Maoni yangu: TFF chunguzeni mechi ya Simba na Kagera

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
5,251
5,323
Kama heading ilivyo naomba uongozi wa TFF na wadau wote wa soka wachunguze mechi ya Simba na Kagera iliyopigwa Shinyanga.

Binafsi nimechukizwa na mwamuzi wa mchezo huo kwa kuonesha upendeleo wa wazi kwa timu ya Simba, mfano ile penati ambayo mpira ulifuata mkono na hakukua na kusudio lolote la beki

Tukiacha hilo goli la refa dakika za mwishoni kama sikosei Isihaka alichukua mpira kwa mikono zaidi ya ile ya beki wa Kagera refarii akaacha.

Kiukweli haya ndio mambo yanayorudisha nyuma soka letu, huyu refa anastahili adhabu kali sana.
 
Hata mimi niliona kama ulivyoona lkn lazima ujue kuwa RUSHWA ndo inaiangusha Africa karibu ktk nyanja zote, hasa pale mchezaji wa simba aliposhika mpira mbele ya refarii ili usimfikie adui ambaye angefunga goli la kusawazisha ilitakiwa atoe RED na penalty lkn wapi?
 
inasikitisha sana hii league ya bongo ovyo sana
 
Hawa ndo wanatufanya tuliosomea fani ya waamuz tz tuzaaurike na tushindwe kuchezesha mashindano ya nje,

mwamuz ameonesha dhahir shairi alikuwa na lake jambo hawa ndo wanaosababisha soka la bongo lizidi kudidimia na kupata bingwa asiye halali na kupelekea vilabu vyetu kuboronga kimataifa, soka la bongo lina dalili ya rushwa waamuz weng hawako fair wanapindisha sheria makusudi kwa masirahi zao.

binafsi naomba kwa hili tff muoneshe makucha yenu.
 
Kwa kipi ambacho kinaonesha rushwa ama leo undo mean a kuangalia mechi . MI nimeona ni human errors tatizo ni mpira Wa kusimuliwa undo unatusumbua humu.Simba kadominate from da beginning hadi anapata goal. Watu walijua Simba itakosa kwenye tatu bora henceforth inawauma sana
 
Kwa tff hii ya Malinzi na Kaburu wake hilo sahau.....

Ni sheeeedaaa! soka la bongo limevamiwa na viongoz wabaishaj hebu fuatilia background za kaburu kuhusu issue ya kumpa mulungula kado utagundua ushindi mwingi wanaupata kwa njia haramu na ujanja ujanja tu.
 
Ligi Kuu ya Tanzania ni Majanga tupu, kama refa alitoa penati kwa Simba kwa kosa kama hilo kwa nini asitoe penati kwa Kagera Sugar? Aibu kwa Waamuzi wetu. Soka letu litazidi kudidimia .
 
Kwa kipi ambacho kinaonesha rushwa ama leo undo mean a kuangalia mechi . MI nimeona ni human errors tatizo ni mpira Wa kusimuliwa undo unatusumbua humu.Simba kadominate from da beginning hadi anapata goal. Watu walijua Simba itakosa kwenye tatu bora henceforth inawauma sana

Tatu bora itakusaidia kushiriki mashindano gani
 
Ingieni mchezeshe. Kama mmepata uchungu nendeni Muhimbili wodi ya wazazi mkazalishwe.
 
Malinzi amefanya kosa kubwa kumweka kaburu tff..malinzi anadharrka vibaya
 
Mbona kwenye mechi na yanga hamkutaka tff wachunguze.Nyie mlivyowafunga kagera ilikuwa ni halali lakini simba kushinda ni rushwa pumbaf.
 
Malinzi amefanya kosa kubwa kumweka kaburu tff..malinzi anadharrka vibaya
Halafu siku hizi baada ya kugundua kuwa pale tifu tifu anavurunda ameamua kuhama jukwaa, yupo facebook na watoto wanadanganyana.....
Huyu muhaya sifuri kabisa sijui amebakisha miaka mingapi huyu atuachie shirikisho letu.
 
kama ni kuchunguza waanzie me hi ya kwanza ya Yanga dhidi ya JKT Mgambo ilyochezwa Uwanja Wa Taifa
Mechi yenyewe ya mgambo na yanga aliiona au umesimuliwa tu!!! Unaweza kunikumbusha tukio moja ambalo lilitokea kwenye ile game ambalo lilitia mashaka kuhusiana na maamuzi ya refarii!?

Je, ni nani leo asiyejua kama kagera suger wamechinjiwa baharini na yule refa wa kaburu!!! Mchezaji amekumbatia mpira kwa mikono kama anacheza rugby halafu refarii anapeta!?

Kwa style hii ya marefa wetu tanzania tutakuwa kichwa cha mwenda wazimu hata dunia ikianza tena
 
Hiv nduguzangu nyie bado mnaangalia mpira vumbi huu wa bongo?mtakufa na presur wakuu
 
Mleta uzi ungekuwa mzalendo kweli na unayejua soka kweli ungeanzia na ile mechi ya Yanga na Kagera Sugar uwanja wa Taifa, tuambie uhalali wa ile penati ambayo hata Sports Bar ya clouds tv walionyesha tukio zima si chini ya mara 3.

Usidhani watu wamekaa kimya hawayaoni yatokeayo mechi za Yanga ni kwamba Yanga wamezoeleka.
 
kama ni kuchunguza waanzie me hi ya kwanza ya Yanga dhidi ya JKT Mgambo ilyochezwa Uwanja Wa Taifa

Cha kushangaza maskini ya Mungu hawa hata hawajui Malinzi anamiliki kadi ya uanachama wa Timu gani. Tumewazoea wakukurupuka hawa ndio maana kila madai au kesi wanazopeleka TFF au FIFA wanarudishiwa mlangoni. Ina maana na Sepp Blatter naye ni mwanachama wa Simba?
 
Back
Top Bottom