mwanawao
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 3,142
- 5,634
Dhumuni kubwa la Maonesho ya nane nane kwa kadri miaka inavyozidi kusonga mbele ndivyo yanavyozidi kupoteza uhalisia wake. Maonesho haya kwa siku nyingi yamekuwa yakijulikana kama maonesho ya wakulima. Uhalisia huu wa kuwahamasisha wakulima kuja kuona jinsi watakavyoweza kufanya kilimo kwa ufanisi zaidi umezidi kupotea jinsi siku zinavyo kwenda.
Watu mbalimbali wanaoenda kuangalia maonesho haya wengi tunategemea kukutana na mambo yatakayohamasisha ukuaji wa kilimo ndani ya nchi yetu. Lakini siku hizi cha kushangaza unapofika kwenye maonesho haya zaidi 50% utakutana na watu wakiuza bidhaa mbalimbali kutoka china, na nchi nyinginezo za Asia. Ukulima wetu hapa upo wapi? Je, maonesho ya nane nane yamegeuka kuwa maonesho ya kichina?
Utakutana na mabenki kibao yakiwa yanajitangaza. Sikatai wajitangaze. Je, katika kujitangaza kwao, ni benki ngapi kati ya hizo zinamjali na kumsaidia mkulima?
Je, kwenye maonesho haya kuna products za kilimo kweli ambazo zinaweza kumhamasisha mkulima kusonga mbele na kumuinua kiuchumi?
Wadau tuchangie ni namna gani tunaweza kuboresha maonesho haya yaweze kuwa tija kwa Taifa letu.