Maoni ya Makongoro Mahanga Kuhusu Kushindwa kwa Sumaye

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,804
71,231
KUHUSU HILI LA MHESHIMIWA SUMAYE....

_Na: Dr. Milton Makongoro Mahanga_

Ni mawazo yangu kwamba Mhe. Frederick Sumaye na wapiga kura wa Baraza la Uongozi la Kanda ya Pwani wote wanaweza kuwa na sehemu yao ya lawama katika sakata la Sumaye kunyimwa kura za kuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo.

Kwa wapiga kura sehemu yao ya lawama inaweza kuonekana kwamba iko wazi zaidi wakati kwa upande wa Sumaye mtu anaweza kuona hastahili lawama, lakini kumbe anastahili lawama ambazo lazima uziangalie kwa jicho la tatu la kisiasa kuweza kuzitambua vizuri.

Nitafafanua.....

Kwa wapiga kura lawama zinaonekana ziko wazi kwa sababu wamemwadhibu Mhe. Sumaye kwenye sanduku la kura kwa sababu tu ya nia yake ya kutaka kutekeleza haki yake ya kikatiba na demokrasia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Taifa. Ni vigumu kuona ni sababu gani nzuri zilizowafanya wapiga kura walio wengi wa Kanda ya Pwani kumkataa Sumaye kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Kanda ya Pwani kwa kumpigia kura nyingi za HAPANA, tena baada ya kumwachia agombee nafasi hiyo peke yake bila mpinzani. Shida imetoka wapi ghafla? Ni rahisi kusema hakukuwa na sababu nzuri bali ni ile tu azma yake ya kugombea pia nafasi ya Uenyekiti Taifa ndiyo iliyomponza. Kama kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Taifa ni haki ya kidemokrasia ya mwanachama yeyote, kwanini wapiga kura wa Kanda ya Pwani wakaamua kumwadhibu Sumaye kwa hili?

Endelea kusoma.....

Nataka nieleze mazingira ambayo watu wanatakiwa wayaone kwa jicho la tatu la kisiasa kabla ya kuwapa lawama zote wapiga kura wa Kanda ya Pwani waliompigia kura za HAPANA Mhe. Sumaye. Ni imani yangu pia kwamba Mhe. Sumaye naye hakuangalia mazingira haya kwa umakini wa kisiasa hasa kwa mwanasiasa mkubwa na mkongwe kama yeye. Mazingira haya ni ya muda mrefu sasa ingawa mengine yamejitokeza kuelekea uchaguzi wa Kanda na siku yenyewe ya uchaguzi wa Kanda ya Pwani ambayo hayakuwa rafiki kwa upande wa Sumaye na yeye hakuyang'amua kabla kwa jicho kali la kisiasa. Baadhi ya mazingira haya toka kabla ya uchaguzi huu na mpaka wajumbe kupiga kura Kanda ya Pwani ni kama yafuatayo:-

1. Ukifuatilia mjadala na mchakato wa Uchaguzi wa Chadema ngazi ya Taifa mwaka huu, hata kabla haujatangazwa rasmi, kumekuwepo na hisia kali sana miongoni mwa wanachama wa Chadema, wanachama wa vyama vingine, wananchi wa kawaida na hata ndani ya vyombo vya Serikali vikiwemo vya usalama kuhusu kwa nini Mbowe bado anafaa au hafai kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Mijadala hii imefanyika kwa hisia kali kwenye mitandao ya kijamii na kwenye mijadala rasmi na isiyo rasmi. Kwa nini mjadala wa kufaa au kutofaa kwa Mbowe umechukua hisia kali sana, tena hadi nje ya Chama? Kwa asilimia kubwa ya wanachama, inaonekana kwamba wale wanaotaka Mbowe ang'olewe, hasa kutoka nje ya Chadema na kutoka Serikalini, hawafanyi hivyo kwa sababu ya kutetea demokrasia bali wana nia ovu, siyo ya kuokoa Chama bali ya kuangamiza Chama. Kwa nini? Kwa sababu kwa wanachadema walio wengi wanaamini kwamba, angalau katika kipindi cha miaka mitano ijayo hakuna mwanachadema aliye tayari na anayeweza kuiongoza Chadema vizuri kuliko Mbowe. Sababu zao ziko wazi: Mbowe ameongoza Chadema kwa ufanisi katika mazingira magumu sana ya kisiasa kwa Chama na kwake mwenyewe. Na kwa mazingira ya siasa nchini chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano, ni Mbowe tu kwa sasa anayeweza kuiongoza Chadema vizuri kuvuka wimbi hili. Ni mtazamo wa wanachadema hawa walio wengi kwamba kwa kutambua ukweli huu wabaya wa Chadema ndani na nje ya Chama, wangependa Mbowe aondoke leo na siyo mwaka 2024 ili Chama kiharibikiwe. Swali la kujiuliza: Sumaye amekuwa kundi gani? Kundi la kuona umuhimu wa Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti ili Chama kiendelee kuwa imara licha ya vitimbwi vingi kutoka Serikali ya CCM, au yuko kundi la wanaotaka Mbowe ang'oke hata kama hawana uhakika nani mwingine kipindi hiki anaweza kuibeba Chadema kama alivyofanya Mbowe? Hili ni swali la kwanza ambalo wapiga kura wa Kanda ya Pwani walijiuliza.

2. Mazingira ya pili ya kuangalia katika suala la Sumaye, na ambalo linatokana na yaliyojadiliwa hapo juu, ni kwamba kumekuwepo na hisia na maswali miongoni mwa wanachama wengi kwamba wanaojitokeza kutaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chadema ni kweli wanasukumwa na takwa la haki yao ya kikatiba na kidemokrasia tu au wanasukumwa na nguvu kutoka ndani na nje ya Chadema isiyompenda Mbowe na inayotaka tu aondolewe kwa maslahi ya wasioitakia mema Chadema na hasa Serikali ya CCM? Wengi wanahisi kuna ukweli wa hili la mwisho. Huenda hisia zao haziko sahihi sana, lakini je, Sumaye katika kutaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Taifa amejiuliza haya na anajiona yuko kundi gani? Au ameangalia tu demokrasia? Kwa mzoefu kama yeye ameshindwa kweli kusoma hisia hizi?

3. Kwa miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na viongozi wa Chadema ambao wameonekana kumpinga wazi wazi Mhe. Mbowe kwa kujaribu kuunda mbinu za kumng'oa na wengine kama wabunge Kubenea na Komu wamefikia hatua ya kuitwa mbele ya Kamati Kuu na kuonywa kwa matendo yao ukosefu wa kimaadili. Lakini hata baada ya kupewa onyo, waheshimiwa hawa wameonekana kuendelea na hujuma zao wakishirikiana na wanaowania nafasi hiyo ya juu kabisa, akiwamo Mhe. Cecil Mwambe. Pamoja nao kuna mtandao fulani ndani ya Chama nchi nzima wa wanaompinga Mbowe wakiongozwa na baadhi ya watendaji wakuu wa Chama hicho. Ingawa viongozi hawa ama watakanusha hili ama watasema ni haki yao ya kikatiba, na huenda ndivyo ilivyo, lakini kwa jicho la wanachadema walio wengi ni kwamba viongozi hawa wanatumiwa kwa nia ovu ya kuhujumu Chama, ama wakijua au bila wao kujua. Mhe. Sumaye pia katika siku za karibuni amesikika na kuthibitika kuwa na mawasiliano au ukaribu na watu hawa ambao wanahisiwa kuwa "wasaliti" wa Chama. Je, Mhe. Sumaye aliliona hili na kulitafakari kabla ya uamuzi wake wa kuchukua fomu ya kugombea ngazi ya Taifa? Na kwa hisia zile zile za awali, wapiga kura wa Kanda ya Pwani wanawezaje kulaumiwa kwa hatua yao ya kumtosa Sumaye?

4. Hili la Demokrasia. Wanasiasa tunapenda kujificha kwenye neno demokrasia kisiasa tu hasa linapokuja suala la kugombea uongozi. Utasikia mtu anasema "nataka kupambana na Mahanga kwenye nafasi yake kwa sababu ni demokrasia yangu". Lakini ukweli ni kwamba mtu huyo ameona mapungufu ya Mahanga ya kiuongozi na kwamba Mahanga hafai na nia yake ni kutaka amng'oe ili yeye afanye mazuri zaidi. Wakati wa kujibu swali moja la mjumbe wa Kanda ya Pwani kwenye uchaguzi huo, Ndugu Sumaye alijibu kwamba ana hakika ya asilimia zote kwamba hata akisimama na Mbowe, yeye Sumaye atashindwa kwa mbali sana! Maana yake ni kwamba hagombei ili amtoe Mbowe na kuleta mabadiliko ndani ya Chadema bali anagombea kwa ajili ya kutimiza tu haki yake ya kidemokrasia lakini bado Mbowe atashinda na kuwa Mwenyekiti! Hii ni hadaa ile ile ya wanasiasa wanapotaka kumng'oa mtu kwenye nafasi yake. Hivi kweli mtu kama Mzee Sumaye, Waziri Mkuu kwa miaka 10 anaweza kwenda kwenye uchaguzi wa "kushindwa vibaya" na Mbowe huku yeye akijua matokeo hayo kabla, ati kutimiza tu takwa la demokrasia? Bila shaka Sumaye anaona mapungufu ya Mbowe na kwamba yeye anaweza kuwa mbadala mzuri zaidi. Sasa kama ni hivyo kwa nini aseme ana hakika Mbowe atamshinda kwa mbali? Je, ni kwa ajili ya kuwahadaa wapiga kura wa Kanda ya Pwani ili wamchague kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda? Ilivyotokea ni kwamba wapiga kura hawakutaka kukubaliana na hadaa hiyo. Wakasema ni heri angesema tu kwamba kwa mtazamo wake kuna mapungufu anayoyaona kwenye uongozi wa juu wa Chadema, ndio maana anataka kupambana na Mbowe ili akishinda ayarekebishe. Ukizingatia nafasi na wadhifa mkubwa wa sasa na wa huko nyuma wa Mhe. Sumaye, hakutakiwa kujificha nyuma ya demokrasia tu. Sasa ukizingatia imani na hisia za Chadema kutaka kuhujumiwa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Sumaye na watu wengine wanawalaumuje wapiga kura wa Kanda ya Pwani kwa maamuzi yao?

Nihitimishe kwa kusema kwamba wakati watu kadhaa wakiwalaumu wapiga kura wa Kanda ya Pwani kwa "kumwadhibu" Sumaye aliyetaka kutekeleza demokrasia yake, wanatakiwa wajiulize, Je, Sumaye kwa uzoefu na wadhifa wake, hivi hatakiwi kulaumiwa kwa kushindwa kusoma mazingira ya kisiasa na alama za nyakati ndani ya Chadema na ndani ya nchi kwa sasa, hata kama anaipenda sana Chadema na hakuwa na nia mbaya katika kuchukua fomu ya Taifa?

Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kwamba Sumaye ana dhamira ya kweli na ya dhati kabisa ya kupambania mabadiliko, haki na usawa wa kisiasa nchini Tanzania unaobinywa na Serikali ya CCM, na anatamani sana CCM iondolewe madarakani mwaka 2020, lakini katika hili la sasa alishindwa kusoma kabisa alama za nyakati na mazingira ya sasa ya kisiasa...... Anatakiwa ajilaumu mwenyewe kwa kilichotokea Kibaha.

Copy & Paste kutoka chanzo kingine cha Habari.
 
Dr. Mzima unajikomba kwa Mbowe ili upate nini kwa mfano. Mahanga umetuangusha. Kwa hiyo kwa kadri ya mahanga Mbowe ni kiongozi pekee mwenye uwezo, na kwa comment hizo hata mgombea uraisi hakuna ndani ya cdm, au mnaona umwenyekiti cdm ni mkubwa kuliko uraisi! Wenzako washatangaza vita kwa wahamiaji kutoka ccm we jipendekezeee wee ila ukiingia anga za Mbowe anakukula kichwa faster
 
Hongera sana Kamanda Mahanga umesomeka,Wanachadema ni MH.Mbowe tu ndio anafaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema ,"Mti wenye matundu matamu kupigwa mawe"Mh.Mbowe anapingwa na CCM na Serikali jiulizeni kwanini? Mpeni kura zenu Mbowe kwa Uhai wa Chadema.
 
Sumaye anaipenda Chadema kuliko Mbowe.

Freeman yuko kibiashara zaidi ndio maana alizembea kwa makusudi ili Tundu Lisu na Joshua Nassari wapoteze ubunge!
 
Angalau una hoja!

Ni kweli Mbowe alitakiwa kupingwa ndani ya chadema ila sio kupingwa na watu wabovu kama Sumaye.

Ata ubalozi wa nyumba kumi atakiwi kupewa uyu fisadi mkubwa wa utawala wa Mkapa.
 
mh sumaye aliomba uenyekiti kanda na uenyekiti taifa kwa wakati mmoja angeshinda nafasi zote ingekuaje kiutendaji? makamanda mje hapa
huo ni ulafi wa madaraka walichomfanya kinapendeza sana anatamaa sana angebaki kuwa waziri mkuu mstaafu ale tu ? mungu mbariki mizengo pinda
 
Mbowe - jina hili ni kubwa. Ukubwa wake hautokani na ukubwa wa cheo bali unatokana na imani yake katika mabadiliko, msimamo usitetereka, uwezo wa kuyabeba magumu mengi yasiyobebeka.

Rais Magufuli alijiapiza kwa nguvu zake zote kuua upinzani. Pamoja na nguvu zote za kidola, Mbowe bado amesimama. Amefanyiwa uovu mwingi usiohesabika, tunaoujua na tusioujua, Mbowe bado amesimama. Watu wa namna hiyo ni wachache sana, siyo tu Tanzania bali Duniani.

Wanaomtaka Mbowe aendelee siyo wajinga, wanajua ugumu wa kumpata mtu kama Mbowe. Kuwa upinzani ni kukubali mateso, kifo, kufilisiwa, kulala lockups za polisi, jela, kujeruhiwa hata familia yako kuishi katika mateso - vyote kwa kuonewa na serikali yetu dhalimu, inayoamini katika ubaguzi na uonevu.

Kule CCM unaweza kupachika yeyote kuwa Mwenyekiti na mambo yatakwenda maana pembeni yupo IGP, Mkuu wa TISS, Jaji Mkuu, Rais, Mkuu wa Majeshi, Mawaziri, Matajiri, n.k. Huku upinzani, kiongozi unasimama kama wewe. Hata wafuasi wako na viongozi wenzio na watu unaowatetea wanaweza kukuacha. Wangapi wapo tayari kwenye mazingira kama hayo zaidinya Mbowe?

Pamoja na Mbowe, wapo makamanda walioiva katika misimamo na imani kama Lisu, Mdee, Lema, Lijuakali, yule wa Tunduma, Msigwa, Sugu, Masonga, (na wengine ambao wanajulikana japo majina yao sijayaweka hapa). Lakini jambo la kushangaza, hawa wote hakuna aliyefikiria kuchukua nafasi ya Mbowe.

Upinzani - sifa kubwa kuu ni MSIMAMO USIOYUMBA, KUJITOA NAFSI YAKO YOTE, KUWA TAYARI KWA YOTE KWAAJILI YA HAKI. KIUFUPI NI KUKUBALI KUWA SADAKA KWAAJILI YA WATU WENGINE.
 
Magu alikataa kofia mbili au huku mnakubaliana na hilo??
 
Sumaye baada ya kuingia CDM angebaki kuwa mshauri wa chama, na si kuingia field kama mwanasiasa mchanga.
 
Wanasiasa wetu wengi, ukiondoa wachache sana wanaojiamini, ni waganga njaa. Watawala wetu wenye uchu wa madaraka hutumia udhaifu huo kuwarubuni na kudhoofisha ushindani wa kisiasa. Mbowe ni kati ya wanasiasa wachache sana ambao wanaonekana kuwa vigumu kurubuniwa kwa vipande vya fedha. Huo ndio mtazamo wa wanachama wengi waaminifu wa Chadema. Kila anayetaka kushindana na Mbowe, hasa kipindi hiki kigumu ambapo agenda muhimu kuliko zote miongoni mwa watawala ni kuua ushindani wa kisiasa, wanaonekana wanatumiwa na adui. Kwa bahati mbaya sana wanasiasa wetu walioko madarakani sasa wamepwaya mno na hawafichi tena kuwa uhai wao kisiasa siyo ushawishi tena bali ghiliba, uhuni, rushwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma. Jitihada hizi za kubaki madarakani kwa gharama yoyote kupelekea jinai kubwa kufanyika. Jinai hizi kubwa hufanya baadhi ya watu kuona kuwa mabadiliko ni mwisho wa dunia kwao. Watu wa aina hii huweza kufanya chochote kuzuia hayo mabadiliko yasitokee. Kwa watu wanaohufu mabadiliko uchaguzi wa 2015 uliwaongezea hofu sana kwani ulionyesha kuwa tukiendelea hivi mabadiliko hayako mbali!
 
Mahanga hajasikia wajumbe kufungiwa hotelini siku mbili na kupelekwa kwa costa kupiga kura? Mahanga kama anaamini Mbowe anastahili na hana mpinzani si waache kura ziamue? Justification za kitoto sana.

Wajumbe walielekezwa cha kufanya na hilo ni doa baya sana kwa Chama! Uchaguzi wenyewe mmelazimishwa na msajili! Aibu! Aibu! Aibu!
 
Mbowe akipita bila kupingwa ni sawa lakini wana ccm wakipita bila kupingwa sio demokrasia hameleweki hamtaki nini na nini mnataka
 
huo ni ulafi wa madaraka walichomfanya kinapendeza sana anatamaa sana angebaki kuwa waziri mkuu mstaafu ale tu ? mungu mbariki mizengo pinda
Mzee alimwaga chozi alivyokosa tiketi ya kugombea urahisi. unajua kwa nn? Cheo cha uwaziri mkuu ni kibaya sana ukistaafu. mana unasubiri huruma ya kuteuliwa na mtawala mpya. Angalia wastaafu wote wanavyohaha kuutafuta urais mana wamezoea kukaa juu juu.
 
Back
Top Bottom