Manji atakiwa kuripoti Ofisi za Mamlaka ya Uhamiaji. Pasi 126 za kusafiria zakamatwa ofisini kwake

Manji ahitajika Uhamiaji: Ofisi ya uhamiaji jijini Dar imemtaka mfanyabiashara Yusufu Manji kuripoti kwenye ofisi hizo baada ya kutoka hospitali alikolazwa.

>> Ofisa Habari wa uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam
amedai kuwa Manji ameajiri watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

--------------------------------------

Kuacha habari hiyo mimi binafsi ningependa kuwashauri mamlaka ya uhamiaji ili kututhibitishia kuwa Operation hii kuwa sio ya visasi wala chuki binafsi kama inavyodhaniwa na wengi. Iendelee kwenye makampuni mengine hasaa yanayomilikiwa na Wahindi

Kumekuwa na Utitiri wa Raia wa India ambao wamekuwa wakifanya kazi ambazo wazawa wana uwezo wa kuzifanya

Wenzetu kenya wameweza kudhibiti utitiri wa Raia wakigeni kufanya kazi ambazo Raia wa kenya wana uwezo wa kuzifanya. Mfano mmojawapo ni kampuni ya Kenya Airways ukiacha Uongozi wa juu ambao ni Kuna Raia wa kigeni wachache. Wengine wote kuanzia mafundi wa ndege hadi marubani ni Wakenya wenyewe
983769e42f3f675acb9e7a422c8546a5.jpg



Mfano mwingine ni kiwanda chao cha kutengeneza Magadi soda yanayotumika kutengeneza sabuni na vitu vingi kana vioo na chupa za glasi (soda hash dese) kiwanda chao kinaitwa TATA CHEMICALS kinachomilikiwa na raia India


Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa maelfu ya watu kenya kuanzia ajira rasmi na zile zisizo rasmi. Lakini mshangao ni kuwa katika maelfu ya waajiriwa wa kiwanda hicho Wahindi wapo wawili tu yaani GM(General manager) na Mhindi anaye husika na maswala ya Account tuu,, wengine wote ni wakenya

Lakini hapa kwetu utakuta kampuni kuanzia Utawala hadi Operations sector kumejaa raia wa kigeni


Kuna mifano mingi saana. Kwani hawa wa Cina wanaochanganya zege au kuuza mitumba wana vibali vyakufanya kazi hapa Tanzania?
 
Kwa akili yako hizo pasi zilijileta Tanzania? Au Immigration wamezitengeneza?
NA WEWE KWA AKILI YAKO KUWA NA PASI NDIO UMEAJIRIWA? KWANI MGENI HARUHUSIWI KUINGIA NA KUPATA VISA YA MIEZI MIATATU ? UMESIKIA MTU AKIAJIRIWA KWA VISA YA MIEZI MITATU ? HALAFU ATATOKA VIPI ?
 
Hii ni Awamu ya Kulipiza Visasi na Kukomoana.

kupitia hizi chuki tunazidi kutengeneza ufukara na Umaskini ulio tukuka.
 
Ha ha ha ha ha ha......jamaa utadhani trafic Polisi, wakikukosa kwenye leseni, watadai kadi ya gari, wakikukosa hapo wataulizia bima.........ili mradi tu wakupate, hata kukuambia mbona gari chafu hawashindwi...........ngoja tusubiri mwisho wa hili saga.

Kuna jamaa alikamatwa pale Sayansi, Wakusanya Kodi wa Polisi wakacheki Leseni iko poa, Registration ya gari na Bima iko poa, Mara triagle ipo, Fire extingisher ipo, Spea tire ipo, Mkanda jamaa kafunga....Traffic kanuna, jamaa akaanza kucheka..Traffik akatazama wiper kasema eti zimeisha ...Dah jamaa kasema hapana hizo ni nzima traffic kakasirika eti jamaa anamfundisha kazi, Jamaa kakomaa hadi wakaitwa traffic wengine jamaa kakomaa wakamuachia eti akabadilishe zile wiper...Dah kiangazi Traffic kakomaa Eti wiper mbovu
 
UHAMIAJI WAKAMATA PASSPORT 126 QUALITY GROUP.



Upepo Mchafu Wazidi Kumuandama Manji, Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....

John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.

Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.

Mara tu atokapo, aliport ofisi hii ili tumuunganishwe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.

Utakamatwa, utawekwa ndani, utajibu mashitaka.
View attachment 470417
Yusuf Mehbub Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini Tanzaznia na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu(CCM) Jimbo la Mbagala Dar es Salaam. Vilevile ni Mwenyekiti wa Club ya Mpira ya Nchini Tanzania Yanga Afrika SC.

Kumbe uhamiaji wameanza hii kazi ya kufuatilia foreigners wanaofanya kazi hapa nchini bila work permit? Je zoezi ni kwa makampuni yote au ni kwa manji tu? Kama zoezi ni kwa wote basi...wakafanye uchunguzi hapa "orange company"

Na pia wanafuatilia na wale wageni wanaojidai wamekuja kufanya kazi hapa nchini kama professionals kwakuwa kwetu Tanzanai hatuna hizo professional na uhamiaji wanawapa vibali halafu eti wanafanya kazi za head of hr, head of finance, head of security, head of business, head of admin. head of customer service, head of cleanliness, head of transport, head of legal huku hawana hata certificates za hizo elimu. eti hizo taaluma hapa nchini hatuna? wataalamu wanatoka huko kwao halafu wanalipwa mishahara balaa over 5 to 10mil.hawakatwi kodi. wanakuwa na sleep salary mbili. moja inakatwa kodi analipwa 1.5mi. na ile ya mamilioni haikatwi kodi. Huku watanzania wakiendelea kulipwa btn 400 & 650 awe na first degree, masters, Diploma au certificate ama std7.

Nadhani kampuni za namna hii walipaswa kuzifuatilia sana kuliko kusubiri mtu mmoja atuhumiwe kwa madawa na aende hosp.ndiyo na uhamiaji wamsubirie apone wamkamate kama hakuna vitu vya kufanya wakakague passport za wafanayakazi wake.

Ni vema hili likawa zoezi endelevu kwa makampuni yote ya kigeni esp. makampuni ya simu na mabenki tena waanze na ile kampuni ya Orange...wamejaa raia wakigeni tena nakumbuka zile movie za wale wanajeshi wao waliokuwa wanapigana vita wengi wanafanana huku wame vaa makofia ya pama ya duara. Kampuni imejaa kwa mamia raia wa "V8-naaaammm"

Welldone Kamishina mpya wa uhamiaji, lakini peleka watu pale. msidanganywe na orange kuenea nchi nzima mpaka vijijini. Mofisa wetu waende kutetea watanzania wanao nyanyaswa pale kazini. Mtu kapata ajali na gari ya kazini. Mzungu raia wa nje hataki hata gari ya office ibebe mwili wa marehemu.Inapelekwa car wash. Anasema ndg za marehemu wakakodi gari magari yao hata pick-up haikununuliwa kubeba maiti za watu weusi, Na office wanasema hatuna bajeti ya watu waliokufa hapo wafanyakazi wanachangishwa kukodi gari la kubeba mwili. Kwenye msiba huoni ngozi nyeupe hata moja, wakizika leo kama ni mtoto wako au mzazi au ndg kesho kazini saa moja na nusu without failure. Unless huna kazi. Huu ni unyama wa kiasi gani?

Wafanyakazi wao wa apartment waliporudikana hao wa v8..naaam wanalazimishwa kufanya 'ng.....no' humo vyumbani wakifanya usafi. mshahara mdogo sana. Nendeni muangalie contract zao je wameruhusiwa kuwepo hapa nchini wangapi na kwa kazi gani zilizo ainishwa kwenye contract je ndizo wanazo fanya? Fanyeni hivyo ili watanzania wetu wapate ajira wamejaa wageni humo wenye dharau na kejeli ya hali ya juu. pata uhalali wa shughuli zilizowaleta na kazi wanazozifanya. Barua iliyomtoa kwao imeandikwa Technical Engineer wa cellular phone. Lakini amekuja anafanya kazi kama head of market. Head of admin. Hapa Tanzania hatuna wasomi wa utawala? Hapa Tanzania mgeni yupi anayejua wapi pa kupata market kwenye nchi yetu? Watanzania tufumbue macho.

Ukituma vijana wa .com watawezeshwa fungu na hutapata majibu pale kuna kamchezo nenda mwenyewe au mnasubiri Mh.Mkuu wa mkoa aende halafu watu waseme anafanya kazi ambayo si yake? ninyi wenye kazi zenu nendeni kwa hao foreignors investors. Kama hamuendi taarifa zitamfikia RC halafu muanze kulalamikal ameingilia majukumu yenu fanyeni.....TRA wapite pale je kodi yetu inalipwa sawasawa? Uhamiaji wapite pale uhalali wa wale wageni over 300, Wizara ya kazi na ajira wapite pale zile contract za ajira kwa wafanyakazi, malipo ya skilled & non skilled labour walizokubaliana zinafuatwa? Msikubaliane jambo halafu hakuna ufuatiliaji.......
 
wageni wameshikilia sana ajira hapa kwetu Tanzania, nadhani waandae operation maaalumu ya kuwapunguza wageni.
 
Wameajiriwa na Manji nyumbani kwake au wameajiriwa na Quality group?
Nani ana shitakiwa hapo? Wajuzi wa sheria mtuweke wazi
 
Hawa jamaa bana. nakumbuka wale wa dangote walipewa vibali vya muda wakiwa wanaendelea kusubiri kushughulikiwa vibali vya moja kwa moja. sasa hapa naanza kuamini yakua ku na chuki binafsi kati ya manji na hii awamu, manji kaajiri zaidi ya watz 5000, cjajua dangote km inafika hiyo idadi, manji analipa kodi, cjajua km dangote keshaanza kulipa hiyo kodi namaana km keshamaliza grace period. kuna kitu hapa. Nadhani kwa sasa manji afunguke ili tujue nadhani ndio itakua salama yake ila akikaa kimya hatuwezi jua. ni ndoto tu nimeota.
Una maono makali sana
 
Anaitwa kama nani, huyu manji si alosha staafu quality group na kubaki mshauri. Kwanini wasimwite muhusika mwenyewe?Sasa tunaanza kujikanyaga wenyewe. Na dalili zote za visasi zinaonekana
 
Safi sana serikali ya magufuli kwa kuonyesha nia ya kumshughurikia huyu mdosi mavi,mm siwapendi kabisa hawa asians people.nimefrah sana kuona mnaanza washughurikia hawa wanyonyaji njii hii
Usimchukie kwa sababu ni Asian huo ni ubaguzi ni unaoneka hapo ulipo hata mlo wa mchana hujala na isitoshe uzeeni lazima utakuwa mchawi tu
 
Hutusemi mtu akivunja sheria asishughulikiwe ila kumchukia tu mtu kisa ni tajiri na kuanza kutumia siasa kumshughulikia kwa mgongo wa sheria hyo haikubaliki Kabisa.

Hao uhamiaji walikuwa Wapi siku zote wasimfuatilie kuhusu uhalali wa wafanyakazi wake wa kigeni kufanya Kazi ktk kampuni zake. Au Manji kampuni zake kazianzisha Jana???
 
Back
Top Bottom