Mapigano katika public hearing ya Muswada wa Katiba (Dsm) leo - Mwanafunzi ang'olewa meno!

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Nimepata taarifa za kusikitisha muda huu kuwa kwenye kongamano la katiba DSM mwanafunzi mmoja wa chuo cha ustawi wa jamii amepigwa na mabaunsa wa CCM na ameumizwa vibaya sana kiasi kwamba meno yote ya mbele yametolewa na kwa sasa yuko polisi anahangaika ili kupata PF3.

Ila alipotaka kusaidiwa na viongozi wa CHADEMA akiwemo Lwakatere na wengine alikataa kwa madai kuwa yeye sio CHADEMA hivyo ataenda polisi peke yake na hahitaji msaada wa watu wa CDM, na hata walipokamatwa wale mabaunsa waliompiga waliokolewa na baadhi ya watu ambao wamedhaniwa kuwa ni polisi waliokuw2a kwenye plain cloth na kuondolewa huku polisi waliokuwa kwenye diffender waki8wa wanawaangalia mpaka alipotokomea na ilikuwa ni mbele ya viongozi wa CCM.

NIta wajuza zaidi huyu kijana anaitwa nani na anaendeleaje mpaka sasa.
 
Safi sana, nadhani Tanzania tunayoitaka na kuiimba kila siku inakaribia kufika.
 
sasa mbona inakuwa ivo tena jamani? hii ni nini sasa? does it mean hatuwezi jadiliana bila kupigana?
 
watu wana shuguli zao, unawaalika kuhudhuria 'workshop' alafu inaishia kuwapiga mabomu na mengineyo!! Kwa walioona video za Tegeta/Kunduchi jana na waendelee na wimbo wao wa "Tanzania nchi ya amani ...wapinzani wanaleta vurugu"!
MUNGU INUSURU TANZANIA KUTOKA MATAPELI WA SIASA!
 
Nimepata taarifa za kusikitisha muda huu kuwa kwenye kongamano la katiba DSM mwanafunzi mmoja wa chuo cha ustawi wa jamii amepigwa na mabaunsa wa CCM na ameumizwa vibaya sana kiasi kwamba meno yote ya mbele yametolewa na kwa sasa yuko polisi anahangaika ili kupata PF3.

Ila alipotaka kusaidiwa na viongozi wa CHADEMA akiwemo Lwakatere na wengine alikataa kwa madai kuwa yeye sio CHADEMA hivyo ataenda polisi peke yake na hahitaji msaada wa watu wa CDM, na hata walipokamatwa wale mabaunsa waliompiga waliokolewa na baadhi ya watu ambao wamedhaniwa kuwa ni polisi waliokuw2a kwenye plain cloth na kuondolewa huku polisi waliokuwa kwenye diffender waki8wa wanawaangalia mpaka alipotokomea na ilikuwa ni mbele ya viongozi wa CCM.

NIta wajuza zaidi huyu kijana anaitwa nani na anaendeleaje mpaka sasa.

Tujuze alichangia ni kilichopelekea kupingwa? Au alifanya nini? Tupe na sababu ndo tukuelewe vizuri. Lakini inasikitisha sana, hii katiba imefikia hapo. Hii ni katiba tu au kuna kingine hatukijui sisi wananchi wa kawaida. Subiri tuone mwisho wake
 
Mara zote nimekuwa nikisema hapa JF kuwa hii nchi inajiongoza hakuna kiongozi........mimi nadhani hii ni dalili tosha kuonyesha kuwa hali si nzuri...Nachoshukuru na huyo kijana kutamka kuwa yeye si mwanachama wala si mshabiki wa CDM,maana la sivyo ingesemwa kuwa ni nguvu ya CDM...

FREEDOM IS COMING TOMORROW....
 
Hata Ivory cost walianza na mambo madogo madogo yasiyo hata na msingi lakini mwisho wa yote tunauona sasa.
Siku za wadhalimu zinahesabika.
 
Amepigwa na mabaunsa wa CCM! Amepigwa kwa nini? Ni lazima maelezo yatimie kwamba nini kilichotokea mpaka akapigwa na kwa sababu ni mtu anayeonekana anajua kutafuta haki yake basi ataitafuta. Hilo litakuwa jambo la busara kwake.

On another note, safari ya kuelekea katiba mpya ni ndefu. Kutakuwa na milima na mabonde. Mungu atuongoze tufike salama.
 
green guard wanajaribu kujiweka mbele kutetea pumba za viongoz wa sisiemu hasa huyo mnaita kikwete dr wa kusingiziwa na maswahiba wake wa udom
 
Back
Top Bottom