Mapambano dhidi ya ufisadi: Uganda waonyesha njia

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Kamati ya bunge ya maadili nchini Uganda imetangaza kuwasilisha bungeni hivi karibuni muswada utakao muwezesha mwananchi yeyote mwenye ushahidi wa ufisadi uliofanywa na kiongozi yeyote, aweze kuruhusiwa kumshtaki.

Muswada huo utailazimisha serikali kumpatia mwananchi huyo usaidizi/ushirikiano wowote atakaouhitaji ili kukamilisha upelelezi au ushahidi wake.

Na itakapotokea serikali imefanikiwa ku recover fedha iliyokuwa imefisadiwa, mwananchi huyo atajipatia 25% ya fedha hiyo.

Source:BBC

MYTAKE.
Sheria ya namna hiyo itatufaa sana hata hapa Tanzania. Hawa mafisadi wanaoitafuna nchi hii hadi jeshi la polisi linasema hawakamatiki tutaweza kuwashughulikia.
 
Back
Top Bottom