Mapenzi yanauma sana

A love

Member
May 17, 2021
93
119
Habari zenu, Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu, jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe muda ili atafute pesa zaidi, nilikubali lakin ilivofikia mwaka huu mwezi wa saba akasema tuachane , hivyo nilimkubalia maana mahusiano hayalazimishwi.

Ikumbukwe huyo kaka wakati nipo nae nilikuwa nikikataa wanaume wengine waliokuwa wakinifuata , baada ya kumuona yupo serious, niliamua kufanya nae malengo,Mimi ninapenda biashara japo elimu yangu chuo sikusomea mambo ya biashara, nilimshauri pamoja na kufanya nae mambo mengi sana, taratibu akaanza kutoka hatuwa aliyokuwa nayo na kwenda hatua ya juu zaidi ya kimaendeleo.

Baada ya kuona nimeshampenda ilifika hatua hadi alihama alipoishi bila kuniambia,lakini mim naishi na wazazi , baada ya Mimi kupafahamu kwake matokeo yake alinitambulisha kuwa mim n mdogo wake niliumia sana na ndy mwanzo wa kunifanya visa hadi tukaachana niliumia sana maana nilimpenda mno.

Sikutaka kupoteza muda pia kuna kaka alikuwa akinitaka niliamua kumkubalia ili nizidi kupoteza mawazo na kumsahau haraka yule wa mwanzo ,tulianza vizuri lakini na yeye yapita wiki moja Sasa tumesha achana, nilichokigundua kwake hakuwa serious na hatahivyo alitaka nimpende kwa pesa zake hivyo alitumia nguvu nyingi kunionesha alivyonavyo, baada ya Mimi kuona nimempima kwa vipimo vyangu ndipo aligundua kuwa nimejua anacho hitaji na kukndoka mwenyewe.

Ndg zangu yote haya yaliyo nikuta , kusema Ukweli ninahitaji faraja ya moyo saana ,maana ninatamani kuwa na mahusiano serious lakini wanaume kwa Sasa hawaeleweki, hata wawe wachaMungu ,hakuna lolote, inshot mi napenda kusali(mkristu) lakini mkaka akishajua jinsi ulivyo nae anakuja kwa style hiyo hiyo Ninahisi kwa Sasa hakuna waoaji maana nimekata tamaa kabisa.

Natamani sana kuwa hata na mpenzi anayejitambua , anayejua kutafuta pesa ,ambaye hajaoa wala Hana mtoto ,maana Mimi pia Sina mtoto, awe mtumishi , zaidi ya yote awe mchamungu .
 
Jambo la msingi ili kumsahau aliekuacha ni kukubaliana na hali kua ameshakuacha na si wako tena, jambo la pili ni kutokukurupuka kuingia kwenye mahusiano mapya mapema sana baada ya kuachana na jambo la tatu ni kutafuta kitu unachokipenda na kukifanya kwa ukamilifu itakusaidia kumsahau huyo aliekuacha.
 
Habari zenu ,Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu , jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe muda ili atafute pesa zaidi, nilikubali lakin ilivofikia mwaka huu mwezi wa saba akasema tuachane , hivyo nilimkubalia maana mahusiano hayalazimishwi.

Pole sana BiDada

Uwe na subra, utafanikiwa.
 
Jitahidi uwe na financial freedom, hakuna Mwanaume atakusumbua.
Yanakuuma kwakua ulitegemea akupe unafuu wa maisha wa kukuoa (My personal view) so huoni tena mwanga wa maisha.
Jitafutie maisha yako ukiwa stable wanaume watakukimbilia na kukulilia.
-This isn't my personal opinion, It's a Fact
 
Habari zenu ,Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu , jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe muda ili atafute pesa zaidi, nilikubali lakin ilivofikia mwaka huu mwezi wa saba akasema tuachane , hivyo nilimkubalia maana mahusiano hayalazimishwi.
1. Unataka mwanaume Mtumishi, je' awe mtumishi wa Mungu ndio unamaanisha?
2.Chura unayo?
 
Habari zenu ,Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu , jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe

Maneno ya mwisho ni summary ya hadithi yote....

Weka picha yako tujipime ubavu.
 
Jitahidi uwe na financial freedom, hakuna Mwanaume atakusumbua.
Yanakuuma kwakua ulitegemea akupe unafuu wa maisha wa kukuoa (My personal view) so huoni tena mwanga wa maisha.
Jitafutie maisha yako ukiwa stable wanaume watakukimbilia na kukulilia.
-This isn't my personal opinion, It's a Fact
Mdanganye tu..😂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom