Maoni: Kwaya ya KWETU PAZURI itumike kurudisha ushirikiano wa Tanzania na Rwanda

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
892
293
Kwa maoni yanga binafsi, nimejaribu kufikiria nini kitakachorudisha umoja kati ya Tanzania na Rwanda,nikaja kugundua kuwa burudani ni sehemu kuu ktk kuleta umoja, upendo na ushirikiano.

Mfano nyimbo ndizo zilizosaidia kuwaunganisha wa S. Afrika katika harakati zao za kupata uhuru, mfano mwingine ni kipindi cha mwaka wa 1995 na 2000 CCM iliweza kuwateka waTanzania kuwaunga mkono kwa kupitia nyimbo za Komba kama sikosei.

Hivyo basi kwaya ya KWETU PAZURI ni moja ya kwaya inayokubalika sana Tanzania kuliko hata Rwanda na ni wao ndio walioumbi wimbo wa "AMANI" ambao uligusa sana wanasiasa wa Afrika ya Mash na kati, ningeomba kwaya hii itumika katika kpindi hiki kigumu baina ya nchi hizi mbili, kwaya hii pia inaweza kwenda mbali kwa kutunga wimbo unaogusa Tanzania na Rwanda.

Ni maoni tu ndugu zangu. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI RWANDA!
 
xaxa sisi wapenda kaswida, mnanda /mchiriku tutaunganishwa na nini? au ndo udini unaanza mdogo mdogo kuwa "separating factor" na badala ya kuwa "unifying factor" sustain mleta mada.
 
La hasha si kumaanisha hvyo, bali ni wao kuimba nyimbo zenye msisitizo wa AMANI
xaxa sisi wapenda kaswida, mnanda /mchiriku tutaunganishwa na nini? au ndo udini unaanza mdogo mdogo kuwa "separating factor" na badala ya kuwa "unifying factor" sustain mleta mada.
 
Back
Top Bottom