Kilimanjaro: 9 wajeruhiwa katika vurugu kati ya wafugaji na wakulima baada ya Mifugo kuharibu takriban ekari 1,800 za nafaka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
1657533257473.png


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameagiza kukamatwa mifugo 1,450 iliyoingizwa kwenye mashamba ya wakulima eneo la West Kilimanjaro, Wilaya ya Siha ambayo imeharibu zaidi ya ekari 1,800 za ngano na maharage.

Kagaigai amechukua hatua hiyo leo Jumapili Julai 10, 2022 baada ya wafugaji hao ambao wanadaiwa kuwa ni jamii ya kimasai kuwavamia baadhi ya wakulima usiku na kuwajeruhi kwa kuwakata mapanga wakati wakizuia mifugo hiyo kutoingia kwenye mashamba yao.

Katika vurugu hizo watu tisa wamejeruhiwa huku Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa akisema wanawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo.

Akizungumza baada ya kutembelea mashamba hayo, Kagaigai amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya wafugaji hao ambao wanaleta vurugu katika mashamba ya wakulima.

'Hiki kilichofanyika ni uhalifu wa hali ya juu nimeelekeza vyombo vya usalama kukamata mifugo yote ambayo imeingizwa kwenye mashamba ya wakulima na tangu jana tumekamata mifugo zaidi ya 1,000 na hatuiachii mpaka sheria itakapochukua mkondo wake, na hatuna mchezo na hili,"

"Serikali iko imara kwa ajili ya kulinda wananchi na mali zao na mhalifu lazima tumshughulikie hilo jambo hatutalinyamazia atakayeingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima asidhani tumelala," amesema na kuongeza

"Lazima tuishi maisha ya kupendana na kuheshimiana kama ilivyo asili yetu kwa Watanzania, hii mifugo tuliyoikamata itakuwa ni fundisho kwa wafugaji hawa na hatuiachii mpaka sheria ichukue mkondo wake,na tujue hatma ya hawa wakulima,"

Kati ya mifugo hiyo iliyokamatwa ng'ombe ziko 485 huku mbuzi na kondoo zikiwa 965.

Diwani wa kata ya Ngarenairobi, Patrick Kimario amesema wakulima zaidi ya 9 wamejeruhi na wako katika hali mbaya baada ya wafugaji kuwavamia.

"Kama kiongozi wa hapa kwa kweli hali ni mbaya, wakulima hatulali majumbani tunalala mashambani kuchunga kilichopo, asilimia 90 tumekopa kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo, tumeweka walinzi mashambani lakini bado tunavamiwa na kupigwa,"

"Yaani imefika mahali wakulima wanavuna mazao mabichi shambani kutokana na uharibifu mkubwa uliofanyika, watu mazao yao yameliwa yote shambani na watu wamekopa hali ni mbaya sana kwa kweli,"

Mkulima wa ngano katika eneo hilo, Fausta Ally amesema mazao yake yameliwa na mifugo ekari 100 zimeliwa na mifugo huku akisema hajui atarudishaje mkopo aliyochukua benki.

"Jamani hatulali tumevamiwa na hawa wafugaji wameingiza mifugo yao kwenye mashamba yetu ukiangalia nyakati za usiku wanakuja kutuvamia na kutupiga, hili jambo linatuwia gumu,tunaomba serikali itoe msimamo wa hili,"amesema

Chanzo: Mwanachi
 
Wangepaka asali kwenye hayo mahindi, Ng'ombe wote sasa hivi wangekua Marehemu
 
Back
Top Bottom