Maoni ya Edo Kumwembe kuhusu Kenya, yanadhirisha ukanjanja wa wanahabari wengi

Edo Kumwembe ni miongoni mwa vijana wachache wanajitambua hapa bongo!Wengi wetu tumeishia kushabikia zilipendwa vs ceduce me!Hatuna muda japo kujifunza mambo ya msingi na tunaamini kila aliyefanikiwa ni mpiga dili,kwamba kiongozi anaweza kunyoosha nchi!Kumbe kinachonyoosha nchi ni katiba na hatuna habari nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaishia kutukana lakini si kujibu hoja, Huyo Edo ni lini amejadili siasa? mbona kila uchwao yeye anajadili soka na wanasoka na ndio anapata kipato. Sasa wengine kujadili muziki kosa? kwani ili uonekane una akili ni lazima ujadili sukari 24/7?
basi utakua unamfuatilia edo kwa matukio.

sio mara moja huwa anaongelea siasa, jaribu kupitia profile yake yote.

poor argument from you! hivi mtu akijadili soka kila siku ndiyo anaondolewa uhalali wa kujadili siasa?

edo anawaita vijana wanapokuwa wakishabikia muziki, wasisahau pia masuala ya msingi kama haya na wala hajawataka waache kushabikia muziki
 
Unamshangaa Edo kwa kusema anachokiamini kuhusu watu wa aina yako tena katika muktadha usio rasmi huku ukiacha kumshangaa Rais wa nchi aliyewataka mfyatue tu yeye atawasomeshea bure, yaani hii sio makala ya muandishi kwenye gazeti.
 
Kama una akili hata kidogo lazima utakuliana nami ya kwamba Edo yeye kila uchwao anaandika na kujadili habari za wanasoka sasa kwanini anawadharau wanaojadili habari za wanamuziki?
hajawanyima watu kushabikia muziki, bali anataka wasipotelee kwenye muziki tu bali wayape nafasi pia mambo ya msingi ya manufaa ya taifa hili.

ndo maana yeye ni pundit wa soka but kayapa nafasi mambo ya katiba mpya pia.
 
AKILI NDOGO MTOA POST HIWEZI ELEWA MAMBO MAKUBWA,YA MAANA NA MAZITO ALIYOONGELEA EDO. ...au sivyo utakuwa mmoja wa watu aliowazungumzia
 
Kila jambo na wakati wake, yeye akijadili soka ni nani anamwambia ajadili sukari? na hao wanaojadili team Kiba na Diamond upo muda wao wa kujadili siasa. Suala hapa ni kulazimishana fani.
 
AKILI NDOGO MTOA POST HIWEZI ELEWA MAMBO MAKUBWA,YA MAANA NA MAZITO ALIYOONGELEA EDO. ...au sivyo utakuwa mmoja wa watu aliowazungumzia
Huyo Edo kama anaona sukari ni muhimu aache kujadili wanasoka kisha ajikite kwenye mjadala wa sukari na siasa kama ndio ''akili kubwa''.
 
Edo Kumwembe ni miongoni mwa vijana wachache wanajitambua hapa bongo!Wengi wetu tumeishia kushabikia zilipendwa vs ceduce me!Hatuna muda japo kujifunza mambo ya msingi na tunaamini kila aliyefanikiwa ni mpiga dili,kwamba kiongozi anaweza kunyoosha nchi!Kumbe kinachonyoosha nchi ni katiba na hatuna habari nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anajitambua kwa kipimo gani? muda wote anawasimulia habari za mpira vijana hao hao sasa iweje awashangae hao hao vijana kufutilia Ali kiba na Diamond?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom