Mapacha waliopoteana kwa miaka 53, Stori iliyonitoa machozi

Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,962
3,600
Jana bhana, baada ya habari ya BBC, StarTV wakarusha documentary ya DW iliyokuwa ikielezea mapacha wawili wa kiyahudi waliozaliwa Ujerumani kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia.

Walizaliwa kipindi ambacho Hitler anachinja Mayahudi kwenye Holocaust, baba wa watoto hawa alikuwa anapigana upande wa Poland na alikuwa yuko vitani ameacha familia ikilelewa na mama.

Katika harakati za Hitler akaja kugundua mama ni Myahudi, mama ilivyogundulika hakutaka mambo mengi akajiua na kuacha watoto wakihangaika wasijue la kufanya, kwa wakati huo walikuwa na umri wa miaka minne.

Kufupisha stori, mtoto wa kiume wa kuitwa Adam alikuja kuokotwa kwenye mahandaki ya kujificha vita akiwa na afya mbaya akachukuliwa kwenda kulelewa na askari wa Poland aliyekuwa na watoto sita, akapewa jina jipya. Ambako hapo alikuja kula msoto wa maisha wa hatari. Unajua ile unaishi na familia inayokuona kirusi.

Mtoto wa kike wa kuitwa Ida akaja kulelewa kwenye familia ya kichungaji ambaye baadae wakaja kuhamia Marekani.

Msoto aliopitia mtoto wa kiume umekuja kuathiri sana maisha yake ya baadae alivyokuja kupatana na ndugu yake.

Kila siku kila mtu kati yao alikuwa akiandika kwenye magazeti kuwa anatafuta ndugu yake aliye survive Holocaust. Baadae baada ya miaka 53 walikuja kuunganishwa na hizo taarifa za magazeti.

Machozi yalinitoka kwa aina ya malezi waliyopitia hawa watoto. Nikawaza familia yangu itakavyoishi baada ya mimi kukata moto, dah.

Maisha ni fumbo kubwa!

Kama uliicheki na kuna kitu sijaweka vizuri unaweza kukazia.
 
Back
Top Bottom