiwa fedha na wanakijiji. Sioni jitihada zozote za kina zinazofanywa na serikali wakati wahusika wote kuanzia mkuu wa mkoa kushuka chini wanajua a to z, tutarajie maafa zaidi maana wamasai nao ni lazima wanajiandaa kwa kulipiza kisasi. ikumbukwe tu last time hawa mwanu waliua ng'ombe 130 waliokuwa wanashikiliwa kwenye ofisi za kijiji, wamasai nao wakamvamia mkulima mfugaji wakasepa na ng'ombe 250.

hivyo visasi kuisha vinahitaji busara za hali ya juu.
 
Ni tanzn
View attachment 322137 View attachment 322138 View attachment 322140 View attachment 322142 View attachment 322143 View attachment 322144 Leo kumetokea mgogoro wa ardhi Wilaya ya Mvomero,ni week moja tu tangu Rais John Pombe Magufuli atoe kauli ya kuwa,Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wailaya wa eneo ambalo mauwaji au mapigano kati ya Wakulima na Wafugaji yatatokea,basi ajizulu haraka kabla ya kuwekwa kando.
Baada ya mgogoro huo kutokea huko Movemero Morogoro,hii ndio kauli za Waziri Mwigulu.

"Nipo Mvomero,Mgogoro wa wakulima na wafugaji,mbuzi zaidi ya 70 wamekatwakatwa.Haikubaliki,sheria na hatua za kudumu za tatizo hili zinakwenda kuchukuliwa haraka iwezekanavyo"....Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba
.
Ni tanzania tu pekee nchi inayoendeshwa kitapeli na matamko ya watawala badala ya sheria za msingi yaani katiba.
Haya sasa tutaona hayo matamko ya rais na waziri wake ni lipi litakuwa utatuzi wa mda.
.
 
Tatizo Kubwa Ni Kutokupimwa Ardhi Na Kuwekwa Ktk Mipango Miji!! Maeneo Ya Mashamba Ambayo Yatakuwa Ya Wale Wanaoendesha Shughuli Za Kilimo!! NA Yale Maeneo Ya Ufugaji Ambayo Yatatumiwa Na Wale Wanaoendesha Shughuli Za Ufugaji!! KWA Kuwekeza Miundombinu Mbinu Muhimu Ktk MAENEO Hayo!! IKIWA Ni MAJI, MARAMBO, MAJOSHO, ELIMU YA KILIMO CHA KISASA, Ambacho Kitawafanya Wakulima Kulima Kisasa Ktk. Ardhi Yenye Eneo Dogo, Lkn Watapata Mazao Ya Kutosha, Badala Ya Kulima MAENEO Makubwa Mno Na Mazao KIDUCHU!!!! PIA WAFUGAJI Kufuga, Ktk Eneo DOGO, Kwa Kupata Huduma Muhimu, Ikiwa Na Upandaji Wa Nyasi Za Malisho Ya Mifugo Yao, Kwani Watakuwa Na MAJI Ya Kutosha!!! KWANI Wakulima Wakihamasishwa Vizuri Wanaweza Kuchangia Ktk KUFANIKISHA Hayo (HASA WAFUGAJI) HIVYO Kupunguza Kwa Kiasi Kikubwa Hayo Mapambano Ya Miaka Nenda Miaka Rudi!!!!
 
Leo hii huko Mvomero yametokea mauaji ya mbuzi na kondoo katika mwendelezo wa mgogoro wa ardhi za malisho kati ya wakulima na wafugaji.
Waziri wa Kilimo amefanya jambo jema kutembelea site ya tukio pengine katika hali ya kujionea mwenyewe na kuzungumza na wahusika ili kupata ufumbuzi. Lakini jambo alilofanya kuvaa nguo za kijeshi ni Usanii mkubwa ili ionekane kama tishio au kwamba yuko tayari naye kwa mapambano.
Hizi siasa za kuendekeza usanii ndizo zinafanya wakati mwingine jambo la msingi lionekane kama uhuni tuu. Mwigulu acha usanii na unapaswa kuzungumza na wakulima na wafugaji kwa weledi sio kuwavalia magwanda kwani hayo wanayaona kila siku na wanapambana nayo, vaa sura ya busara kama mwanasiasa mshawishi.
ImageUploadedByJamiiForums1455029244.969100.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1455029263.494963.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1455029285.608519.jpg
 
Back
Top Bottom