Mapenzi kinyume cha maumbile na utumiaji mirungi ndio yanaathiri vijana kwa sasa

Wamajanga

Senior Member
Jun 24, 2014
133
47
Siku hizi huku uswahilini vijana wa kisasa wana tabia nzuri na wengi wana tabia mbaya na hizo tabia mbaya huwa wanaiga kutoka kwa watu maarufu bila kuangalia hasara zake, siku hizi kuna tabia nyingi mbaya ila kuna hizi mbili nataka nizizungumzie zinaathiri sana vijana nazo ni :-

(1)Mapenzi kinyume na maumbile
Siku hizi hiki kitendo cha kawaida tu kwa vijana japo zamani ni jambo la laana kubwa huku mtaani kuna vijana wengi kuanzia miaka 17 wanafanya kwa kushawishiwa na marafiki zao wa kiume au wenzao wanawahadithia wanavyofanyiwa wao huu upo sana huku na msichana mwenye tabia hizo anawindwa sana na mvulana yupo tayari kutoa chochote ili ampate.

(2)Mirungi
Hiki ni kilevi kikubwa sana kwa vijana kwa sasa na wengine hawajui madhara yoyote ya kilevi hiki na wengine hawajui kama ni dhambi au ni kosa kisheria na wengi wanatumia kwa kuamini inaongeza nguvu za kiume.

Wazazi na serikali muwe makini kwa hili
 
Back
Top Bottom