Maoni;- Katika hili, Wazanzibari wanahaki kulalamika

Julius Kaisari

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,176
676
Kwanza nina- declare interest,Mimi ni Mtanganyika,na naipenda Tanganyika. Baada ya hayo,turudi kwenye mada. Nimekuwa natafakari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Tanganyika, kuanzia maandalizi,matangazo, ushiriki na kila kitu, nikajikuta naona kama " haya maadhimisho yanafanywa na Tanzania, ambayo na Zanzibar wamo.

Sijui kwa upande wa gharama ikoje,lakini kubwa zaidi ni ile dhana ya ushiriki kama TAIFA, huku ikiwa dhahiri inatuhusu Watanganyika, lakini ikifanywa na Tanzania. Sijui kama huko Zanzibar kuna hata kibwagizo kinachosikika,kuhusu Uhuru huo wa Tanganyika /tanzania/tanganyika /tanzania.....???? Je Ikifika Jubilee ya uhuru wa Zanzibar, itakuwa vipi?

Tanzania itahusika? walau hata kupiga Promo???? Nidhahiri huu muundo wa Serikali hautufai tena.

Mnaionaje jambo hili Wanajamvi?
 
wazanzibar hawaeleweki
mwanzoni ilionekana hawautaki muungano ila Tundu Lissu alipouchokonoa na kuonesha ni kwa namna gani kuna maswali yasiyojibika kuhusu huu muungano ni haohao wazanzibar walimshambulia kuwa anataka kuvunja muungano.
zanzibar waache hivyohivyo
 
Ni sawa, lakini hilo haliondoi uharamu huu wa mambo yanavyokwenda/endeshwa.
 
Katika huu Muungano ni Tanganyika inayobena gharama 90%
Kwa hiyo jambo lolote la Tanganyika ni la Tanzania wote, ila jambo la Zanzibar ni lao Wazanzibar
Hivyo sherehe hizi za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ni za Tanzania wote, ikifika miaka 50 ya mapinduzi watafanya wao
Haya ni maono yangu ktk muungano huu
 
wazanzibar hawaeleweki
mwanzoni ilionekana hawautaki muungano ila Tundu Lissu alipouchokonoa na kuonesha ni kwa namna gani kuna maswali yasiyojibika kuhusu huu muungano ni haohao wazanzibar walimshambulia kuwa anataka kuvunja muungano.
zanzibar waache hivyohivyo

UmenifuraHISHA NDUGU! Hawa watu ni kichekesho, anyway ndio maana Nyerere alimuingiza mkenge Karume.
 
Ni kwel wazanzibar they always complain about Mungano lakini wao mchango wao katika huu Muungano ni mdogo, compared to wanachokipata. But tuwabebe hivyo hivyo.
 
Ni kwel wazanzibar they always complain about Mungano lakini wao mchango wao katika huu Muungano ni mdogo, compared to wanachokipata. But tuwabebe hivyo hivyo.
hakuna kubebana hapa kama zanzibar ni nchi basi ni lazima tuuimalishe muungano tena kwa kuanzia tuiludishe TANGANYIKA,
KUUKOSOA NA KUREKEBISHA MUUNGANO SI DHAMBI!
 
hakuna kubebana hapa kama zanzibar ni nchi basi ni lazima tuuimalishe muungano tena kwa kuanzia tuiludishe TANGANYIKA,
KUUKOSOA NA KUREKEBISHA MUUNGANO SI DHAMBI!
Hakika. au Iwepo serikali moja. kwani serikali tatu kwa maana ya kuirudisha Tanganyika itatugharimu zaidi watanganganyika katika kuendesha serikali ya Muungano,ama sivyo Muungano upigwe panga. Hekima inahitajika zaidi ya ushabiki. Pia pamoja na yote,Wazanzibar waache majigambo,na mbwembwe.
 
Tuwachie waende zao! Watuache na Tanganyika yetu nao wabaki na Zanzibar yao labda kelele zitapungua! Wao kuwanyanyasa wabara waishio visiwani wanaona sawa, ngoja nasi tuwaambie wahame au waombe vibali vya kuishi na kufanyabiashara bara muone watakavyo lialia na kulalama!
 
Muungano una matatizo na hakuna Nchi inaitwa Tanganyika Duniani .Pia hakuna Nchi Duniani inaitwa Tanzania inatimiza miaka 50.Kosa kubwa ila wana siasa wamejiandaa kula nchi na pesa ukihoji mhaini .Leo wanasema uhuru wa Tanganyika kesho Lissu atahoji watakuja juu .
 
Back
Top Bottom